Watanzania kuweni makini na matapeli hawa wakubwa, waliojificha kwenye kutoa Elimu ya Biashara

Hiyo semina hakuna alieshikwa mkono kuwa uende au usipoenda unapigwa. Ni uamuzi wa mtu

Mawazo ya kila mtu nayaona kuwa sahhihi, jinsi ya kuwasilisha na kutilia mkazo ndio watu wanapotofautiana.
Kwa mfano, ukiwa unajua mtaa fulani, kama Congo, Kariakoo, kuna vibaka, naamini ni vyema kutahadharisha wanunuzi wanaokwenda maeneo hayo. Nitamshangaa mfanyabiashara wa mtaa huo atakayekutolea lugha ya kejeli, matusi, ....
Watu maskini na wasio na uelewa wanatapeliwa kwa namna nyingi ikiwaamo kuuziwa bidhaa duni kwa bei ya juu kwenye shopping malls, semina elekezi zisizokidhi mahitaji, ...
Tushindane kwa hoja!
 
Freelancer

Wewe unaleta ubishi tu na ligi ,na huelewi kabisa nimesema sijamshikia bunduki hasiende,natoa mawazo yangu kwa kile ninachoona sahihi kulingana na kipato cha wananchi walio wengi,hivi unajua Tanzania ni nchi masikini zaidi duniani?

basi yaishe mkuu maana hatupati hata senti tano kwa kubishana:lol:
 

BEST REPLY IN THE WHOLE THREAD, any mature bussinessman will agree with u!!
 
Ndio kuna wengine wanaweka tangazo la kutafuta wachumba kumbe nao ni matapeli tuu tusiwe watu wa kukurupuka umu jamii forum.
 

Mimi namshukuru mtoa maada kwakunihabarisha maana nilitaka kwenda huko kumbe ninepoteza pesa zangu tu
 
sidhani kama ni sahihi kusema utapeli, kutoa elimu ni ujasiriamali pia, na mtu anapanga bei kutokana na anavyodhani ndivyo anavyostahili. wala usihangaike kuwaasa watu wasiende, mwenye nazo automatically kwa kupima atapata nini ataenda, asiye na uwezo ataenda aliyo na uwezo nayo. hata hiyo elfu 30 - 50 unayosema kuna wengine hawana pia, lakini kuna ambao akisikia elfu 30 haendi kwa kudhani hana hadhi hiyo! akisikia laki mbili anaenda.

hizo semina za elfu 30 wengine wanaziita za kufundishana kutengeneza sabuni za maji, biskuti na batiki, au za wanaotaka kuanza kujiajili, wengine hawako huko, wanatafuta mawazo mapana zaidi ya hapo.

automatically mwenye kutoa 1.2 ml kwa semina unadhani niwa kwenda semina ya elfu 30? humu JF tumo makundi mbali mbali, usiumize kichwa kuusemea moyo!!!!!!!!
 
Serikali itawalipia officers mwishowe wanaenda kulala tu huko kama wale wa bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…