baba anjela
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 431
- 310
Kwa kweli ni mambo ya kushangaza sana tukio la Lissu kukutana na mama na shangaa watu wakiponda na wengine kuingiza ushabiki wa vyama.
Wote ni viongozi na wanasiasa wanachokiongelea si kwa faida yao tu, bali kwa nchi nzima au tulitaka hivi vikao vifanyike kwa hisani na shinikizo la UN au USA, baada ya watu kumwaga damu na kufa, au tunataka maridhiano kama yaliyokuwa yakiendelea Libya au Sudan.
Hapana. Tufike mahali tujitafakari tunataka nini na hatutaki nini? Tungekuwa na wanasiasa wenye uchu na madaraka leo Watanzania tungekuwa wakimbizi kama wenzetu walivyo. Wazungu wanatamani sana tufike hapo lakini kwa nguvu na uweza wa Mungu hatutofika lakini hizi propaganda za kijinga zisipokomeshwa tutafika sababu si viongozi wote wana akili ya kuchuja. Tutapata wanasiasa/viongozi vichwa vibovu wataongozwa na hizi porojo.
Watanzania mambo yanayotokea kwa ndugu zetu yanaweza kutokea na kwetu. Leo kinywa hakina nguvu sana kama kidole. Pale unpoandika ujumbe kabla ya kutuma jaribu kutafakari je hiki kitaleta hafya kwa taifa langu au la?
Usikubali kujiunga na wajinga wa chache wanaokata tawi la mti wakati ndilo walilokalia.
Nenda kasome chanzo cha vita vya Syria utatambua kuna nguvu kubwa katika mitandao. Si sehemu ya mzaa..
"Tambua massage yako watasoma watu tofauti, wenye ufikiri tofauti na wenye mapito tofauti"