Th3the
JF-Expert Member
- Aug 6, 2014
- 1,327
- 1,779
Wakuu
Ipo siku sisi kama watanzania tutaruhusu nchi yetu iingie katika kipindi kigumu zaidi Cha kiutawala ambapo tutajikuta tumeruhusu kutawaliwa na mtu asie mtanzania halisi bila sisi kujijua kwa sababu tunaonekana hatuna uzalendo kabisa.
Imefikia wakati watu Wanapenda vyama kuliko kuipenda nchi yao, yaani ni Bora nchi iharibike kuliko vyama vyao kupotea.
Vyombo vya ulinzi na usalama vimegeukia kulinda watawala na kuwapa mamlaka makubwa pasipo kujali Wala kukumbuka jukumu la kuu la kulinda nchi na maslahi ya nchi.
Mihimili yote ya nchi( bunge na mahakama)imehodhiwa na kunajisiwa wa kikundi kidogo Cha watu wasio wazalendo, wasio angalia maslahi ya kizazi Cha sasa na kizazi kijacho Cha watanzania.
Matukio yanayoendelea sasa yanatisha sana na kufikirisha sana, democrasia inachezewa bila woga, utekaji Kila kukicha huku watu wakifungwa midomo wasipaze sauti zao.
Je kama watawala ambao ni watanzania wenzetu wanatufanyia hivi, je siku akiingia mtu asie mtanganyika itakuwaje? Au sisi kama watanzania kama hatuwezi kudhibiti watanzania wenzetu tuliowapata dhamana ya kiutawala, je huo utabiri ukitimia tutaweza kumdhibiti raia asiye mtanzania kututawala, kuiba Mali zetu?
Wito wangu kwa watanzania:
-inabidi tuwe wazalendo tuipende nchi yetu kwanza halafu vyama baadae.
-Vyombo vya ulinzi na usalama vielewe majukumu yake na wajibu wake wake, viache kubeba wanasiasa Wanao pita.
- Mihimili yote itambue wajibu wake na mipaka yake ili kutokurusu muingiliano wa majukumu.