Uhuru alichukua maamuzi ya kuusafisha uongozi wa serikali ya Jubilee kwa gharama ya kumuingiza hasimu wake mkuu kwenye serikali na kumsaliti Rafiki yake Ruto, Kwa bahati nzuri Ruto aliliona hilo mapema akaanza kujipanga bila kusubiri support/endorsement ya Uhuru, Ruta akapanga mikakati yake tangu 2018 matokeo yake yameonekana kwenye uchaguzi huu, upande mwingine Raila akawa mlevi wa madaraka akaona atapita kirahisi kwakuwa ana support ya serikali.
I respect your perspective, japo nitatofautiana na wewe kwa hilo.
Raila Odinga huko nyuma aliwasumbua sana Uhuru na Ruto (licha ya kwamba at one time walikuwa timu moja). Sasa ule ugomvi, hasa uliozua vita na mauaji, na kushtakiana the Hague, matokeo kufutwa na kurudiwa uchaguzi upya 2017, wakasusia, ni wazi Raila Odinga kwa Uhuru alikuwa amevuka mipaka ya uadui na kuwa hasimu.
Uhuru inaonekana alikuwa amemmezea fundo moyoni na kumkubalia tu awe naye (plus ahadi-bubu ya kumrithisha kiti baada yake) ili nchi itulie, ajenda yake na maendeleo visonge mbele.
Vinginevyo, kwa influence ya Raila wakati huo, na tuhuma iliyoonekana kuwa wazi katika mchakato wa uchaguzi, angezua taharuki kubwa zaidi na nchi isingetawalika.
Which means, alilazimika kumwaminisha Raila, umma, especially supporters wa Raila, kwamba sasa yeye hayuko tena na makamu wake Ruto, ili kumwandalia njia RO.
If that was not the case, kwa ushawishi na mamlaka ya Uhuru, angemwondoa kabisa Ruto kwenye nafasi ya umakamu wake na kumweka mtu mwingine (kupitia mchakato wa Bunge na Seneti, of course).
Na wala Uhuru asingeshindwa kitu kwa sababu kuna viongozi wengi tu tena wa chama chake waliosafishwa wakati wa fukuto ndani ya chama na serikali in the past two years.
Another evidence muhimu sana pia ni kwamba Ruto na Uhuru wamekuwa makini sana (tangu waonesha hali ya kutofautiana hadharani) katika uchaguzi wa maneno na namna ya kuwasilisha kauli walizokuwa wakirushiana.
Ni mara chache sana (na hasa hapa mwishoni kuelekea kwenye uchaguzi), ndipo joto lilipanda kidogo, but ilikuwa ya kutawalika. Kazi hiyo ya purukushani mara nyingi ilifanywa na viongozi wengine loyal na supporters wa pande hizi mbili (ambao pengine walikuwa hawajui dili lililokuwa likichezwa na hawa bosses wa kwanza na wa pili.
Na hii danganya-toto ya Uhuru kumtenga ilikuwa opportunity kubwa sana kwa William Ruto.
Kwanza, anaendelea ku-enjoy privileges na heshima almost zote muhimu za vice president (tena akiwa amepunguziwa mzigo wa majukumu ya msingi), na hivyo kujitanua kisiasa, kueneza sera zake, kusoma hali ya hewa kisiasa, kuwajua marafiki na maadui, kupima joto na kina cha maji, kujimegea ^mafungu^ as usual, na kuendelea kujitambulisha kwa Wakenya na kulikana zaidi.
Pili, ingekuwa rahisi kuchagulika baada ya Uhuru kwa sababu angeji-portray kama mhanga (victim), aliyenyimwa nafasi kamili ya umakamu. Hii ingemsaidia kuishambulia na kuikosoa kihalali serikali ileile ambayo yeye ni kiongozi wake mkuu namba 2.
Ikumbukwe kwamba wapinzani wagombea hupewa kipaumbele na raia kuliko wale waliomaliza muda wao na wanaomba ridhaa nyingine ya uongozi.