Watanzania mnamzungumziaje mkoloni Herrmann von Wissmann?

Bwana mtafiti habari yako, mie sio mwanahistoria hivyo habari za huyo bwana uliemtaja sizijui.

Nina swari moja kwako, unamaoni gani juu ya kile kinachodhaniwa mali za Mjerumani?
Asante kwa jibu lako! Sijaelewa swali lako. Unamaanisha mali gani?
 
Asante kwa jibu lako! Sijaelewa swali lako. Unamaanisha mali gani?
Inasadikiwa Mjerumani alivyojua vita atashindwa basi mali zake akazizindika kwa makafara ambayo si rahisi mtu mwingine kuzichukua hizo mali.
Kwa Tanzania inasadikika kuna maeneo mengi ambayo yamefichwa hizo mali za Mjerumani hivyo kufanya baadhi ya yatu kutwa nzima wanahangaika kuzitafta huku kukiwa na simulizi za kutisha za mauza uza
 
Herrmann von Weissman alimwaga damu nyingi ya Wanabagamoyo katika kile kinachitwa "Vita vya Bagamoyo" ambayo kiuhalisia ilikua ni resistance ya watu wa Pwani ya Bagamoyo na Mrima dhidi ya Wajerumani tokea 1888

Abushiri alikamatwa Bagamoyo 1889 na kurudishwa kwao Pangani aliponyongwa. Lakini Wajerumani waliendelea kuwatafuta washirika wake akiwemo Makanda Bin Mwinyimkuu (huyo anayeonekana kushoto kwenye picha ya Abushiri)

Bagamoyo Massacre ilifanywa na Wajerumani wakiua watu waliokua wanahisi ni washirika wa Abushiri na walipowakosa wao (wengi walikimbia) basi waliwauwa ndugu zao. Ushahidi upo lakini vitabu rasmi vya historia vimeelezea kwa kifupi sana (pengine mstari mmoja au miwili) mauaji haya
 
Mtafute kaka ake fred vunja bei.....anaitwa fadhili fabian ngajiro.. ingia Facebook utampatia yupo fair Sana atakuaaidia sana kwenye hii topic Yako.....
Usiache kutupa mrejesho....
 
Asante sana! Nilifanya literature review tayari. Sasa ninataka kujua kuhusu maoni ya Watanzania. Lakini umenisaidia tayari na jibu lako.
Kwa kuongezea tu Wajerumani walisifika pia kwa ubaguzi na ukatili mkubwa hasa bwana mkubwa Carl Peters na waambata wake akiwemo Winsman
 
Mchezo wa watu weusi kusalitiana haujaanza leo. Tuna hii dhambi toka zamani. Laiti tusingesalitiana leo tungekua miongoni mwa nchi ambazo hazikuwahi kutawaliwa.

Turudi katika mada. Ndugu Mtafiti wa Ujerumani, babu zako bwana Herrman Von Wissman alikua ni katili mkubwa na ameua halaiki ya watu. Nilipata kufahamu habari zake kwa uchache sana kutoka kwa Mchungaji na mwanamageuzi Kamara Kusupa. Ana ubobezi wa masuala ya harakati kabla na baada ya uhuru.
 
Asante kwa jibu lako. So inamaanisha kwamba mchungaji Kamara Kusupa alijua Hermann von Wissmann? binafsi/personally?
 
Asante kwa jibu lako. So inamaanisha kwamba mchungaji Kamara Kusupa alijua Hermann von Wissmann? binafsi/personally?
Siwezi kusemea moja kwa moja.
Lakini naweza kusema hapana kwa sababu ya tofauti ya nyakati(zama) baina yao.
Nafikiri alikusanya nyaraka na tafiti ambazo ndiyo msingi wa kumhitimisha Hermann kama mtu aliyefanya unyama na ukatili mkubwa
 
rafiki wa tanzania?
karne ya 18 kulikuwa na tanzania
 
Nimejifunza kwa miaka miwili.ni for and not since.
 
Mohamed Said
 
Nimewahi kukutana na ushairi mmoja wa kiswahili cha zamani ulindikwa kwa maandishi ya kiarabu (lakini ni wa kiswahili) huko Zanzibar miaka hiyo ya mwishoni mwa karne ya 19

Bila kukosea uliandikwa huko Zanzibari lakini ulielezea mji wa kilwa (dola ya kiislamu pia) na kiongozi wake Makungunya. Pia ulimuelezea huyu Wisman kwa uchache,

Ulikuwa unamuelezea Wismann kama kijana mwenye akili nyingi kweli kweli, muungwana kisawasawa, hodari katika vita, na boti lake la kivita lililo izunguka kilwa kisiwani, yani ukimbubujia sifa zisizo na kifani

Nikipata huo ushairi ntakuwekea hapa
 

Aiseee...
Wewe mbona umechanganya madesa.....
 
Sha'iri la Makunganya

Sha'iri la Makunganya (1898) by Mzee bin 'Ali bin Kidogo bin il-Qadiri

"Sha'iri la Makunganya"; mwenye kuandika Mzee bin 'Ali bin Kidogo bin il-Qadiri, Zanzibar


1-6

Bismillahi awali,ya pili rahmaninataka kutakallam,na khabari kwapanimsishikwe na ghururi,tafaddalini jamani

7—12

na shamba mtapandiwaleo mnajuta ninibaa la kujitakia?bass mwalimkisemaashukapo Jerumani

13-19

Tutapigana jihadiKwa rehema ya mannani,Jeremani akashukaAkangia fordani.Pasiwe mtu kujibuIkawa kutaka amani,Leo mnajuta nini

20-26

Baa la kujitakia?Mtawambia kwa yaqiniNiwape yangu moyoniNitasema kwa bainiWaliondoka mjiniWaliokwenda utamboniKilwa Kivinje mjini.

27-32

Ntawataja fursaniWaume wanao shaniWaliondoka mjiniWakaingia sitimaniWatoto wa Kijerumani.Ma'askari yaqini

33-38

Elfu na sabini:Kuwataja sitawezaWatu wote kujitengeza:Amiri jeshi Raamza,Ndiye aliye haziria.Leo mnajuta nini?

39-45

Baa la kujitakia?Wazungu thabiti mitima yaoYalikuwa marudia.Wala haina khofuKulla harubu kuingiaNa furaha kuwapata,Shindo wakilisikia,

46-52

Na bunduki mikononiMji wakuwania.Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Kwa kulla neno ntatiaHapana lakubaqia:Khabari ya Makunganya.

53-58

Sikizeni ntawambia:Alianza upotovuKufanya mambo daifuNa watu kuta'arifaKujifanya mtukufu,kumbe kijitu daifu

59-64

Machoni ukimtokea;Wenziwe akawaghuriPasiwe kufikiri;Wakaingiwa na ghururiWakaja wakafa zuriHatta shahada kutoa.

65-72

Ukali wake kama ra'adiJerimani; hawarudi.Huenenda kama jaradiHapo watapotokea.Askari wa JermaniAnavowapamba kwa shaniViatu viko miguuniNa mabete kiunoni

73-80

Burangiti mgongoniGisi wanavowaliaLeo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Walipoazim vitaKwa Makunganya kufikaHatta walipomshikaNa watu kumi na sita:

81-89

Hapana pakutokeaOte wakatiwa nyororoWakawa kama watoroZikawafa roho zaoNafsi zao kupotea.Watu waliposhikanaVita vilipopiganaMjini mwa MakunganyaWatu kujikimbilia

90-98

Watumwa kwa wangwana;Hapana mtu kusemaWote wana teketeaWatu wa MakunganyaWamekufa kama panyaGisi alivoingiliwa.Boma lake likavunjwaWatu yake wakanyongwaWakewe wakapotea

99-106

Naye tanzini kangia.Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Kwa hesabu sitaweshaWengine nitawabaqishaWote wakapigwa pichaPasiwe kusalia,Leo mnajuta nini,

107-114

Baa la kujitakia?Khabari nitawapaniWalio ondoka mjiniMa'adwi wa zamaniWaliokwenda Kilwa KishwaniKumondoa SulutaniYeye bwana VismaniNa tena na Govmani.

115-121

Sitima iko tayariImekwisha jingiliaWakenda wasimwone.Maneno yao wasisemeWakawa kama waganeHapa walipo kukaa.Damiri yao moyoni

122-128

Wampate VismaniBana mkubwa wa shaniAqili nyingi kichwaniMtoto wa KijermaniEmemiliki KivinjiHatta Kilwa KishwaniTangu awali ya Lindi

129-136

Hatta Tanga Afrikani.Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Ushahidi sijatoaSasa mnawayawaya - ;Bandari Salama UlaiaUzuri wamebarabaraJinsi ilivotulia.

137-144

Zimekwisha sifa zakeVisman peke yakeWala hana mwenzi wakeAmbaye kumzidia.Kwa kulla neno ntatiaNi kama hapa AfrikaWala hana mushirikaSikizeni ntawambia:

145-153

Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Yeye mtu taratibuHakuumbwa na ghadabuUkimwona mwarabuMachoni mtokea;Ameumbwa na rehemaAmefanya mambo memaInchi zote kutengea

154-162

Ajua sana kusemaKiswahili kumwelea.Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Niwacheni nimsifuNa yeye mtu nadifuNa la tatu mtukufuRoho yake hana khofu.Tena mtu shuja'a

163-170

Jina lake tulijua:Tangu pwani hatta baraHapo asiyo sikia.Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Kaipanda AfirikaTangu nyanza hatta nyikaHapana asipofika

171-178

Barra yote kutembea.Amezaliwa BerlinaVismani mtu mwemaAnaye nyingi rehemaWatu wote wamjuaKhabari hio kufika,Walipotaka kumshikaMwaka u nussu kupita,

179-187

Hatta siku zikipitaShauri akafanyizaNa zana akatengeza;Wakenda wakifunza.Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Ushairi ntasema sanaSiku waliokutanaVisman na Makunganya.

188-196

Kwanza alimtukanaNa yeye kajinamiaKumtukana machoni kwakeMakunganya na watu wakeKamwambia: mwanamke.Nani anayo kujua?Akisema akapoaKitini kajikaliaKaondoka bana Mayoa

197-204

Maneno akitongoaKizungu: hayakumwelea.Nitawaambia kwa yaqiniSahha na bana FeltiniWakasema KiswahiliWatu wote kusikia:Bana Sahha kamwambiaLeo mnajuta nini,

205-212

Baa la kujitakia?Banyani na WahindiWaarabu na WashihiriNa wengine WaswahiliWote wakaitikia.Makunganya asisemeWakanyongwa watu sabaNa mwenyewe ndio wa nane,

213-221

Hapo asiotazama;Watumwa na wangwanaWakubwa hatta vijanaWote wakashuhudia:Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Sahha ni bana mzuriWahindi akawashauriWote wakajikania.

222-230

Bana Sahha akafikiriAqili ikamwingiaRoho ikaghadhabikaKarakoni akafikaAskari akawetaWote wakamtokea;Walingiwa na uchunguAskari na wazunguWote wakamwandamia.

231-238

Akafanyiza nadhariAkaweka watu wawiliMzungu na AsikariNyumba moja kumngojea;Maneno nitawakifuZikesha zote nyumba tatuNa ya nnne ntawambiaNyumba iliobaqia

239-246

Na jina utawatajiaYa Muhindi Kassum PiraBana Sahha akaondokaIle nyumba akangiaVitabu akavichukuaMfukoni akavitia.Akawashauri sana:Wahindi wanne wakakana,

247-254

Bana Sahha akitongoaVitabu akavitoa:Ote wakujinamia.Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Twamjua ma'alumBana Sahha kwa hukumHukumu anaiweza

255-292

Shauri kuitengeza;Naye kawatoza fedhaWahindi kujitolea.Na Wahindi Kilwa wengiWakatoa fedha nyingi.Nitafanyiza hesabuHalafu ntawambia:Najua kwa yaqini

263-269

Ni elfu 'asheriniHesabu nawambiaNi watajiri mbali-mbali.Niwasifu mahodari:Abdallah bin Omari;Ndiye aliyetokea,Hakukaa mwanamke,

270-276

Hakungojea ashikwe,Mwenyewe alijiendeaHatta tanzini kufikaNa shingo akaipelekaNa tanzi akajitiaNa watu kumtazamaNaye kimya hakusema

277-284

Marra akajangukiaKhabari nisha wapaniOte meshasikiaYa Makunganya kuuwawaMiji yote wamejuaMwanzo hatta akhiria:Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?

285-292

Wahindi wakatiwa nyororoniWakawekwa karakoniSitima wakangojea,Ilipokuja wakapakiwaWote safiria.Wakafika Bender-EssalamaWote wkaonekanaWatumwa kwa wangwana

293-300

Wote wakatazamaHapana asiwaone:Wakashukwa kama watumwaKette ilivowangia.Leo mnajuta nini,Baa la kujitakia?Bana Sahha twamjua ma'alumuAjua sana hukumu

301-308

Kawafunga kwa siku zakeAijua miaka yake,Halafu atawafungua:Hukum yao kabisaMiaka saba ikafikaWote watafunguliwa.Wakapakiwa sitima ingineNa kwao wasikuone

309-315

Wakawa kama wagane,Tanga wakasikilia.Wakatiwa katika kazi ya gariKufanyiza hawajuiWahindi wanaolia.Msimamizi tayariYupo kuwapokea

316-322

Machozi hujifutiaKazi wakifanyia:Leo mnajuta nini,Baa la kujitakiaQadi tamati sha'riNimesha kuwapa khabariYa Kilwa iliyojiri

323-330

Yote nimeidhukuriSina nililoachaKwa khabari ya MakunganyaKauwawa kimya-kimyaFitina hapana tenaKilwa yakutokea.Nimefikiri peke yanguHatoa rohoni kwangu,

331-338

Mimi na bibi yanguNyumbani tumejikalia:Nilipo nikiandikaBibi yangu anapikaHatta halafu kikeshaChakula, tukajilia,Yote nimeyandikia.Wakatabahu harufu

339-343

Wakatabahu: kuandikaUshairi umekwishaKhabari ya MakunganyaIliyo kujiri KilwaNimekwisha kwambia.

344-348

Mwenyi kuandika usha'iriAna mu'alimu MzeeBin mu'allimu AliBin Kidogo bin Al-QadiriNa il usuli Zingibari.
 
general Paul von Lettow-Vorbeck who was buried with military honours.

SIMULIZI ZA NAIBU MKUU WA UTAMBUZI JESHI LA GHANA KUHUSU GERMAN EAST AFRIKA KTK VITA KUU YA KWANZA YA DUNIA

By the Ghana army's Dep. Chief of Defence intelligence , Big. Gen . James Hagan on Gold Coast Regiment battles in Germany East Africa (Tanganyika)...



View: https://m.youtube.com/watch?v=sl3Pl0I6Agc

SURA YA PILI

MAENDELEO YA RELI YA DAR-ES-SALAAM — LAKE TANGANYIKA

Hali ya kijeshi, wakati Kikosi cha Gold Coast kilipokea maagizo yake ya kuchukua uwanja huo, ilikuwa takriban kama ifuatavyo. Tanga, kituo cha pwani cha kaskazini zaidi ya reli mbili za Ujerumani, ilikuwa imeanguka muda fulani kabla, na njia nzima ya kutoka Moshi hadi baharini sasa ilikuwa mikononi mwa Waingereza.....


READ MORE : READ MORE : The Gold Coast Regiment in the East African Campaign, by Hugh Charles Clifford.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…