Watanzania, hususani wa Dar, tuache ulimbukeni wa kuagiza watu mizigo isiyo na tija watu wanaposafiri

Watanzania, hususani wa Dar, tuache ulimbukeni wa kuagiza watu mizigo isiyo na tija watu wanaposafiri

Niliwahi kutumwa miche ya sabuni nipeleke kijijini kwa wazazi wa mshkaji mmoja. Nilichofanya niliiacha geto kwangu nikaenda mpaka bush nikanunua kwenye kiosk nikawapelekea.

Niliporudi wazazi wa mshkaji wakanituma debe la maharage, nikayaacha home kwetu nikaja mpaka dar nikamwitisha mshkaji kufika geto kwangu akamaindi kuona miche ya sabuni aliyonituma imelala geto, nikampeleka sokoni nikanunua debe la maharage nikamtwisha na kumwambia ni zawadi ya wazazi wake baada ya kuwapa miche ya sabuni uliyowatumia. AKAEREWA

Sijui na nyinyi MMENIEREWA? Sitaki ujinga kabisa
Ha ha ha umetisha..ila mandondo ya kijijin na mjin mengine hapo tofauti
 
Nichukulie Machungwa Tanga Angalia Wasikupe Mabovu[emoji45][emoji45][emoji45][emoji45]
 
Inategemea ....inawezakana kikijin kwenu kuna njaa ..na wewe mtoa mada unaonekana una njaa sana ...sisi kijijin kwetu ukika kuondoka unapewa kuku kama 10 ...sasa hapo unawaachaje si bora uwauze ...ili... au wakuukangie ....then mtu kukupa zawadi ...ni Kama ameamua kupay back ...kwasababu unapokwenda kumtembelea kijijin.... anaona umemthamin...kwaiyo ni kama na yeye anapoamua kukupa kijizawadi ...nikama anaamua kulipa Fadhila....ila kiukwel wewe mtoa mada inaonekana ...kijijin kwenu kuna Njaa sana.

Acha ujinga wewe, Maisha yangu yote tangu nikiwa mtoto hadi leo over 30s sijawahi kushuhudia njaa wala kula milo miwili au mmoja. Tunavuna mwaka mzima, tena varieties za vitu. Zao pekee ambalo halistawi kwetu ni mpunga tuu kwa sababu ya hali ya hewa ya baridi na milimani... Mengineyo mazagazaga yote yamejaa tele, mahindi, maharage, karanga, viazi mviringo, vitamu, ngano, mihogo, ndizi aina zote, miwa, matunda aina zote, njegere na mengineyo, utajumlisha mwenyewe. Mifugo ndo usiseme imejaa. Sana sana kila mwaka lazima nishuhudie kuona watu wakija from other places kuja kuhemea kwetu. Acha dharau kama kitu hujui bora uulize. Asilimia 50 ya viazi vitamu kwetu ni chakula cha nguruwe na siyo binadamu.
 
Hao wanaokuagiza uwaletee ni Sawa hawafanyi vizuri na una haki ya kunung'unika lakini nikwambie tu mtu anayekupa mzigo upeleke kwako anakuwa kakudhamini sana nashaa unachukia dhamani mtu anayokuonyesha na huwa hawakupi wewe wanasema wapelekee watoto na familia wanajua mjini vipo lakini wanakupa kama shukrani ya kuwatembelea wakati wewe unashishindwa kubeba kwenye gari wasio na magari wakipewa wanabeba kichwani wakiwa na furaha tele

Hujanielewa bado. Hakuna sehemu nimesema mimi mchoyo na wala sipeleki zawadi. Mimi ndiye ninayeamua nipeleke nini kwa muktadha wa sehemu ninayoenda. Kama kwetu hatulimi mpunga, nachofanya napiga safari yangu nikifika home kabla sijafika nyumbani kabisa nanunua mchele mjini napeleka home hapo ni kama 20 km. Watashukuru kwa sababu nimepeleka kitu ambacho kk mazingira yao hawana, na hata pale niliponunua kimeletwa from other place.

My point ni kwamba utabebaje mzigo mzito mwendo mrefu wakati hicho unachobeba kipo huko uendako? tumia akili
 
Niliwahi kutumwa miche ya sabuni nipeleke kijijini kwa wazazi wa mshkaji mmoja. Nilichofanya niliiacha geto kwangu nikaenda mpaka bush nikanunua kwenye kiosk nikawapelekea.

Niliporudi wazazi wa mshkaji wakanituma debe la maharage, nikayaacha home kwetu nikaja mpaka dar nikamwitisha mshkaji kufika geto kwangu akamaindi kuona miche ya sabuni aliyonituma imelala geto, nikampeleka sokoni nikanunua debe la maharage nikamtwisha na kumwambia ni zawadi ya wazazi wake baada ya kuwapa miche ya sabuni uliyowatumia. AKAEREWA

Sijui na nyinyi MMENIEREWA? Sitaki ujinga kabisa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] duuuh wee jamaa ni noma sana ulisimplify
 
MI ndio maana nikiwa natoka mbeya naenda mkoani sitoi taarifa, maana utajuta. unaweza kuhisi genge linatembea
 
Leta mapera tule wacha porojo,bob..[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hujanielewa bado. Hakuna sehemu nimesema mimi mchoyo na wala sipeleki zawadi. Mimi ndiye ninayeamua nipeleke nini kwa muktadha wa sehemu ninayoenda. Kama kwetu hatulimi mpunga, nachofanya napiga safari yangu nikifika home kabla sijafika nyumbani kabisa nanunua mchele mjini napeleka home hapo ni kama 20 km. Watashukuru kwa sababu nimepeleka kitu ambacho kk mazingira yao hawana, na hata pale niliponunua kimeletwa from other place.

My point ni kwamba utabebaje mzigo mzito mwendo mrefu wakati hicho unachobeba kipo huko uendako? tumia akili
Nilikuelewa vizuri tu nisome tena hàkuna sehemu nimesema wewe mchoyo
 
Back
Top Bottom