Watanzania kuweni makini na matapeli hawa wakubwa, waliojificha kwenye kutoa Elimu ya Biashara

Watanzania kuweni makini na matapeli hawa wakubwa, waliojificha kwenye kutoa Elimu ya Biashara

Hiyo semina hakuna alieshikwa mkono kuwa uende au usipoenda unapigwa. Ni uamuzi wa mtu

Mawazo ya kila mtu nayaona kuwa sahhihi, jinsi ya kuwasilisha na kutilia mkazo ndio watu wanapotofautiana.
Kwa mfano, ukiwa unajua mtaa fulani, kama Congo, Kariakoo, kuna vibaka, naamini ni vyema kutahadharisha wanunuzi wanaokwenda maeneo hayo. Nitamshangaa mfanyabiashara wa mtaa huo atakayekutolea lugha ya kejeli, matusi, ....
Watu maskini na wasio na uelewa wanatapeliwa kwa namna nyingi ikiwaamo kuuziwa bidhaa duni kwa bei ya juu kwenye shopping malls, semina elekezi zisizokidhi mahitaji, ...
Tushindane kwa hoja!
 
Freelancer

Wewe unaleta ubishi tu na ligi ,na huelewi kabisa nimesema sijamshikia bunduki hasiende,natoa mawazo yangu kwa kile ninachoona sahihi kulingana na kipato cha wananchi walio wengi,hivi unajua Tanzania ni nchi masikini zaidi duniani?

basi yaishe mkuu maana hatupati hata senti tano kwa kubishana:lol:
 
Mleta mada,

Tatizo ninaloliona hapa ni wewe kuwa kinyume na mfumo wetu wa sasa wa maisha. Kwa maana nyingine, wewe unaishi kijima sana!

Dunia ya leo jinsi ilivyo ni kwamba, kama mimi ni mfanyabiasha au mtoa huduma, na kama hakuna msimamizi (regulator), basi nina uhuru wa kuchagua bei ninayoitaka ya bidhaa zangu!

Hapa Tanzania kuna private investigator, unajua kwa huduma moja wanatoza kiasi gani!? kwa ushamba wako ukijua unaweza kufanya maandamano ya haraiki!

Aidha, semina iwe ya Milioni moja, milioni kumi, it doesn't matter, what matters is that people are the ones to decide which among of the seminars held in town they wanna go to. So, kama mimi nafikiri it worth it kutoa milioni moja na kupata ujuzi utakao nitengenezea milioni 10 zaidi kwa mwezi, why not paying for that!

By the way, huko mitaani zipo mpaka seminar za bure. Je, it worth kwenda kwenye hizo seminar? Mimi sijui, watu wanao kwenda ndio wanatambua hilo. Lakini zipo hadi seminar zina charge $ 350 - 500 hapo Kenya na watu wanaenda. So, it all about choice!

Lakini sio vyema mtu tu upo kwenye bench huko mtaani kisa umepata access ya internet na uwezo wa kutype kwenye Tecno yako basi uanze tu kuwaita watu wengine matapeli na unafanya hivyo bila kuambatanisha ushahidi wowote usio na shaka kwa hizo tuhuma zako! Huo ni upuuzi na mtu mzima mwenye akili nzuri hawezi kufanya hivyo!

Halafu katika kuhalalisha upuuzi wako unasema " mimi siachi kufanya kile ninacho kiamini ni sawa!" Hivi una akili nzuri wewe? Wapo wenzako wajinga kama wewe wamefanya mauaji (cold blood), niliwauliza kwanini mmefanya hayo, wakasema waliamini wanafanya jambo sahihi. Kwa sasa wanaozea jela!
..................
Binafsi sina mahusiano yoyote na hizo seminar ijapokuwa nakiri kuhudhuria baadhi na niseme tu nimefaidika nazo sana katika kuyaendesha maisha yangu.

BEST REPLY IN THE WHOLE THREAD, any mature bussinessman will agree with u!!
 
Ndio kuna wengine wanaweka tangazo la kutafuta wachumba kumbe nao ni matapeli tuu tusiwe watu wa kukurupuka umu jamii forum.
 
Wewe unatetea ujinga na hujui unachokitetea. Sijatukana fikra zake. Kilichoniudhi ni kukurupuka kwake na kuanza kuita watu wezi na matapelio. Sina interest na hii semina lakini pia siwezi kaa kimya mtu anapoongea vitu bila facts na huku akitukana wengine ni matapeli. Kabla ya kuita watu matapeli angeweka break down of how yeye anaweza akaorganize the same seminar at much cheaper price. Acheni kukariri maisha. Jifunzeni kuwa objective katika kujadili mambo. Kama unataka usitukanwe changia kama mtu mwenye akili. Ukichangia kama umekunywa komoni utaishia tu kuambulia matusi. Sisemi kwamba mawazo yangu ndo sahihi.Nachosema ni ajifunze kujenga hoja kwa facts bila kukurupuka tu na kugeneralize vitu ambavyo huna uelewa navyo

Mimi namshukuru mtoa maada kwakunihabarisha maana nilitaka kwenda huko kumbe ninepoteza pesa zangu tu
 
sidhani kama ni sahihi kusema utapeli, kutoa elimu ni ujasiriamali pia, na mtu anapanga bei kutokana na anavyodhani ndivyo anavyostahili. wala usihangaike kuwaasa watu wasiende, mwenye nazo automatically kwa kupima atapata nini ataenda, asiye na uwezo ataenda aliyo na uwezo nayo. hata hiyo elfu 30 - 50 unayosema kuna wengine hawana pia, lakini kuna ambao akisikia elfu 30 haendi kwa kudhani hana hadhi hiyo! akisikia laki mbili anaenda.

hizo semina za elfu 30 wengine wanaziita za kufundishana kutengeneza sabuni za maji, biskuti na batiki, au za wanaotaka kuanza kujiajili, wengine hawako huko, wanatafuta mawazo mapana zaidi ya hapo.

automatically mwenye kutoa 1.2 ml kwa semina unadhani niwa kwenda semina ya elfu 30? humu JF tumo makundi mbali mbali, usiumize kichwa kuusemea moyo!!!!!!!!
 
Serikali itawalipia officers mwishowe wanaenda kulala tu huko kama wale wa bungeni.
 
Back
Top Bottom