Watanzania mnamshauri nini Rais wetu?

Watanzania mnamshauri nini Rais wetu?

ushauri kwa mkuu wa kaya ni muhimu. ila jamani matatizo yetu makubwa KIUTAWALA yanachangiwa na KATIBA yetu hii. raisi amepewa nguvu kubwa sana kupitia katiba ndo maana lawama za uongozi na utawala zinamwendea yeye moja kwa moja. Raisi anawajibika moja kwa moja kwa wananchi kupitia wasaidizi wake. Lazima awe na picha kamili ya taifa analoliongoza na angependa liweje wakati wa uongozi wake (VISION). Sasa mkuu wa KAYA ana vision gani na taifa hili kwa sasa? Je anafikiaje malengo hayo? Mambo ya kukumbuka matatizo ya nyuma na kuanza kuleta huruma kwa utawala uliopo haijengi. huyu ni kiongozi wa taifa kwa sasa na jukumu lake ni kubeba yote mazuri na mabaya kuyarekebisha. sio kulaumu, huo sio uongozi. afterall yeye ni wa chama kile kile toka uhuru kwa hiyo amepokea kutoka kwa wenzie wenye mwelekeo mmoja kiitikadi.

watanzania tupende kuwa objective kwani kwa kufikiria kwa mapana yake na tuwe watu wa kuamini inawezekana. Jana mh zitto aligusia hasara tulizopata na tunazoendelea kupata kutoka sekta ya madini. ila akatoa changamoto yaliyopita hayana tija tusonge mbele kwani tutakuwa na migodi mingi zaidi miaka 20 ijayo. Hivi twaelewa taifa hili litaendelea kuwepo kwa vizazi vijavyooo!! sas tujenge misingi endelevu sio blah blah na cheap popularity. Mfumo wa kiutawala kwa sasa haundani na hali halisi ya taifa!!! kama kiongozi wa nchi hatendi kwa nn sisi watanzania tusitende kwa vitendo. Taasisi za umma kwa nn utendaji wake sio wa kuridhisha? je hawa sio watanzania wenye dhamana katika taifa lao?

afterall VISION ya taifa ikoje na kweli inakidhi haja ya sasa? je twailewa na kufuatilia kwa vitendoooo... mapungufu yanarekeibshwaje na kwa wakati gani?
bahati nzuri huo mpango upo lakini wadau wanaulewa utekelezaji wake na wanashiriki vipi?

Kosa kubwa linalodumaza maendeleo yetu ni mfumo wa kupata viongozi wetu.

ni baadhi ya changamoto nizionazo katika taifa hili ambalo tuna jukumu kuliendeleza sote.
 
Mkulu Joka Kuu,

Kama utasoma vizuri bandiko langu,sipo mbali na maneno yako ila sehemu moja tu,hii, "
..Civil Service ni ileile iliyofanya kazi na Mkapa. sasa mbona huyu mkwere anapwaya?"

Hii ndio inaletelea ile fact kwamba,kuna watu wamemgeuka humo humo chamani au serikalini kwa kutumia hizo influence walizonazo kwa maslai yao ili as you have put it,Mkwele aonekane hafai.

.

Kama anaona wasaidizi wake chamani na serikalini wamemgeuka unadhani ni kwa sababu gani hasa unazoweza kuzitaja kwa undani ?au hayo yanayoitwa maslahi binafsi je waweza pengine kufafanua ni maslahi yepi hayo tuyajue kwa mifano angalau?

Je unadhani Raisi na mwenyekiti wa Chama Taifa anao uwezo wa kuwatoa hao wasaidizi wake chamani na serikalini ambao wana maslahi binafsi au uwezo huo hana kiasi kuwa naye inabidi alalalamike kama walalahoi wanavyolalamika kuwa wasaidizi wake hawamsaidii kama ambavyo wananchi wanalalamika kuwa wasaidizi wa Raisi ni wabovu na hawawasaidii wananchi?

Kama uwezo anao unadhani kwa nini hawatoi na kuweka wengine akiwa kama mwenyekiti wa Chama na Raisi? Kama uwezo wa kuwatoa au kuwadhibiti hana unadhani ni kwa nini?
 
Rais wetu ashauriwe kuibadili katiba kwanza kabla ya mengine, kwa sababu mpaka leo bado tuna katiba ya chama kimoja na ni kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo ya taifa,

Katiba ikibadilika, then wananchi hatutakua na choices za kumpa rais yoyote asiyetufaa wananchi tuliomchagua, tutamng'oa kwa kutumia bunge, maana katiba ya sasa haitupi hiyo nafasi, sisi wananchi tuliomchagua.
 
Moelex,

Mi naungana na wewe moja kwa moja Jk kwa ku-prove watu wrong angeamua kufanya mambo moja kwa moja badala ya kufata procedures,akaamua kua Dictator of some sort mpaka nuda wake uishe na kwa kipinde hicho at least ajitahidi kulipa wananchi walio muaamini na kumpa ushindi wa kishindo vinginevyo hao jamaa zake hawata lest mpaka wamuone anaondoshwa kwenye madaraka kwa nguvu ya umma au hata kwa nguvu za ziada kama walivyo aanza kwa hii social un-rest kidogo kidogo mpaka kutakua hakukaliki tena hapa

SM, ndiyo maana napenda na kuiamini kauli mbiu yangu hapo chini!
 
Rais wetu ashauriwe kuibadili katiba kwanza kabla ya mengine, kwa sababu mpaka leo bado tuna katiba ya chama kimoja na ni kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo ya taifa,

Katiba ikibadilika, then wananchi hatutakua na choices za kumpa rais yoyote asiyetufaa wananchi tuliomchagua, tutamng'oa kwa kutumia bunge, maana katiba ya sasa haitupi hiyo nafasi, sisi wananchi tuliomchagua.

Mimi naungana na wewe ndugu Fiel Marshall es, abadili katiba na pia ajaribu kuwa dictecta katika kipindi hichi kilichobaki, atoe amri na sio ombi, AAMUE KUTOA AMRI MF. IKIFIKA TAREHE FURANI WAZEE WAWE WAMESHARIPWA then auone itakuwaje.

Mimi nadhani akiamua kuwa dictecta nchi itabadilika na yeye atarudisha heshima yake lakini kwa sasa heshima imeshuka na sidhani kama term inayofuata wananchi watamkubari tena, hata kama CCM watamteua wananchi watagoma, Tumechoka kwa kweli.
 
Kudai haki ni uhuru na madai ya hawa watu yameanza zamani sana. Kumlaumu Kikwete kwa haya si vyema na kwa mawazo yangu haya matatizo ni ya muda mrefu sana.

Madai ni kweli yameanza zamani na pia ni kwamba hayataisha mpaka pale yatakapotimizwa na kuwalizisha wahusika wakuu. Sidhani kama Muungwana analaumiwa kutokana na kuibuka kwa madai haya bali ni kutokana na hatua za kisanii ambazo zimekuwa zinachukuliwa na Utawala wake kwa ujumla kuhusiana na kuyamaliza Madai haya na kuleta Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.

Ama tulitaka viongozi ambao walikuwepo madai haya yalipoanza ndio wawajibike? Ni muda huu kila aliye na nafasi katika utawala abebe msalaba wa nafasi yake.
 
Ushauri mwingine ni kuwa abatilishe ule usemi wake kuwa urais wake hauna ubia. halafu aanze kumsikiliza Dk Shein katika mambo mengi
 
Hivi kumbe shein yupo?nilishamsahau! I always wonder what goes on in that gentleman's mind
 
kama ianwezekana Japan, Italy, Israel, South Africa n.k kwa nini isiwezekane Tanzania? aachie ngazi
 
Mkuu Domo Kaya, ninaheshimu sana kazi yako kwenye magazeti, unajua zile article zako za Richimonduli ninazo zote kwenye maktaba na zilisaidia sana kwenye kusaidia uchunguzi wa Richimonduli, heshima mbele bro maana najua mazingara mnayoafanyia kazi yalivyo magumu, lakini with watu kama nyinyi taifa hili tutakua sawa tu na mabadiliko yanakuja karibuni.

Respect bro!
 
sanda matuta said:
Mkulu Joka Kuu,

Kama utasoma vizuri bandiko langu,sipo mbali na maneno yako ila sehemu moja tu,hii, "
..Civil Service ni ileile iliyofanya kazi na Mkapa. sasa mbona huyu mkwere anapwaya?"

Ambayo wewe mwenye unaji-contradict,Ikiwa civil servant ni walele nini kinashindikana wasifanye kazi zao kama wakati ule wa Ben?
Hii ndio inaletelea ile fact kwamba,kuna watu wamemgeuka humo humo chamani au serikalini kwa kutumia hizo influence walizonazo kwa maslai yao ili as you have put it,Mkwele aonekane hafai.

Hivi,kuna asiyekua anajua kwamba Uncle Ben ni mtu wa mtungi mpaka anasinzia mahara,mtungi unaenda na mambo yake wote tunaya jua hizi nazo si ni starehe?
Eti,mizaha uliza waliokua na Ben pale Sayansi na tekinologia(Jamuhuri street)watakuambia Ben ni waina ipi hana tofauti na Mkwele.

Alafu,by the way,kumwita huyo JK kwa jina la kabila lake na jinsi ulivyo litumia in your sentence,i for one kama mtu wa pwani i felt offended naona ile dhana ya watu wa mwambao hawezi kitu bado unayo.
Na nadhani nastahili samahani kutoka kwako.

Sanda Matuta,

..serikali yetu ni mfano wa timu ya mpira ambapo kocha wake ni Raisi. timu hiyo ilikuwa ikicheza vizuri[wakati wa mkapa] mpaka alipopatikana kocha mpya[kikwete] aliyekuja na mtindo wake mpya wa ufundishaji.

..tangu aingie kocha mpya timu imekuwa ikicheza vibaya. kwa mazingira hayo tatizo litakuwa ni wachezaji[serikali & watumishi], au ni kocha[raisi].

..wako wananchi waliokuwa wakimfahamu Kikwete vizuri ktk kufanya naye kazi. walionya kwamba wa-Tanzania tutajitumbukiza kwenye matatizo makubwa kwa kumchagua kuwa Raisi, kwasababu uwezo na nafasi hiyo hana.

..hata wakati wa kampeni, wapenzi na wapambe wa Kikwete, walikuwa wakishindwa kuelezea rekodi yake ya utendaji kazi kila mara walipoulizwa kuhusu suala hilo.

..kwa kweli ni vigumu sana kupata Mtanzania aliyefanya kazi[wizara za madini,fedha,foreign] na Kikwete, akamsifia kwa uchapa kazi, au umakini wa aina yoyote ile.

..historia yake hiyo, na mwelekeo wa taifa letu tangu Kikwete aingie madarakani, ndivyo vinavyonifanya ni-conclude kwamba tatizo siyo serikali na watumishi wake, bali Raisi wetu na uwezo wake mdogo wa kuongoza.

NB:

..mmakua[mkapa]ana sifa ya kunywa pombe kama kinyamkera.

..sifa nyingine za Mkapa ni kujiandaa na kutafiti kuhusu jambo lolote lile aliloamua kulitekeleza.

..Mkapa pia alikuwa very demanding kwa watumishi waliofanya kazi chini yake.

..JK yeye huwa yupo yupo tu. hata suala dogo kama kutokea kwenye appointment on time ni matatizo, halafu tunakaa kutarajia miujiza toka kwake.
 
Nadhani baada ya muda wengi watakubaliana na kile ambacho baadhi yetu tumekuwa tunakisema hapa kuhusu Kikwete for a while now.
 
Nadhani baada ya muda wengi watakubaliana na kile ambacho baadhi yetu tumekuwa tunakisema hapa kuhusu Kikwete for a while now.

Kweli kabisa, taratibu anadhihirisha kuwa alijiandaa kuyapata madaraka kwa gharama yoyote, lakini hakujiandaa kuongoza
 
Kweli kabisa, taratibu anadhihirisha kuwa alijiandaa kuyapata madaraka kwa gharama yoyote, lakini hakujiandaa kuongoza
...Ndio maana Nyerere alimtolea nje 1995 alishamuona dogo upstairs ZERO...Kuuza sura na kazi ni vitu tofauti kabisa!!!!
 
SM, ndiyo maana napenda na kuiamini kauli mbiu yangu hapo chini!

Ni sisi tu watanzania hatuna mazoea ya kutazama yale wenzetu wanayoyasema na kuya chungua kwa makini,Lakini Mkulu MWANAGENZI vision au tuseme dhana (notion) yako ni ya muhimu kupigiwa mstari.
Watu wanaweza kulipinga hilo ila hatuna njia mbadala kutoka hapa kwenda kwenye Maendeleo ya kweli na kufaidi matunda ya nchi hii.

Umeona mbali.
 
..mmakua[mkapa]ana sifa ya kunywa pombe kama kinyamkera.

..sifa nyingine za Mkapa ni kujiandaa na kutafiti kuhusu jambo lolote lile aliloamua kulitekeleza.

..Mkapa pia alikuwa very demanding kwa watumishi waliofanya kazi chini yake.

..JK yeye huwa yupo yupo tu. hata suala dogo kama kutokea kwenye appointment on time ni matatizo, halafu tunakaa kutarajia miujiza toka kwake.[/QUOTE]

Just for the record,hivi nani hasa anaye panga RATIBA ya Rais (kwamba atafika sehemu fulani saa fulani,ataondoka saa ngapi?na mengineyo kadhalika) ni Rais mwenyewe au wasaidizi na Usalama?

Au haya mambo yamebadilika kiasi cha kwamba Jk anapanga ratiba yeye mwenye siku hizi?
Nifahamishe au ajuae atuambie.

NB;i am still awaiting to that apology,'' ..mmakua[mkapa]ana sifa ya kunywa pombe kama kinyamkera. ''

Wahenga wanasema,"two wrongs ,do not make it right"
 
Sanda Matuta,

..wanaopanga ratiba ya Raisi ni wasaidizi wake. lakini kama Raisi mwenyewe ni mzito kufuata ratiba matokeo yake ndiyo kuchelewa.

..kuna mchangiaji alileta taarifa za Kikwete kuchelewa on the day he was giving a speech alipokwenda UN majuzi.

NB:

..nilipomtaja Mkwere nimemaanisha Kikwete. zingatia kwamba sikusema Wakwere.

..sioni kwanini uwe offended wakati unaelewa kabisa mhusika hapa ni Kikwete na si kabila zima la Wakwere.
 
Ushauri kwa Rais Kikwete kwa sasa ni simple ..... fanya kazi yako kama mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa watanzania - yaani saidia kulinda mali za watanzania wote na sio wachache tu. Kama hiyo imemshinda basi ...... ngoja nisiseme kwa sauti......
 
Watanzania wengi washa jua kwamba uwezo wa jamaa yetu ni duni. Kama jamaa hataki kufa kwa presha aachie ngazi mapema. Maana kama miaka mitatu ya mwanzo watu washaanza kumtupia mawe sijui hiyo saba kama ataendelea itakuwaje.

Kisiki tumekikwaa wenyewe. Ila mimi siwalaumu sana wananchi kwa kumchagua Muungwana, nafikiri wa kulaumiwa ni CCM!!!!!!!!!!!!!
 
Sera mbovu za chama chake. Yeye anawezakuwa msafi ila amerithi chama ambacho sera zake hazitekelezeki sasa hayo ndio mavuno
 
Back
Top Bottom