Kwahiyo, kwa maelezo yako hayo ndo unatarajia nchi fulani kukitokea vita basi serikali ianze kupekua watu walipita kwenye airports zetu kwenda kwenye hizo nchi, ama?Kwani wakati wana ondoka wana pitia wapi serikali isijue? Ofisi za uhamiaji pale airport zina kazi gani? Mbona wana tuhoji paka jina la wife na watoto kijiji shughuri kwanini wasijue idadi ya watu. Serikali zetu hamna kitu kama vitamburisho vya taifa kutoa ni shida ndo waweze hilo.
Tuchukulie hii issue ya Ukraine kwa mfano... je, serikali ianze kupitia orodha ya miaka mingapi nyuma?! Na ukishapitia, utakuwa na uhakika gani kwamba bado wapo Ukraine?!
Hivi unajua unachokiongea?!
Na wakati mwingine, unakuta watu wametoka Bongo, say to Russia kwa ajili ya masomo. Wakimaliza masomo yao, wanajichanganya huko kwa huko... ndo hapo unakuta mtu kaondoka Bongo kuelekea Russia lakini baada ya kumaliza masomo yake, anaenda kutafuta maisha, say, Georgia au Maldova!!
Sasa watu kama hao unatapata wapi taarifa zao wasipoenda kuripoti ubalozini?