joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Hiyo pesa haikupotea siku moja, ni kwa kipindi cha miaka mingi kwa kupitia usafirishaji wa makinikia walikua wanadanganya kwamba ndani kuna kiasi kidogo cha madini kumbe ni kiasi kikubwa, ni kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi au zaidi, sio kwamba hiyo pesa wanayo...wewe ni kati ya waliodanganywa.
..barrick ndiyo walioanzisha/waliounda kampuni ya acacia.
..na walipounda kampuni hiyo waliuza hisa chache, wakabakiwa ya 64% ya hisa.
..kwa hiyo ulangai na ujanja-ujanja wa kwanza kabisa ni barrick kujidai wao ni wasafi na acacia ndio wezi au wachafu.
..na serikali ndiyo walikuwa vinara wa uongo na propaganda kwamba barrick wana nia njema na waTanzania.
..huwezi kusema acacia wameshindwa kulipa? How? serikali itueleze usd 191 billion walizoiba acacia zimekwenda wapi? hiyo siyo hela ya chenji inayoweza kupotea kirahisirahisi.
..sijui kama unaelewa tofauti kati ya usd 191 billion na usd 300 million. Nakuomba uchukue calculator yako ujaribu kulinganisha viwango hivyo viwili. Ukishindwa nitakusaidia kukuelewesha.
Ni sawa na kumuweka mfanyakazi wako dukani na kila siku akawa anaiba mia tano, baada ya miaka kumi ukapiga hesabu ukakuta jumla ya pesa aliyoiba ni million 200, hiyo haina maana kwamba anazo hizo pesa, alikua anaiba na kuzitumia.