Ndugu zangu watanzania mnamshauri nini Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete???????? Maana mwezi huu tu maandamano kibao
1. Waalimu - Maandamano
2.Wahariri - Maandamano
3.Wazee - Maandamano
Tumshaurini afanye nini maana kila kukicha matatizo yanaongezeka, NAULI BEI JUU, MAISHA MAGUMU, AJIRA HAKUNA -BADALA YA AJIRA MILION MOJA ZIMEPUNGUA MILION MOJA, WAMACHINGA KILA SIKU WANAKIMBIZANA NA MGAMBO. KILA KITU KIPO JUU, KILICHOBAKI NI KULIPIA HEWA TUNAYOVUTA.
1.Je Ajiuzuru
2.Je Akimbie nchi (Apotee)
3.Je Asigombee term ya pili
4. Au oungozi unaomzunguka ni mbovu?
AU AFANYAJE??????????
Tatizo Yeye mwenyewe ni mbovu na tatizo kubwa zaidi ni kuwa wasaidizi wake aliowachagua wengi ni wabovu karibu kila eneo sababu vigezo alivyotumia kuwaweka ni tu kama ni wana mtandao au washikaji waliomsaidia kwenye kampeni au watoto au ndugu wa washikaji au aliwahi fanya nao kazi zamani hivyo hafuatilii watu hao kama bado wachapa kazi au la.
Wasaidizi wake Wengine wameamua kuwa wabovu baada ya kuona kuwa na yeye si mtu serious wakaamua nao kutokuwa serious.
Wasaidizi wake wengine hawako serious sababu wanamjua udhaifu wake kutoka A-Z hivyo hawaogopi wanasema akitugusa tunamwanika.Hivyo naye anawaogopa.Sasa kama anawaogopa kwa nini aliwachagua.Cheo humpi mtu kwa kuwa unamwogopa unampa kwa kuwa ni mchapa kazi.
Cha kufanya abadilike utendaji wake.Muda mwingi atulie ofisini afanye kazi.
Watu wanasema nchi haijapata Raisi bado ina waziri wa mambo ya nchi za nje kutokana na anavyosafiri nje ya nchi.
Wengine hadi wanasingizia kuwa hataki kutulia ofisini sababu ni mshirikina kwa kuwa waganga wamemwambia Ikulu hapafai kukaa kuna mashetani mabaya kwake kwa hiyo ndiyo maana anakwepa ofisi. Akitoka safari za nje ya nchi anahamia kutembelea mikoani ili mradi asiweko ofisini kwa woga wa kishirikina.
Anachotakiwa kufanya angalau kwa sasa kwa kuanzia kama atapenda nitataja machache:
1.Abadilike utendaji wake na wa walio chini yake ili arudishe imani ya wananchi kwake.
2.Atulie nchini na ofisini kwake Ikulu afanye kazi aache kuruka ruka.Aliomba kazi ofisini Ikulu ni vizuri awepo ofisini.
3.Atafute wasaidizi wazuri wajuao kazi kila eneo hata kama hawapendi na si washkaji au wanamtandao iko haja ya kufanya mabadiliko makubwa katika serikali yake kwa wasaidizi wake inabidi apange upya safu zake za uongozi
4.Awe na maamuzi kwenye masuala mazito yeye mwenyewe.watu wamechoka na hizo tume zake zisizoisha nchi inaendeshwa na Raisi siyo na tume.Watu wanasema nchi sasa hivi haiendeshwi na Raisi bali tume ndizo zinaongoza nchi.
5.Wakati wote azingatie katiba katika utendaji wake.Kitu kama hakipo katika katiba ya sasa ambayo haijabadilika asithubutu kukivalia njuga.Mfano mambo ya Kadhi na OIC aachane nayo.