Watanzania mmerogwa na nani? Badala ya kujadili hoja za Kamati ya Maadili ya Bunge nyie mnamjadili Spika Ndugai na Yesu

Watanzania mmerogwa na nani? Badala ya kujadili hoja za Kamati ya Maadili ya Bunge nyie mnamjadili Spika Ndugai na Yesu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli Watanzania kama taifa bado tuna safari ndefu sana kufika kule tunakotarajia kufika.

Jana mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge mh Mwakasuka na wajumbe wa kamati wametumia takribani saa 3 kuelezea utovu wa nidhamu uliofanywa na wabunge Jerry Silaa na Askofu Gwajima.

Kwa bahati mbaya wakati wa kuhitimisha Spika aliteleza ulimi kwa sentensi ya sekunde moja tu.

Cha ajabu watanzania hawa wameachana kabisa na hoja za kamati na badala yake wamemshupalia Spika Ndugai.

Wananchi tubadilike tuwe wazalendo.
 
Jana wabunge karibu wote walikuwa na mipasho na mihemuko tu na ukifatilia vizuri unaona wanauhasama na gwajima. Pili kila mjumbe alijifanya ni Mkristo safi na kuijua biblia vizuri mpaka mmoja wapo akatamba anaujua Ukristo sana eti kwa kutalii Israel Mara 4 ndio kujua neno la Mungu!

Hapo sasa ndio akatuonyesha kichwa maji kwa kusema Yesu alienda na mke wake Bethlehem. Hapo ndipo Mungu akamshushua kwa kuuthihilisha uma wa Watanzania kwamba hakuna kitu hapo.

Mtu anatamba anasema mm ndio speaker nitakushugulikia humu na kamati kuu nipo nako nitakushughulikia.analazimisha MTU aombe msamaha adhalani huo ni unyanyasaji.
 
Wao hao wabunge wameiingiza Tanzania kwenye shida nyingi sana ila hawajatuomba ladhi hata siku moja Leo watu wanakuwa kinyume nao wanajifanya wakali.

Kwenye maslahi yao wakali ila kwenye maslahi ya Taifa hawana kitu mfano wabunge wanashangaa kuona atcl deni linakua. HV inamaana hawaoni rais wao anavyosafiri kwa kutumia hzo ndege.

Waziri mkuu, makamo wa rais kila siku ndege zipo angani. Hapo kwa nn deni lisikue.maana sio za biashara ni kutumika tu bure na wafanyakazi wanatakiwa kulipwa
 
Tanzania haina wabunge wa kuchaguliwa na wananchi. Ni punguani peke yake ndiye anaweza kuamini kuwa Tanzania ina bunge.
 
Bwashee hapo bungeni mmejazana tu vichwa maji wote. Kuanzia waliotuhumiwa na waliowatuhumu na kuwapa adhabu. Hakuna wanachofanya zaidi ya kula kodi za walalahoi tu.

Haiwezekani utulazimishe tujadili upuuzi kama huo. Na Mungu alivyo sio Mzee Mkumba ametuonyesha jinsi walivyo watu wa hovyo kwa kuropoka hovyo kuwa Yesu alikuwa na mke.

Tena baada ya blunder hiyo wakatuandikia na barua ya kuomba radhi nayo wakafanya tena blunder ngingine. Sijui sasa kama watatoa tena barua ya kurekebisha barua ya mwanzo.

Upuuzi mtupu. Bunge hewa kabisa.
 
Udaku udaku tu.

Baadhi ya hao wanapenda UBUYU zaidi ya HOJA ZENYE MANTIKI.

CCM IENDELEE KUTUTAWALA TU

#SiempreCCM
 
Kiukweli watanzania kama taifa bado tuna safari ndefu sana kufika kule tunakotarajia kufika.

Jana mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge mh Mwakasuka na wajumbe wa kamati wametumia takribani saa 3 kuelezea utovu wa nidhamu uliofanywa na wabunge Jerry Silaa na Askofu Gwajima.

Kwa bahati mbaya wakati wa kuhitimisha Spika aliteleza ulimi kwa sentensi ya sekunde moja tu.

Cha ajabu watanzania hawa wameachana kabisa na hoja za kamati na badala yake wamemshupalia Spika Ndugai.

Wananchi tubadilike tuwe wazalendo.
👊
 
Back
Top Bottom