Kasema kweli mleta mada, sasa kama inalenga wenye pesa ikawafate huko mafanikio mafisadi, kipi kipya katika izo seminar hakijawai kuandikwa? Kila siri ipo katika vitabu, leo eti watanzania maskini wanaoishi chini ya dollar 1 umwambie dollar 700? Seminar
Ni wezi, ni. Majambazi labda kama iyo seminar wanafundisha jinsi yakuuza unga bila kukamatwa, ila hata aje billgate naimani semina zke zitakuwa na yaleyale wanayosema na kuandika katika vitabu kila siku.
Then seminar ni maandiko tu sio reality unaweza pigwa brash na ukatoka ukawa maskini kama wewe ivo ivo milele.
Mkuu,
Siku zote elimu inapotolewa, suala la matokeo ya ulichojifunza, hilo utaamua wewe uliyejifunza.
Ndio maana leo hii kuna shule kama IST ada yao ni TZS 11 Milioni kwa mwaka na wapo wanafunzi wana feli. Vilevile kuna Fedha boys, ada TZS 5 milioni kwa mwaka na wapo wanao faulu pia wanaofeli wapo.
Pia kuna shule kama Green acres ada ni Milion 1.2 tu utakuta wanao faulu na wanao feli.
Hiyo mifano yote ni kukuonyesha kuwa, it's a free world, full of choices and options. Wala halazimishwi mtu kufanya maamuzi. Na kama huwezi wewe, wapo wanao weza. In fact, Mtanzania mwenye uwezo wa kutoa Laki 7 sio sawa na wewe kiakili kabisa.
Wewe hapo laki saba unaona pesa, ila kuna watu hiyo ni bajeti ya vocha kwa mwezi. So, tuna vipato tofauti, matumizi tofauti, mipango tofauti. Sio kisa wewe una njaa na uwezo mdogo wa kufikiri, basi ukadhani JF members wote wapo sawa na wewe. No, we differ!
Mfano mwingine, hata humu JF kukudhihirishia kuwa kuna classes au matabaka, kuna watu ni Gold member, kuna Tanzanite na hadi Platnum members! Unadhani hizo status unapewa bure!? Ni pesa tu ndio itakuweka kwenye kundi lako.
Yani Watanzania ujamaa umetuathiri sana, yani kwenye seminar laki 7 inaonekana nyingi hadi kuitana matapeli!!! Na utakuta katika hiyo laki 7 kuna huduma ya chakula pia. Bado ni nyingi tu?
JF matajiri wapo; maskini mpo na pia wenye vipato vya kati tupo. Hivyo mtu yeyote hakatazwi kuweka chochote humu as long as hakivunji taratibu na miongozo yetu tuliyojiwekea.
Kama wewe ni maskini na unaogopa kulipia elimu, basi baki na umaskini wako + Ujinga. Waacheni wengine wanaoona umuhimu wa elimu itolewayo kwenye seminar regardless of the entry fee, waende.