Watanzania kama hatuwezi kuendesha Bandari ni kipi tunaweza? Huko CCM kuna shida gani?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari JF,

Hivi Watanzania tunashindwa kuendesha kitu ambacho hakituhitaji tuweke mtaji tutengeneze au tuuze vitu kisha tufanye hesabu ya faida tuliyopata, tutaweza kufanya kipi?

Unahitaji nguvu, tunayo ya kutosha. Unahitaji Vifaa na mitambo/mashine, uwezo wa kununua tunao. Unahitaji uweke utaaribu wa kusafirisha na kupokea mizigo, uwezo huo tunao, wateja wapo wa kutosha, tunashindwa wapi kuendesha hii Bandari ya Dar es Salaam?

Je, tutaweza endesha biashara ya ndege, treni, viwanda na nchi kwa ujumla?​
 
Habari Jf ,hivi watanzania tunashindwa kuendesha kitu ambacho hakituhitaji tuweke mtaji tutengeneze au tuuze vitu kisha tufanye hesabu ya faida tuliyopata ,tutaweza kufanya kipi ?

Unahitaji Nguvu -Tanayo ya kutosha

Unahitaji Vifaa na mitambo/ mashine -Uwezo wa kununua tunao

Unahitaji uweke utaaribu wa kusafirisha na kupokea mizigo -Uwezo huo tunao

Wateja-wapo wa kutosha

Tunashindwa wapi kuendesha hii bandari ya Dar es Salaam?

je tuataweza endedha biashara ya ndege ?treni ,viwanda na nchi kwa ujumla ?​
Kwani CCM ni kipi washawahi ku archive? Washawahi ku manage kipi wakafaulu?
 
Tatizo linakuja Kuna mapapa halafu Kuna njaa!.. mkuu hivi ulishawahi kumpa hotpot la chakula mtu mwenye njaa alisafirishe unafikiri litafika..?

Tumeendekeza njaa huku tukisahau faida tutakayoipata tukifika kileleni!, wachache waliopata dhamana ya kuhudumu ni wabinafsi sio wazalendo wanatanua mifuko yao.. kiujumla bandari ni mwanamke mnono Kila atakaepewa amuendeshe anakosa namna ya kujizuia anamla!.. mkuu huenda hata wewe ukashindwa maana upo zako ofisini mara anakuja mtu na libahasha Lina million mia anataka apitishe magendo yake! Sasa utaacha nawakati umasikini unakuta umekupiga kabari..😅
 
Kwani CCM ni kipi washawahi ku archive? Washawahi ku manage kipi wakafaulu?
Hakuna hata kitu kimoja, yan hawawezi hata kitu kimoja, sijawah kuwadharau CCM kama kipindi hichi, alafu kwanini haya mambo yanafanywaga siri? Kwanini wasiwe wanatangaza na maspika ili watanzania wote wakisikia wajue linaloendelea wajue wafanyaje? Mbona kipindi cha kampeni kila kitu wanakisema hadharani, nimeyachukia sana majitu ya ccm na huu muungano ni hopeless kabisa bora tubaki wenyewe... HAPA BILA KATIBA MPYA HATUTOBOI...
 
Kazi zote Tanzania pamoja na nafasi za uongozi zingepatikana kwa kupima uwezo wa watu tungeweza. Wewe jiulize huyo mkuu wa TPA ni nani?? Alipatikana kwa vigezo vipi? Kabla ya hapo alikuwa na uzoefu gani kwenye masuala ya bandari na uongozi??

Utaambiwa ooh sijui usalama wanafanya upekuzi na kupendeza watu, ni mfumo wa kijinga ambao ni rahisi kuuchezea. Hauwezi kupata watu sahihi bila kuwa na mchakato wa wazi na wa haki.

Hakuna miujiza, ukiwa na mfumo mbovu wa kugawana vyeo kwa fadhila na kupenyeza majina ya watu hauwezi kufika popote. Hata waliopo kwenye hizo nafasi hawana ujasiri wa kufanya lolote la maana kwasababu muda wowote fadhila inaweza kuondolewa.
 
Hakuna hata kitu kimoja, yan hawawezi hata kitu kimoja, sijawah kuwadharau CCM kama kipindi hichi, alafu kwanini haya mambo yanafanywaga siri? Kwanini wasiwe wanatangaza na maspika ili watanzania wote wakisikia wajue linaloendelea wajue wafanyaje? Mbona kipindi cha kampeni kila kitu wanakisema hadharani, nimeyachukia sana majitu ya ccm na huu muungano ni hopeless kabisa bora tubaki wenyewe... HAPA BILA KATIBA MPYA HATUTOBOI...
Kamwe haiwezekan kuweka mikataba wazi maan kuna some interest humo, cz kama ni mikataba yenye maslahi kwa Taifa always wangekua wanaweka wazi!!
 
Habari JF,

Hivi Watanzania tunashindwa kuendesha kitu ambacho hakituhitaji tuweke mtaji tutengeneze au tuuze vitu kisha tufanye hesabu ya faida tuliyopata, tutaweza kufanya kipi?

Unahitaji nguvu, tunayo ya kutosha. Unahitaji Vifaa na mitambo/mashine, uwezo wa kununua tunao. Unahitaji uweke utaaribu wa kusafirisha na kupokea mizigo, uwezo huo tunao, wateja wapo wa kutosha, tunashindwa wapi kuendesha hii Bandari ya Dar es Salaam?

Je, tutaweza endesha biashara ya ndege, treni, viwanda na nchi kwa ujumla?​
Kama tumeshindwa kuiendesha na kuisimamia bandari yetu basi hakuna haja kuendelea kununua ndege za kibiashara. Nani atazisimamia?
Mimi naona hata liinchi lote tulibinafsishe uarabuni.
 
😆😆😆😆
 
Now you're talking, wezi hawa viongozi... Mwanangu bila katiba mpya hatutoboi... Yan haiwezekani
Ni ukwel usiopingika! Hata wao wanajua that's why hawataki kusikia wimbo wa katiba mpya yaan ni chukizo kwao!! Ingawa hakuna kisicho na mwisho.
 
Habari JF,

Hivi Watanzania tunashindwa kuendesha kitu ambacho hakituhitaji tuweke mtaji tutengeneze au tuuze vitu kisha tufanye hesabu ya faida tuliyopata, tutaweza kufanya kipi?

Unahitaji nguvu, tunayo ya kutosha. Unahitaji Vifaa na mitambo/mashine, uwezo wa kununua tunao. Unahitaji uweke utaaribu wa kusafirisha na kupokea mizigo, uwezo huo tunao, wateja wapo wa kutosha, tunashindwa wapi kuendesha hii Bandari ya Dar es Salaam?

Je, tutaweza endesha biashara ya ndege, treni, viwanda na nchi kwa ujumla?​
Kuendesha bandari kwa tija katika dunia ya sasa anahitajika mtu mwenye taaluma ya uchumi na uzoefu wa uendeshaji wa biashara za kimataifa.

Hizi sio nyakati za kupeana vyeo nyeti kisiasa, mtu hana uzoefu wa biashara ya aina yoyote anapewa ukurugenzi wakati hana uzoefu wowote ule wa kusimamia miradi mikubwa.

Siasa zimeharibu tija ya bandari tena miaka na miaka.
 
Watu wanaifilisi nchi halafu wanajificha kwenye kivuli cha zile timu pacha za mitaa ya kariakoo na maujinga mengineyo!!
 
Back
Top Bottom