Watanzania kuweni makini na matapeli hawa wakubwa, waliojificha kwenye kutoa Elimu ya Biashara

Watanzania kuweni makini na matapeli hawa wakubwa, waliojificha kwenye kutoa Elimu ya Biashara

Maisha yanatofautiana,kuna mtu amewahi kununua mboga ya mil10 atashindwa kutoa $700 kwa siku?
 
Mbona mnagombana na kukashifiana na kutoleana lugha gongana jamani
mwenye uwezo wa kuhudhuria hizo seminar za laki7 aende naasiye na uwezo aache
acheni kutoeleana maneno gongana kisa seminar atakayeona inaffaa kwake kutoka
kwenye uchumi na kupanuka kimawazo aende tu ni hiari ya mtu

na hapa ni sehemu ambayo mtu anaongea atakavyo na kwa uwazi wake alivyo
 
hapa ndio napoelewa kwann hatutakaa tupige hatua, ni wagumu kugharamia taaluma yenye tija ila wepesi kugharamia gambe na vitu vya sifa za kijinga
 
hivi si majuzi tu serikali ilipiga marufuku ku-price bidhaa kwa pesa za kigeni?
au mimi ndio sielewi? labda semina sio bidhaa...
 
Kasema kweli mleta mada, sasa kama inalenga wenye pesa ikawafate huko mafanikio mafisadi, kipi kipya katika izo seminar hakijawai kuandikwa? Kila siri ipo katika vitabu, leo eti watanzania maskini wanaoishi chini ya dollar 1 umwambie dollar 700? Seminar

Ni wezi, ni. Majambazi labda kama iyo seminar wanafundisha jinsi yakuuza unga bila kukamatwa, ila hata aje billgate naimani semina zke zitakuwa na yaleyale wanayosema na kuandika katika vitabu kila siku.

Then seminar ni maandiko tu sio reality unaweza pigwa brash na ukatoka ukawa maskini kama wewe ivo ivo milele.

kama wewe unafikiri wa Tanzania kuishi chini ya $1 inahalalisha watu wasiende kwenye seminar ya $700 kwa siku endelea na ujinga wako. Nakushauri pia kuanzia leo uache kutumia Internet. umeme, gari zuri kama unalo na uhamie kwenye nyumba ya udongo kwa sababu ni wa Tz wachache wenye access na hivo vitu na itakua vzr ukiwaunga mkono kwa hilo
 
As long there will be a seminar sio kwamba anatapeli hela that price is nothing!

QUOTE=Money Stunna;12369452]Kuna watu umu wanaleta matangazo ya semina za siku moja kupata masoko kwa gharama za dolla 700 zaidi ya Tsh 1,260,000 Tsh . Awa watu hawana tofauti na matapeli wakubwa wanaotaka kupata utajiri wa siku moja kupitia kuwakamua nyie pesa zenu bila huruma kabisa.

Hizi semina za biashara gharama inabidi ikiwa kubwa iwe 30,000 -50,000 Tsh mwisho hisizidi hapo Lakin ukiona mtu anawambia dolla 700 hujue huyo ni 419 anaotaka kupata utajiri mkubwa kupitia pesa zenu na wengi wanakuwa hawana ata biashara zaidi ya kutapeli ata hao wenye biashara pia wanaowakamua hizo dolla ujue utajiri wao wa mashaka ni 419 utatozaje mtu pesa yote Hiyo!! Huo ni mtaji kabisa.

Kuweni makini ni hayo tu[/QUOTE]
 
Mkuu,

Siku zote elimu inapotolewa, suala la matokeo ya ulichojifunza, hilo utaamua wewe uliyejifunza.

Ndio maana leo hii kuna shule kama IST ada yao ni TZS 11 Milioni kwa mwaka na wapo wanafunzi wana feli. Vilevile kuna Fedha boys, ada TZS 5 milioni kwa mwaka na wapo wanao faulu pia wanaofeli wapo.

Pia kuna shule kama Green acres ada ni Milion 1.2 tu utakuta wanao faulu na wanao feli.

Hiyo mifano yote ni kukuonyesha kuwa, it's a free world, full of choices and options. Wala halazimishwi mtu kufanya maamuzi. Na kama huwezi wewe, wapo wanao weza. In fact, Mtanzania mwenye uwezo wa kutoa Laki 7 sio sawa na wewe kiakili kabisa.

Wewe hapo laki saba unaona pesa, ila kuna watu hiyo ni bajeti ya vocha kwa mwezi. So, tuna vipato tofauti, matumizi tofauti, mipango tofauti. Sio kisa wewe una njaa na uwezo mdogo wa kufikiri, basi ukadhani JF members wote wapo sawa na wewe. No, we differ!

Mfano mwingine, hata humu JF kukudhihirishia kuwa kuna classes au matabaka, kuna watu ni Gold member, kuna Tanzanite na hadi Platnum members! Unadhani hizo status unapewa bure!? Ni pesa tu ndio itakuweka kwenye kundi lako.

Yani Watanzania ujamaa umetuathiri sana, yani kwenye seminar laki 7 inaonekana nyingi hadi kuitana matapeli!!! Na utakuta katika hiyo laki 7 kuna huduma ya chakula pia. Bado ni nyingi tu?

JF matajiri wapo; maskini mpo na pia wenye vipato vya kati tupo. Hivyo mtu yeyote hakatazwi kuweka chochote humu as long as hakivunji taratibu na miongozo yetu tuliyojiwekea.

Kama wewe ni maskini na unaogopa kulipia elimu, basi baki na umaskini wako + Ujinga. Waacheni wengine wanaoona umuhimu wa elimu itolewayo kwenye seminar regardless of the entry fee, waende.

Unaweza ukaongea maneno yoote hayo lakini haiondoi ukweli kwa $ 700 ni nyingi, na unaweza kuta mtu kama wewe unaejifanya una exposure kwa kuzungumzia hizo shule hapo juu si ajabu wazazi wako wapo madongo poromoko wewe upo jijini kujifanya una exposure, dola 700 ni nyingi hata mtu usemeje hata uwe una pata 4,000,000 kwa mwezi dola 700 ni nyingi aiseee
 
mmekutana mburulaz. Nyie ndo mburula mnakuja hapa mnalalmika kwanini juisi samaki samaki elfu tano wakati sokoni embe miatano. Je ni kwanini? Kati ya mnaoshadidia hiyo hoja hapo juu mnaweza mkanipa jibu la swali langu? Mkijibu kwa ufasaha nitanyamaza kimya

Dola 700/= kwa siku moja kwa kipato gani kwa wengi wetu sisi watz wewe mbona unatetea Kitu cha ajabu Duuh au umezaliwa Na yule alikuwa waziri ambae kasema 10m ni Ya kuendea sokoni. Acha hizo babu usichukulia poa... Unajua wastani Wa pato la mtz kwa siku... Inawezekana jamaa hajatumia Lugha nzuri kwa upande wako ila wengi wetu tumeelewa nini anasema/anatahadharisha.
 
Hata ingekuwa elfu hamsini wewe ungeenfda au unapiga tu domo hapa vitendo zero
 
Hata ingekuwa elfu hamsini wewe ungeenfda au unapiga tu domo hapa vitendo zero

Duh unalazimisha watu waende au? Umelipwa kiasi gani? Mbona unatoka povu sana? Hutaki demokrasia? Wacha watu waseme "akili za kuambiwa..." Sioni hata mantiki Ya swali lako? Maana hata hatujuani? Sasa kwenda kwangu mimi au kutokwenda wewe utafaidika na nini? Duh
 
Haya Team ulalamishi. I wish some body could see a bigger picture and not that $700. Nachoencurage ni kwamba sisi tunaosuggest elfu hamsini tuwe wa kwanza organize na sio kulalamika tu kwa excuse za eti Watanzania maskini. Aliyewaambia mwenye semina anataka watu wa dola moja kwa siku nani? Mimi siipigii debe but I am trying to be objective:biggrin1:
 
We jamaa unajiona tajiri sana!!!
 
kaa kimya basi. Maana umewaita watu matapeli hayo ni matusi ni si mawazo tena. Una ruin credibility za watu halafu unataka unangaliwe tu. Kama huwezi kaa kimya nba wewe organize lakini maneno matupu hayana tija

Anachozungumza mwanzisha thread ni sahihi na nakielewa. Hapa town kuna watu wengi tu wanaoendesha maisha kwa kutumia hizo semina. Wanapanga ofisi, wanasomesha watoto wao, na kujenga na kununua magari kwa pesa za semina hizo za kuelimishana na kukuza profesional networks.
Semina hizo sio mbaya ila tatizo ni pale zinapokuwa shallow halafu gharama zinakuwa juu na unadanganywa na bites, kahawa na soda wakati presentation inakuwa ya kilayman kutoka kwa wajanja wajanja fulani tu wasiojielewa wala kuelewa walichokileta halafu ukiangalia umelipia dola 350.
419 ni jina linalowakilisha scam yoyote inayolenga kumtajirisha mwizi ghafla kwa kupitia ujanja.
Nilishaachana na kuhudhuria visemina uchwara nilipoligundua hilo, siku hizi nahudhuria za kueleweka.
 
kwa hiyo mtu akianzisha thread anatakiwa aungwe mkono tu? tukitaka kupingana na mawazo yake tuanzishe thread nyingine??? mm napingana na ww na mleta thread pia kwa kulalamikia gharama ilihali kuna wenye uwezo wa kulipia. mbona samakisamaki wanauza mishikaki sh 5000 wakat sisi huwa tunakula mishkaki sh 500 sehemu nyingine? uswaz watu wanakula mishkaki ya chelewa kwa sh 200?
 
nilishasema sijamshikia mtu bunduki hasiende,we nenda tu ( $ 700 ZIDISHA 1000 ) hapo ndio hatujulikana nani amekuwa millionea,nani amepoteza,we nenda kwa amani sijakuzuia
 
kuna wengine wanauza vitabu namna ya kuwa tajiri lakini watu hawajui wakishanunua vitabu hivyo tayari wamewatajirisha wengine hakuna njia ya mkato katika maisha hilo watu inabidi walijue ndio maana watu wengine pamoja na elimu yao wanaua albino kwa ajili ya kutaka utajiri wa haraka haraka
 
Watanzania bwana wakiambiwa wanaibiwa wao wanabisha sana lakini baadae utasikia tumeibiwa(rejea ununuzi wa rada)
 
Hiyo semina hakuna alieshikwa mkono kuwa uende au usipoenda unapigwa. Ni uamuzi wa mtu
 
Back
Top Bottom