Sasa unafikiri Kila mtu ni lazima awe na pharmacy unafikiri tanzania hii maana tz Kila uchochoro pharmacy hii ni afya ya binadamu mzee sio Kila mtu afungue pharmacy hoja zako za kitoto sana kwahiyo watu wasije USA kisa pharmacy kufungua gharamaKufungua Pharmacy USA Gharama zinaweza kubadilika kutoka $250,000 hadi $1,800,000. tarajia gharama za kufungua kufikia $500,000 – $700,000
Hao ni mateja wa madawa hamna mwenyeji mwenye akili timamu ale barabarani acha uongo mzee
Unabisha kitu gani mzee unataka udanganye watu humu kuwa hao wasio na makazi wote ni wa kuja Methadone Mile, Boston niliona wengi tu wenyeji
Mzee nadhani hiyo Boston unayozungumiza ni ya huko kwenu mbeya itakua ulikua ndotoniUnabisha kitu gani mzee unataka udanganye watu humu kuwa hao wasio na makazi wote ni wa kuja Methadone Mile, Boston niliona wengi tu wenyeji
Una marafiki Wamarekani wale Wazungu hivi unafahamu namna gani wanalia na gharama za kuishi pale tena nchi yao waliozaliwa wenyewe? Unafahamu kisa cha Wazungu wengi kuishia kwenye ulevi na umalaya ni nini? Sababu ni maisha kuwa ghali sana kule usishangae babu wa miaka 90 anafumuliwa chemba na wahuni ili apate hela ya kunywa kahawa mana kuna baridi sanaSasa unafikiri Kila mtu ni lazima awe na pharmacy unafikiri tanzania hii maana tz Kila uchochoro pharmacy hii ni afya ya binadamu mzee sio Kila mtu afungue pharmacy hoja zako za kitoto sana kwahiyo watu wasije USA kisa pharmacy kufungua gharama
Mzee nadhani hiyo Boston unayozungumiza ni ya huko kwenu mbeya itakua ulikua ndotoni
SawaSasa Mbeya inahusianaje na hii mada, kama unabisha endelea kubisha ila ukweli ndio huo
Chemba kufukuliwa hata huko tanzania mbona kibao mnafukuliwa swala la gharama za maisha ni Kwa watu kama nyie ambao hamfanyi kazi lazima maisha yawe gharama kwenu ila kama unaofanya kazi ndani ya masala 6 tu unampunga wa maana ulifikiri huku ukifika utagawiwa tu pesa sioUna marafiki Wamarekani wale Wazungu hivi unafahamu namna gani wanalia na gharama za kuishi pale tena nchi yao waliozaliwa wenyewe? Unafahamu kisa cha Wazungu wengi kuishia kwenye ulevi na umalaya ni nini? Sababu ni maisha kuwa ghali sana kule usishangae babu wa miaka 90 anafumuliwa chemba na wahuni ili apate hela ya kunywa kahawa mana kuna baridi sana
Marekani ni ulaya ?Kikubwa nipo ulaya hayo mengine utajua wewe
Ngoja nikupe siri ya Marekani, pale maisha ni magumu sana ukiwa na hela unaweza kuwala wote, Marekani pale ukiwa na hela mwambie mtu njoo liwa na mbwa wangu nikupe hela atakuja haraka sana, wanashida na hela ndio maana hawajui maana ya neno dhambi, Mmarekani mfanye chochote umpe hela atakubaliChemba kufukuliwa hata huko tanzania mbona kibao mnafukuliwa swala la gharama za maisha ni Kwa watu kama nyie ambao hamfanyi kazi lazima maisha yawe gharama kwenu
Hata tanzania ukiwa na hela mbona unafokoa wengi tu tena huko ndio mnamaisha magumu sababu mpo dunia ya mwisho mzee halafu Mimi hamna Siri ya marekani utayonipa sababu siigizi nipo uwanjaniNgoja nikupe siri ya Marekani, pale maisha ni magumu sana ukiwa na hela unaweza kuwala wote, Marekani pale ukiwa na hela mwambie mtu njoo liwa na mbwa wangu nikupe hela atakuja haraka sana, wanashida na hela ndio maana hawajui maana ya neno dhambi, Mmarekani mfanye chochote umpe hela atakubali
Bei ya wastani ya kikombe cha kahawa Kwa ujumla, ukanda wa pwani una bei ya juu zaidi, ikiongezeka kwa $4.98 huko Hawaii na $3.88 huko California. The Great Plains ina bei ya chini kabisa, kwa $2.12 huko Nebraska na $2.56 huko Montana.Hata tanzania ukiwa na hela mbona unafokoa wengi tu tena huko ndio mnamaisha magumu sababu mpo dunia ya mwisho mzee halafu Mimi hamna Siri ya marekani utayonipa sababu siigizi nipo uwanjani
Unajua wewe akili hamna kichwani yaani kama mtu anafanya kazi masaa 6 tu analipwa $100 atashidwa kununua kikombe Cha kahawa Sasa piga hesabu huko tanzania raia wangapi wanaolipwa masaa sita $100Bei ya wastani ya kikombe cha kahawa Kwa ujumla, ukanda wa pwani una bei ya juu zaidi, ikiongezeka kwa $4.98 huko Hawaii na $3.88 huko California. The Great Plains ina bei ya chini kabisa, kwa $2.12 huko Nebraska na $2.56 huko Montana.
$100usd haitoshi kitu pale ukweli ndo huo bill ya maji na umeme sio sh mbili internet sio sh mbili bei ya kucharge gari pale unaijua kweli? Je bei ya parking kila siku, aseeUnajua wewe akili hamna kichwani yaani kama mtu anafanya kazi masaa 6 tu analipwa $100 atashidwa kununua kikombe Cha kahawa Sasa piga hesabu huko tanzania raia wangapi wanaolipwa masaa sita $100
unachosema ni sahihi!Kama una ndugu yako kule mwambie akutumie $500usd akituma niite mbwa
We kweli kilaza mtu mwenye gari USA anaingiza kipato zaidi ya $100 hapo nimekutolea mfano wa fukara wa marekani sio mtu mwenye kipato Cha kueleweka hivi mzee ulienda hata shule kidogo halafu mambo ya bili na maji umeme serikali inachukua Chao mwisho wa mwezi Kila nyumba kutokana na matumizi Yako naona wewe hata USA hujaishi ila unaigiza$100usd haitoshi kitu pale ukweli ndo huo bill ya maji na umeme sio sh mbili internet sio sh mbili bei ya kucharge gari pale unaijua kweli? Je bei ya parking kila siku, asee
Huduma za afya utapewa lakini kumbuka hela utakayolipia bima hapa bongo utapata boda nne ambazo ukiwapa vijana umetokaUmechukulia mambo kijumla mno mkuu.
Kama ilivyo kwingineko, Marekani kweli maisha siyo lelemama kama hukupiga shule ya maana; na huna mishe za kueleweka. Pamoja na hayo, kwa maoni yangu, wanatuzidi katika mambo makubwa manne.
1. Kule hakuna hii rushwa na ufisadi huu wa kihayawani. Mambo mengi unajifanyia mwenyewe kwenye mtandao tu na mambo yanakwenda. Mtu unaagiza pasipoti yako online siku ya siku unaitwa unakwenda kuchukua tu...Challenge kubwa kwangu ukirudi huku Bongo ni hii ya kujuana na kila mtu ndiyo upate huduma. Hospitali uwe na mtu wako. Polisi. Kila ofisi yaani. Inachosha balaa na mtu unaweza kukata tamaa!
2. Mambo ya afya. Japo bima ipo juu kama siyo mwajiriwa wa serikali za majimbo au federal lakini kwenye dharula angalau una uhakika wa kuhudumiwa; na mengine mtajuana baadaye. Kama ingekuwa ni Marekani huyu dogo wa SUA hapa chini sidhani kama angekata moto maana medical malpractice ambayo hiyo hospitali wangepata si ajabu hata wangefilisika!
DOKEZO - Uzembe wa Hospitali Kuu ya Mkoa Morogoro umesababisha kifo cha Mwanafunzi wa SUA
Juzi usiku tulimpeleka hospitali ya Nanguji mwanachuo mwenzetu ambae alizidiwa, wakamfanyia vipimo na kusema utumbo umejikunja hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kwa haraka, kwa pale gharama zilikuwa ni laki 8 hivyo tukaombwa kupelekwa hospitali ya mkoa kwasababu ya unafuu wa matibabu, tukapewa...www.jamiiforums.com
Jana pale Mbezi mwanamke mmoja akaanguka. Medical emergency ile lakini hakuna aliyemjali maana hakuna aliyejua cha kufanya. Marekani 911 ilishapigwa na ndani ya dakika 5 wameshafika kutoa huduma ya kwanza huku chumba cha emergency huko anakopelekwa kimeshaandaliwa. Kama ni stroke ndani ya robo saa kichwa kimeshafunguliwa wanatafuta hiyo blood clot iko wapi. Huku kama huna pesa unakufa tu kibudu na hakuna anayejali. Sijui kama mama yule alipona. Msaada pekee aliopata ni kumwagiwa maji ya baridi kichwani! 😳
3. Elimu! Elimu! Elimu! Na hili nadhani halihitaji maelezo mengi. Elimu yetu hapa ni ya hovyo sana. Ndiyo maana hata akina Kishimba utawasikia wanakandia wasomi bungeni lakini watoto wao wote wamesoma nje!
4. Social security. Kwamba hata hawa homeless walioko barabarani wengi wao wanapata vihela angalau vya kuwasukuma sukuma japo kwa chakula na mahitaji mengine ya msingi. Sisi ukiwa masikini kabisa kufa tu; na hakuna anayejali.
Shida kubwa ya Marekani ni ukweli kwamba 1% ya wale ultra rich wanamiliki utajiri wa karibia 95% ya watu wote. Na sijui mgawanyo huu wa matabaka ni sustainable kwa muda gani. Wengi wameanza kumkumbuka Karl Marx aliyesema kwamba kwa vile ulafi wa binadamu wa kujilimbikizia mali hauna kikomo, itafika mahali njia kuu za uchumi zitakuwa mikononi mwa watu wachache sana huku umma ukiwa hauna kitu. Na hili hatimaye litepelekea kuanguka kwa mfumo mzima wa kibepari. Ndiyo maana utaona japo ni ubepari pure lakini wanajaribu kuchomekea vielementi vya kijamaa mf. Msaada kwa watu masikini, kusamehe mikopo ya elimu, huduma za bure kwa wanawake wenye mimba n.k. japo wahafidhina wa Republicans huwa wanapinga sana.
Kwa hivyo ukienda Marekani nenda ukiwa open minded. Kafanye kilichokupeleka huko na kama siyo mjanja huku mtaani basi kazingatie sana shule vinginevyo utakuja kuishia tu kuwa mlevi na huna hata vibali vinavyokuruhusu kufanya kazi. Unaingia kwenye vicious cycle mbaya sana ambayo kujichomoa ni shughuli pevu maana ukitoka tu hutarudi tena kama viza iliyokupeleka ilishaisha; na nyumbani huku unaogopa kurudi maana wenzio uliowaacha utawakuta wamepiga hatua sana kimaisha.
It is a delicate balancing act hasa kama una emotional IQ ndogo na maisha yako yanatawaliwa na kujilinganisha na wengine na kufuata fomyula kwamba ukiwa na miaka fulani ni lazima uwe na hiki na kile.
Kama umesomea mambo ya afya (MD, RN, Pharmacology...) fanya kila uwezalo uende Marekani. Mengine utapambana huko huko!
Kama uko vizuri kwenye mambo ya IT/Computer Science we nenda tu. Mengine mtajuana huko huko...na mengineyo!