tuusan
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 17,972
- 20,221
Safi umeongea kwa weledi uwe na siku njema bro!Kwa mkaazi wa Kimara hayo mabasi yana unafuu sana kwake maana ni mbali na mjini na pia huko ndiko mwisho kama sijakosea au kusahau. Hivyo kwake yeye 1,300 ni nafuu, lakini hebu ifuate hiyo barabara yote ya Morogoro ujaribu kuwaza hali ilivyo kwa wakaazi wa maeneo ya kati kama Ubungo vile, waliokua wamezoea daladala za 300 leo hii umemshtukiza na lipipa linamgharimu mara mbili ya hiyo.
Halafu limehodhi barabara yote, daladala haziruhusiwi humo, hivyo hana mbadala inabidi alisubiri, na likija linakua limefurika maana maskini wote wanang'ang'ania humo kwa kukosa mbadala.
Pia usiwalinganishe wachuuzi wa kwenye magenge maana kama ilivyo hata hapa Nairobi, wao hupiga hela ndefu sana hata kuzidi makarani ofisini, na pia wengi wao mjini huenda labda mara moja au mbili kwa wiki wakati wanafuata bidhaa. Lakini karani mvaa tai anayesubiri laki tano kila mwisho wa mwezi, hana kipato kingine, kazi yake kupanga stakabadhi na madaftari ofisini siku nzma, lazima aone hizo 1,300 zikiwa ndefu.
Sent using Jamii Forums mobile app