Mleta mada,
Tatizo ninaloliona hapa ni wewe kuwa kinyume na mfumo wetu wa sasa wa maisha. Kwa maana nyingine, wewe unaishi kijima sana!
Dunia ya leo jinsi ilivyo ni kwamba, kama mimi ni mfanyabiasha au mtoa huduma, na kama hakuna msimamizi (regulator), basi nina uhuru wa kuchagua bei ninayoitaka ya bidhaa zangu!
Hapa Tanzania kuna private investigator, unajua kwa huduma moja wanatoza kiasi gani!? kwa ushamba wako ukijua unaweza kufanya maandamano ya haraiki!
Aidha, semina iwe ya Milioni moja, milioni kumi, it doesn't matter, what matters is that people are the ones to decide which among of the seminars held in town they wanna go to. So, kama mimi nafikiri it worth it kutoa milioni moja na kupata ujuzi utakao nitengenezea milioni 10 zaidi kwa mwezi, why not paying for that!
By the way, huko mitaani zipo mpaka seminar za bure. Je, it worth kwenda kwenye hizo seminar? Mimi sijui, watu wanao kwenda ndio wanatambua hilo. Lakini zipo hadi seminar zina charge $ 350 - 500 hapo Kenya na watu wanaenda. So, it all about choice!
Lakini sio vyema mtu tu upo kwenye bench huko mtaani kisa umepata access ya internet na uwezo wa kutype kwenye Tecno yako basi uanze tu kuwaita watu wengine matapeli na unafanya hivyo bila kuambatanisha ushahidi wowote usio na shaka kwa hizo tuhuma zako! Huo ni upuuzi na mtu mzima mwenye akili nzuri hawezi kufanya hivyo!
Halafu katika kuhalalisha upuuzi wako unasema " mimi siachi kufanya kile ninacho kiamini ni sawa!" Hivi una akili nzuri wewe? Wapo wenzako wajinga kama wewe wamefanya mauaji (cold blood), niliwauliza kwanini mmefanya hayo, wakasema waliamini wanafanya jambo sahihi. Kwa sasa wanaozea jela!
..................
Binafsi sina mahusiano yoyote na hizo seminar ijapokuwa nakiri kuhudhuria baadhi na niseme tu nimefaidika nazo sana katika kuyaendesha maisha yangu.