BONGOLALA
JF-Expert Member
- Sep 14, 2009
- 16,508
- 11,897
Eneo litakalojengwa bandari mpya Bagamoyo ni lile lile ambalo chuo cha uvuvi mbegani kipo. Waalimu wanasema mamlaka ya bandari imeahidi kujenga chuo kingine eneo ambalo hawajajua ni wapi. Ikumbukwe kuwa chuo kile ni cha aina yake Afrika Mashariki, kati na Kusini, kuna wanafunzi toka nchi mbali mbali.
Pia chuo hicho kilijengwa mwaka 1972 na baadae wa Norway wakakikarabati kwa majengo ya kisasa na zana za kisasa za kufundishia kama boat za uvuvi na cold rooms. Je, leo hii wa Norway wakisikia chuo ambacho tulitumia maneno matamu kuomba msaada na wao wakatumia kodi za wananchi wao kutujengea, kimevunjwa na kupewa mchina kwa matumizi mengine watatuelewaje?
Na serikali imelisema hili kwa watanzania tukakubali chuo kuvunjwa? Ikumbukwe tunahitaji sana wataalamu wa mambo ya uvuvi kwani tuna ukanda mkubwa wa bahari na maziwa lukuki! Kwa nini huyo mchina asipewe eneo jingine aanze upya ujenzi wa miundombinu? Pale chuo kuna maji safi ya dawasco, kuna umeme mkubwa, kuna gati ndogo, pia kuna barabara ya lami toka main road ya kuelekea Bagamoyo-Dar, kuna nyumba za waalimu na madarasa, maabara, mabwawa ya samaki wa shamba darasa.
Yaani hapo mchina hatawekeza chochote zaidi ya kuweka mashine za upakuaji mizigo na kuanza kuvuna! Hii ni sawa na serikali ilipotaka kuuza jengo la mahakama ya rufaa ili kupisha ujenzi wa hotel-kempinsk. Wabunge, Wananchi tunalijua hili na tumeridhika na uamuzi huo wa kukiua chuo?
Ninavyo jua mamlaka ya bandari-TPA kujenga hicho chuo sehemu nyingine ni hadithi kwani vya kwao wenyewe vinakufa wameshindwa kuviendesha. Kama ni hivyo mchina ajenge kwanza chuo cha kisasa zaidi ya kile ndipo aende mbegani kuanza ujenzi wa bandari.
Mkataba unasemaje juu ya hili?
Nawasilisha.