The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Imeelezwa kuwa Wananchi wengi hawana uhakika kuhusu matumizi ya mapato yatokanayo na tozo kwani 42% wanasema kuwa hawajui yanatumikaje ikilinganishwa na 38% ya wanaosema wanajua namna mapato hayo yanavyotumika.
Hii ni kwa mujibu wa Ripoti mpya ya Shirika lisilo la Kiserikali la TWAWEZA ambalo limefanya uzinduzi wa matokeo ya utafiti mpya wa Sauti za Wananchi ambao umeangazia maoni ya Wananchi kuhusu uchumi kwa jumla na hasa tozo ya miamala ya pesa kwa njia ya simu.
Takwimu hizo ambazo zimekusanywa kutoka kwa wahojiwa 3,000 kuanzia Oktoba na Novemba 2021 na Juni na Julai 2022, pia zianaonesha kuwa Wananchi wanaonesha dalili kuwa wangeunga mkono zaidi Tozo hizo iwapo wangekuwa na taarifa kamili kuhusu matumizi ya Fedha zinazokusanywa.
Asilimia 63 wanasema wangekuwa tayari zaidi kulipa tozo iwapo wangeweza kufuatilia matumizi, huku asilimia 39 wanasema wanajua pesa zinatumikaje.
Je, unajua mapato ya Tozo yanapokwenda?