Watanzania mnajua kuhusu Bandari mpya Bagamoyo?

Watanzania mnajua kuhusu Bandari mpya Bagamoyo?

Mie mamuzi ya baba mwanahasha yamenichosha kweli, yani huwa simwelewi kila kukicha zengwe analizua kwani mama cholo huwa hamshauri jamani hivi kweli amekosa pahala pa kujenga mpaka avunje chuo hicho majanga.

Si Bora uamuzi atoe mwenyewe kuliko....
 
ninaelekea huko wiki hii kuanza valuation ya fidia kwa eneo la bandari. Nimeshakagua majengo yale hayana upekee kama vuvuzela linavyopigwa. Ntakuwa fair kwa mali za wananchi. Mwenye hoja za maana alete au a pm sio majungu mradi huu ni muhimu.
 
Eneo litakalojengwa bandari mpya bagamoyo ni lile lile ambalo chuo cha uvuvi mbegani kipo.Waalimu wanasema mamlaka ya bandari imeahidi kujenga chuo kingine eneo ambalo hawajajua ni wapi.Ikumbukwe kuwa chuo kile ni cha aina yake Africa Mashariki,kati na kusini,kuna wanafunzi toka nchi mbali mbali.

Pia chuo hicho kilijengwa mwaka 1972 na baadae wa Norway wakakikarabati kwa majengo ya kisasa na zana za kisasa za kufundishia kama boat za uvuvi na cold rooms.Jee leo hii wa Norway wakisikia chuo ambacho tulitumia maneno matamu kuomba msaada na wao wakatumia kodi za wananchi wao kutujengea, kimevunjwa na kupewa mchina kwa matumizi mengine watatuelewaje?

Na serikali imelisema hili kwa watanzania tukakubali chuo kuvunjwa?ikumbukwe tunahitaji sana wataalamu wa mambo ya uvuvi kwani tuna ukanda mkubwa wa bahari na maziwa lukuki!Kwa nini huyo mchina asipewe eneo jingine aanze upya ujenzi wa miundombinu?Pale chuo kuna maji safi ya dawasco,kuna umeme mkubwa,kuna gati ndogo,pia kuna barabara ya lami toka main road ya kuelekea bagamoyo-dar,kuna nyumba za waalimu na madarasa,maabara,mabwawa ya samaki wa shamba darasa.

Yaani hapo mchina hatawekeza chochote zaidi ya kuweka mashine za upakuaji mizigo na kuanza kuvuna!hii ni sawa na serikali ilipotaka kuuza jengo la mahakama ya rufaa ili kupisha ujenzi wa hotel-kempinsk. wabunge,Wananchi tunalijua hili?na tumeridhika na uamuzi huo wa kukiua chuo?ninavyo jua mamlaka ya bandari-TPA kujenga hicho chuo sehemu nyingine ni hadithi kwani vya kwao wenyewe vinakufa wameshindwa kuviendesha.Kama ni hivyo mchina ajenge kwanza chuo cha kisasa zaidi ya kile ndipo aende mbegani kuanza ujenzi wa bandari.

mkataba unasemaje juu ya hili?Nawasilisha
Samahani hivi kumbe tunao wataalamu wa uvuvi,sasa huo utaalamu wao huwqa wanautumia sehemu gani?maana ukienda pale feri utakuta uvuvi unaendeshwa kijima.Kwa staili hii bora kivunjwe tu maana uwepo wake hauna faida kwa taifa,kama ungekuwa na faida tungeona mapinduzi kwenye sekta ya uvuvi.
 
Ndo hivyo wadanganyika tushaliwa, Huku mi ccm inashangilia kuua nchi
 
Back
Top Bottom