Watanzania kuweni makini na matapeli hawa wakubwa, waliojificha kwenye kutoa Elimu ya Biashara


Na wewe anzisha thread yako utapata support mkuu. Si lazima wote tufanane mawazo. Si kila mwenye fikra tofauti ni "mburula".
 
Mleta mada,

Tatizo ninaloliona hapa ni wewe kuwa kinyume na mfumo wetu wa sasa wa maisha. Kwa maana nyingine, wewe unaishi kijima sana!

Dunia ya leo jinsi ilivyo ni kwamba, kama mimi ni mfanyabiasha au mtoa huduma, na kama hakuna msimamizi (regulator), basi nina uhuru wa kuchagua bei ninayoitaka ya bidhaa zangu!

Hapa Tanzania kuna private investigator, unajua kwa huduma moja wanatoza kiasi gani!? kwa ushamba wako ukijua unaweza kufanya maandamano ya haraiki!

Aidha, semina iwe ya Milioni moja, milioni kumi, it doesn't matter, what matters is that people are the ones to decide which among of the seminars held in town they wanna go to. So, kama mimi nafikiri it worth it kutoa milioni moja na kupata ujuzi utakao nitengenezea milioni 10 zaidi kwa mwezi, why not paying for that!

By the way, huko mitaani zipo mpaka seminar za bure. Je, it worth kwenda kwenye hizo seminar? Mimi sijui, watu wanao kwenda ndio wanatambua hilo. Lakini zipo hadi seminar zina charge $ 350 - 500 hapo Kenya na watu wanaenda. So, it all about choice!

Lakini sio vyema mtu tu upo kwenye bench huko mtaani kisa umepata access ya internet na uwezo wa kutype kwenye Tecno yako basi uanze tu kuwaita watu wengine matapeli na unafanya hivyo bila kuambatanisha ushahidi wowote usio na shaka kwa hizo tuhuma zako! Huo ni upuuzi na mtu mzima mwenye akili nzuri hawezi kufanya hivyo!

Halafu katika kuhalalisha upuuzi wako unasema " mimi siachi kufanya kile ninacho kiamini ni sawa!" Hivi una akili nzuri wewe? Wapo wenzako wajinga kama wewe wamefanya mauaji (cold blood), niliwauliza kwanini mmefanya hayo, wakasema waliamini wanafanya jambo sahihi. Kwa sasa wanaozea jela!
..................
Binafsi sina mahusiano yoyote na hizo seminar ijapokuwa nakiri kuhudhuria baadhi na niseme tu nimefaidika nazo sana katika kuyaendesha maisha yangu.
 
Dola 700 kwa siku moja hiyo ni balaa,atakua amatafuta mtaji kupitia migongo ya watu,hawezi kua na jipya kwenye hiyo semina zaidi ya kutoa historia na ndoto zisizotekelezeka....kutoa mifano kibao mpk siku inaisha...
 
Kweli dola 700 kwa siku ni wezi hao kaa mbali
 
HAMY-D

Kasema kweli mleta mada, sasa kama inalenga wenye pesa ikawafate huko mafanikio mafisadi, kipi kipya katika izo seminar hakijawai kuandikwa? Kila siri ipo katika vitabu, leo eti watanzania maskini wanaoishi chini ya dollar 1 umwambie dollar 700? Seminar

Ni wezi, ni. Majambazi labda kama iyo seminar wanafundisha jinsi yakuuza unga bila kukamatwa, ila hata aje billgate naimani semina zke zitakuwa na yaleyale wanayosema na kuandika katika vitabu kila siku.

Then seminar ni maandiko tu sio reality unaweza pigwa brash na ukatoka ukawa maskini kama wewe ivo ivo milele.
 
Last edited by a moderator:
Mtu anavuta harufu ya utapeli hutaki atuonye! We kama unaona sawa kajiunge kwenye semina hukatazwi, lakin usikataze watu kutoka ushauri wao
 

Mkuu,

Siku zote elimu inapotolewa, suala la matokeo ya ulichojifunza, hilo utaamua wewe uliyejifunza.

Ndio maana leo hii kuna shule kama IST ada yao ni TZS 11 Milioni kwa mwaka na wapo wanafunzi wana feli. Vilevile kuna Fedha boys, ada TZS 5 milioni kwa mwaka na wapo wanao faulu pia wanaofeli wapo.

Pia kuna shule kama Green acres ada ni Milion 1.2 tu utakuta wanao faulu na wanao feli.

Hiyo mifano yote ni kukuonyesha kuwa, it's a free world, full of choices and options. Wala halazimishwi mtu kufanya maamuzi. Na kama huwezi wewe, wapo wanao weza. In fact, Mtanzania mwenye uwezo wa kutoa Laki 7 sio sawa na wewe kiakili kabisa.

Wewe hapo laki saba unaona pesa, ila kuna watu hiyo ni bajeti ya vocha kwa mwezi. So, tuna vipato tofauti, matumizi tofauti, mipango tofauti. Sio kisa wewe una njaa na uwezo mdogo wa kufikiri, basi ukadhani JF members wote wapo sawa na wewe. No, we differ!

Mfano mwingine, hata humu JF kukudhihirishia kuwa kuna classes au matabaka, kuna watu ni Gold member, kuna Tanzanite na hadi Platnum members! Unadhani hizo status unapewa bure!? Ni pesa tu ndio itakuweka kwenye kundi lako.

Yani Watanzania ujamaa umetuathiri sana, yani kwenye seminar laki 7 inaonekana nyingi hadi kuitana matapeli!!! Na utakuta katika hiyo laki 7 kuna huduma ya chakula pia. Bado ni nyingi tu?

JF matajiri wapo; maskini mpo na pia wenye vipato vya kati tupo. Hivyo mtu yeyote hakatazwi kuweka chochote humu as long as hakivunji taratibu na miongozo yetu tuliyojiwekea.


Kama wewe ni maskini na unaogopa kulipia elimu, basi baki na umaskini wako + Ujinga. Waacheni wengine wanaoona umuhimu wa elimu itolewayo kwenye seminar regardless of the entry fee, waende.
 
Huu ni utapeli tu,$700 hata mkiutetea vipi. Maana kuna watu wanautetea na kutoa mapovu kabisa.

Robert Kiyosaki(Rich Dad Poor Dad) mwenyewe anafanya semina kwa $99 tena kwa "VIP" tickets,sembuse hapa Tanzania! ukiangalia ni zaidi ya mara saba ($700/99) na ukitaka zaidi ($295). Sasa kufanya semina $700 hapa Tanzania ni utapeli wa wazi kabisaa.[h=1]
Robert Kiyosaki Live - 'Masters of Wealth'
[/h][h=2]Fast Track Your Fortune with Tips and Tricks from the Leaders in Finance! Only $99 for a VIP Ticket to the 'Masters of Wealth' Seminar featuring Highly-Acclaimed Financial Analyst, Forecaster and Author Robert Kiyosaki. Learn How to Invest, Generate Multiple Streams of Income, the Secrets of Entrepreneurial Success and Much More. Valued at $295)[/h]
Angalia hapa taarifa kamili -->Robert Kiyosaki Live - 'Masters of Wealth' Deals. Unbeatable Daily Deals on Cudo.
 

Shida yako ni ni hasa.Muache mwenzio awasilishe mawazo yake kila mtu atachambua mwenyewe.
 
Next time unapowasilisha mawazo yako epuka ktumia lugha ya ya kuwadhalilisha wengine kwa kuwahukumu kwamba ni wezi au matapeli. Jifunze kujenga hoja kuepuka kuwa trashed

Mkuu wewe ndiyo umeandaa hiyo event/seminar? Maana naona unatumia nguvu nyingi kutetea hoja yako. Ninachojua hata hizi Taasisi/Kampuni zinazofundisha Ujasiliamali nao pia ni wajasiliamali wanatengeneza pesa, wanatafuta watoke vipi. 700usd ni nyingi kwa level ya watu wa chini laki kwa watu wengine ni ndogo, maana watu wa aina hii mbali na hayo mafunzo huwa wanakwenda kupanua mtandao wa marafiki wafanyabiashara. Ushauri wangu ni kwamba mtu afanye kitu ambacho ana uwezo nacho.
 
Huyo mwenye seminar mwenyewe anafundisha asichokijua kuki apply ,hajui pricing ndo ina drive kila kitu
Pricing inaendana na kipato cha watu ,so hana kitu kipya cha kufundisha maana hilo ni badhi ya mapungufu.na kudhihirisha wahudhuriaji watarajiwa kwamba ni utapeli mtupu.
 
Duh..700 nyingi sana. Washiriki mafisadi ila sie wengine utakuwa unatuibia kabisaaaaa.
 
Money Stunna na wenzako acheni kutoa povu kuhusu tozo la hiyo semina. Ungekuja na ushahidi wa packages za hiyo semina hoja yako ingekuwa na mashiko zaidi.
Halafu pengine muandaaji ameandaa hiyo semina kwa class flani za watu so mwenzangu na mimi kapuku usitie maguu hapo. Na mwisho wa siku ni kwamba kila mtu hapa anakiri kuwa semina hizi ni chachu ya kuyafikia malengo ya kila mtu atakaehudhuria na waendao huko wanaelewa manufaa ya wanachoenda kujifunza.
 
Last edited by a moderator:
Wewe unaleta ubishi tu na ligi ,na huelewi kabisa nimesema sijamshikia bunduki hasiende,natoa mawazo yangu kwa kile ninachoona sahihi kulingana na kipato cha wananchi walio wengi,hivi unajua Tanzania ni nchi masikini zaidi duniani?

Acha mambo ya kugeneralize kuwa TANZANIA NI NCHI MASKINI DUNIANI; hii ni nchi tajiri sana maskini ni wewe na nduguzo wenye mawazo mgando kwani hamchangamkii fursa zilizopo nchini mmebaki kuwa omba omba!!! Huna habari kuwa kuna mabilionea nchi hii, sasa hao nao maskini? Wewe kama unaona $700 nyingi sana basi wenzio hizo ni fedha za kunywea kahawa na wapo nchi hii hii!!
 

Ok Tanzania ni nchi Tajiri duniani,umefurahi sasa,sina muda aw ubishi
 
Ok Tanzania ni nchi Tajiri duniani,umefurahi sasa,sina muda aw ubishi

Ndio hii nchi ni tajiri na wanaoufaidi huo utajiri ndio hao wanaoweza kulipa $700 na kwenda kwenye hizo seminar!! Wengi wetu huo utajiri wa nchi tunausikia tu kwenye majarida na takwimu!!
 
Mkuu Money Stunna, heshima yako mkuu.

Mimi nafikiri hujakosea kuleta wasiwasi wako kuhusu hio $700 kama tozo ya kila kichwa cha mwanasemina.

Lakini ilikuwa ni vizuri ungeleta mchanganuo wa gharama nzima kuhusu hio semina kwamba wapi inafanywa , chakula, maji au maji ya matunda vifaa kama laptop na Project yake na kadhalika.

Unaweza kukuta ndio inafikia labda $500 au 600 na hio $100 inakuwa faida ya muendesha semina.

Hakuna mwendesha semina asielenga kupata chochote katika kuuza mawazo yake.

Hata wewe kama unataka kufanya "after dinner Speech" au tu semina yoyote ile utaangalia matunda yake baadae na itakua ni kiasi gani umepata kama faida.

Hvyo chunguza tena ikiwezekana lipa hio $700 ujifunze mwenzio mwendesha semina anawezaje kupanga hio semina yake na jinsi ya kutoka kivyako na wewe.
 

Kaka usipoteze muda kubishana na huyo mjinga
 
Na wewe anzisha thread yako utapata support mkuu. Si lazima wote tufanane mawazo. Si kila mwenye fikra tofauti ni "mburula".

Wewe unatetea ujinga na hujui unachokitetea. Sijatukana fikra zake. Kilichoniudhi ni kukurupuka kwake na kuanza kuita watu wezi na matapelio. Sina interest na hii semina lakini pia siwezi kaa kimya mtu anapoongea vitu bila facts na huku akitukana wengine ni matapeli. Kabla ya kuita watu matapeli angeweka break down of how yeye anaweza akaorganize the same seminar at much cheaper price. Acheni kukariri maisha. Jifunzeni kuwa objective katika kujadili mambo. Kama unataka usitukanwe changia kama mtu mwenye akili. Ukichangia kama umekunywa komoni utaishia tu kuambulia matusi. Sisemi kwamba mawazo yangu ndo sahihi.Nachosema ni ajifunze kujenga hoja kwa facts bila kukurupuka tu na kugeneralize vitu ambavyo huna uelewa navyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…