Kwa wale wanao fuatilia mchakato wa bunge maalumu la katiba washanifahamu. Kuna mambo yanayoendelea yanayoshadidisha kuwa mchakato wote wakutafuta rasimu ulikua Bure 1. Mtu ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa au kuna dalili kuwa mafisadi tayari wana mkono wao. 2. Hakuna nia thabiti au mujaradi ya kupata katiba mpya! ""Rejea msimamo Wa chama tawala " au rejea mbilingembilinge za kuamua kura ya kuchagua mwenyekiti Iwe ya Siri au ya wazi! 3. Badala ya kuzungumzia rasimu na mchakato wa kupata mwenyekiti bora wajumbe wakaanza kuzungumzia posho! Mshanifahamu! 4. Sasa ndugu zangu ombeni watu wasio na viwango wapite' wakipita tutajuta miaka! Mshanifahamu ? 5. Mbaya zaidi watanzania wengi si wafatiliaji Wa siasa hasa watu Wa bara tofauti name Zanzibar. Mshanifahamu? Dalili za kuliwa naziona. Mshanifahamu