BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
kwanza napenda niwashukru japo si kwa furaha wanablog hii kwani mnaonekana wenye mtazamo wa kutaka kuleta mapinduzi lakini shabaha ndiyo mbovu.
pili nimpe pole rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh. Jakay M. Kikwete kwa juhudi zake z akila siku katika kulipeleka taifa hili kule tunatakiwa japo ni wale tu wenye lensi kamili katika macho yao na ambao kichwani kuna ubongo wanaweza kulion hili.
tatu nimpe pole mzee wangu rafiki Yusufu makamba kwa kuwa sasa amekuwa kama jalala la hata watoto wadogo kumsema watakavyo. nadhani tungetumia uhuru huu kuelez aumma athari za sera kam agenda 50-50 na uzazi wa mpngo ingekuwa bora.
tatu nawapa pole wana blog hii walioigeuza kambi ya kupigia soga za siasa za chadema na kuwa msumari wa moto kwa ccm kwa hapo tumepoteza mwelekeo.
leo nakuja na hoja amabyo nitaitambulisha tu kisha nitaiacha hewani. hivi ni wapi na ni nchi gani ambayo watu wake wana uhuru wa kumsemea lolote mtawala wa nchi. najua ni uhuru lakini uhuru usio na mipaka ni vurugu. leo hii kila mmoja anaamua tu kusema mara hosea, mara mwanyika, mara oooooh fisadi fulani kama tunaishi nchi ya KICHAA iliyo katika tamthilya ya MFALME JUHA. hakuna cha wasomi wala wakulima wote tu tumepoteza maana ya blog hii.
wana blog hii wengi hawana uhakika wa yale wanayoyasema na ndiyo maana wameficha majina yao. nadhani ingekuwa ni vema kama tungejuana kwa majina kamili na kule tunaishi au kufanya kazi badala ya haya mwanakijiji, mpenda nchi na mengine kama hayo.
hakuna haja ya kuwa na watoa maoni ambao wameficha nyuso zao, ni watu wasio na ujasiri, ni sawa na shule ya msingi ambako darasani kuna kijana mkorofi lakini pia ni mbabe na msumbufu darasani, ikifika mwalimu wa zamu anauliza ni nani mkorofi kila mmoja huinama na kutaja jina la yule mkorofi ilimradi tu jina litajike, si una ujasiri wa kutaja? simama watu wakuone sema ni JUMA mkorofi naye akuone ajue hhakika huyu ni shujaa kanitaja.
huu sasa ni ujinga hatuwezi kuendelea kusema Rais hajafanya lolote kwa vile Lipumba kasema, ikiwa kikwete hafai kugombea 2010 basi akigombea msimpe kura msiwe vibaraka wa wale wanaowatumikisha pasipo kujua.
blog hii iliaanza nyakati za uchaguzi na miongoni mwa memebrs wa humu 90% walitoka kule na ni wengi waliompigania kikwete achagulike kutoka kura za maoni, mimi falesy nilkuwa kinyume na kikwete lakini leo hii ni rais wa jamhuri ya muungano, biblia inasema usiwasemee vibaya wakuu wa watu wako. Kikwete ni mkuu wa watu wangu watanzania hata siku moja siwezi kumsemea vibaya. MNA LAANA NYIE MNAOMSEMA VIBAYA RAIS KILA KUKICHA NA LAANA YENU HAITAPONA HATA VIZAZI VYENU VITATU NA VINNE. tafadhali sana najua mna jazba na RAIS lakini isiwe kila kukicha mnatafuta kumgombanisha na wananchi kama hawafai basi subirini 2010 msimchague.
na hao kina lipumba na slaa wanona hafai basi wasubiri 2010 wagombee washinde hapa jamani ni jukwaa la mawazo huru ya kujenga taifa hili si jukwaa la kujadili maamuzi ya Rais yapi afanye, yapi alitakiwa afanye na nani na nani wawajibishwe kama mnataka kasomeeni sheria na mfungue mahakama zenu na muanzishe majeshi yenu ya polisi muwakamate hao mnaotaka wakamatwe. pumbafuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Ha ha ha ha ha Mpumbavu mwingine kapandikizwa hapa na watetezi wa mafisadi na si ajabu mwenyewe pia ni fisadi. Adabu wewe umeifahamu tangu lini? Unaweza kutupa definition ya adabu kama unavyoifahamu wewe?
Au adabu kwako wewe ni kukaa kimya wakati mafisadi akina Mkapa, Manji, Rostam, Chenge, Subhash Patel, Jeetu, Karamagi, Idrissa, Yona na wengineo chungu nzima wakiendelea kupira urajiri wa Watanzania kwa mabilino wakati asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi kwa maisha ya ufukara wa kutisha? Au unataka tukae kimya kuhusu utendaji dhaifu wa Kikwete ambaye aliingia madarakani kwa kutumia mabilioni ya mafisadi ndiyo utaona tuna adabu?
Kwa hiyo kwa akili yako finyu hata Viongozi wa dini zetu mbili kubwa wanaosema kwamba nchi inaenda mrama, na viongozi wa zamani kama Warioba, SAS, Butiku na wengineo wengi wanaosema mwelekeo wa nchi hauridhishi nao hawana adabu! ila mwenye adabu ni wewe tu mtetezi wa mafisadi mwenye adabu ya woga unaogopa hata kuhoji chochote kile kinachohusiana na uongozi mbovu wa Kikwete!
Waungwana, hivi ndiyo viroja tutakavyoviona kuelekea 2010. Wewe mwenye adabu kaa na adabu yako na siye tusiokuwa na adabu tuache tufanye vitu vyetu.
