Watanzania na Viongozi wa Dini tufunge na kuliombea hili Taifa

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Sitaki kunyoosha kidole kwa mamlaka maana nina imani kila mamlaka inawekwa na Mungu. Iwe mbaya au nzuri ila anaye isimika ni Mungu pekee iwe kwa wizi wa kura ama kwa namna yoyote bado Mungu ndie anaye ziweka mamlaka nakuzipa ridhaa kuwaongoza watu. Yes kama Mungu angakuwa sio anaye bariki mambo kutokea asinge ruhusu Uzaliwa wa kwanza wa Esau uwende kwa Yakobo. Ndio Yakobo alichukuwa baraka za nduguye kwa kupata taarifa toka kwa mama alie vujisha siri ya kumbariki Esau.

Ndivyo ktk siasa wananchi tunagombana na kuumizana ila watu wamesha peana urithi wa kwanza.

Kifo cha Rais wa Tano wa Taifa hili sio kifo ambacho tunaweza kukichukulia cha kawaida nikifo chenye mambo mengi yakufikirisha na sisi tunasema kazi ya Mungu haina makosa.

Hayati Magufuli ameondoka tumebaki sisi na watoto wetu na kama angekuwa hai akapewa nafasi ya mwisho kuongea angesema Watanzania msinililie mimi ila jililieni ninyi na watoto wenu.

Utabiri unaonyesha zipo nyakati ngumu tutaziendea pasipo kufunga na kuombea hili taifa hali itakuwa mbaya zaidi. Maamuzi magumu sana yapo mbeleni msiniulize maamuzi gani ila chukueni haya maono tunayo yaona na tusio yaona Mungu ndio anaye juwa.

Tupo karibu nakujaa kikombe na mwisho kumwagika ndugu zangu ombeeni Taifa Ombeeni Mungu atupe viongizi wazuri wenye nia ya dhati kuliongoza Taifa pasipo kujali dini au kabila la mtu.

Hili taifa sii mali ya mtu au chama au taifa au kabila au dini fulani hili ni taifa la watanzania ndani yake wakiwemo Watanganjika na Wazanzibari kuwa na fikira Taifa hili ni mali ya watu ni kitisho kwa uchumi na ustawi wa watanzania.

Nilazima tuwa na Tanzania mpya chini ya mwamvuli wa Mungu tuna muamini.

Ndugu zangu mimi napenda hii kauli yajayo yanafurahisha wana maombi tupige spana Mungu huyu ashuke na aonyeshe utukufu wake. Amen
 
kama angekuwa hai akapewa nafasi ya mwisho kuongea angesema Watanzania msinililie mimi ila jililieni ninyi na watoto wenu.
... kiburi cha uzima na madaraka alichokuwa nacho wala kisingemwacha kutamka hivyo wewe! Ni unyenyekevu wa hali juu mno kutamka hayo maneno mbele za watu sembuse watesi wako!
 
Mbona unatutisha, sasa tunapokuwa tunaombea tuwe tunasema maneno gani?!
 
Mkuu wewe hivi uchoki kulialia!?

Maana tangu Samia aingie ghafla umekuwa mrithi wa shekh Yahya kwa utabiri usiotimia!

Umekuwa Kama fisi anayesubiria mkono wa binadamu uanguke!
 
Kweli nchi hii ngumu, wewe mtu wa Mungu kama unamwona Magufuli kuwa shujaa pamoja na mauaji, ubaguzi wa kikabila, wizi mkubwa wa fedha kupitia tenda za kulazimisha, uongo, visasi, n.k., basi kweli Tanzania tunahitaji kuombewa.
 
Amen, hakika tunaihitaji maombi zaidi kuweza kuliokoa taifa hili mkuu, unamengi ya kusema ila umeyatunza moyoni, linahitajika jicho la tatu au maono zaidi mtu kukuelewa.
 
Aya ya MWISHO umeharibu,
Kwamba unapenda kauli hii, "yajayo yanafurahisha", afu tupige spana?
Mara nyingine Nchi hupigwa Kwa magonjwa au majanga Kwa makosa ya viongozi wao,
Mimi sipendi mabaya yatupate.
Namuomba Mungu awape moyo wa nyama, wasikize vilio na mateso ya wananchi,
WATUBU na kubadilika mapema, wasisubiri mabaya yatokee.
Ameeeeeeeen.
 
Tumwombe Mwenyezi Mungu, lakini mambo mengine ni uzembe wetu.

Kiongozi mkishamchagua anawafanya mateka na watumwa wake, anaweza kuamua au kufanya lolote na hakuna wa kumkosoa,
Zaidi ataandaa chawa wa kusifia kila jambo baya au zuri,

Hali hii sio kwa watawala tu hata viongozi wa upinzani pia,
 
Sitaki kunyoosha kidole kwa mamlaka maana nina imani kila mamlaka inawekwa na Mungu. Iwe mbaya au nzuri ila anaye isimika ni Mungu pekee iwe kwa wizi wa kura ama kwa namna yoyote bado Mungu ndie anaye ziweka mamlaka nakuzipa ridhaa kuwaongoza watu. Yes kama Mungu angakuwa sio anaye bariki mambo kutokea asinge ruhusu Uzaliwa wa kwanza wa Esau uwende kwa Yakobo. Ndio Yakobo alichukuwa baraka za nduguye kwa kupata taarifa toka kwa mama alie vujisha siri ya kumbariki Esau.

Ndivyo ktk siasa wananchi tunagombana na kuumizana ila watu wamesha peana urithi wa kwanza.

Kifo cha Rais wa Tano wa Taifa hili sio kifo ambacho tunaweza kukichukulia cha kawaida nikifo chenye mambo mengi yakufikirisha na sisi tunasema kazi ya Mungu haina makosa.

Hayati Magufuli ameondoka tumebaki sisi na watoto wetu na kama angekuwa hai akapewa nafasi ya mwisho kuongea angesema Watanzania msinililie mimi ila jililieni ninyi na watoto wenu.

Utabiri unaonyesha zipo nyakati ngumu tutaziendea pasipo kufunga na kuombea hili taifa hali itakuwa mbaya zaidi. Maamuzi magumu sana yapo mbeleni msiniulize maamuzi gani ila chukueni haya maono tunayo yaona na tusio yaona Mungu ndio anaye juwa.

Tupo karibu nakujaa kikombe na mwisho kumwagika ndugu zangu ombeeni Taifa Ombeeni Mungu atupe viongizi wazuri wenye nia ya dhati kuliongoza Taifa pasipo kujali dini au kabila la mtu.

Hili taifa sii mali ya mtu au chama au taifa au kabila au dini fulani hili ni taifa la watanzania ndani yake wakiwemo Watanganjika na Wazanzibari kuwa na fikira Taifa hili ni mali ya watu ni kitisho kwa uchumi na ustawi wa watanzania.

Nilazima tuwa na Tanzania mpya chini ya mwamvuli wa Mungu tuna muamini.

Ndugu zangu mimi napenda hii kauli yajayo yanafurahisha wana maombi tupige spana Mungu huyu ashuke na aonyeshe utukufu wake. Amen
Tuombee Tupate Katiba mpya itokanayo na RASIMU ya Judge Warioba kabla haijachakachuliwa na kuwa Katiba PENDEKEZWA.

Roho ya visasi na kuviziana IKOME ktk Nchi yangu nzuri Tanzania.

Ameeeen.
 
Amen, hakika tunaihitaji maombi zaidi kuweza kuliokoa taifa hili mkuu, unamengi ya kusema ila umeyatunza moyoni, linahitajika jicho la tatu au maono zaidi mtu kukuelewa.
Rekebisha hapo kwenye JICHO la TATU, JICHO la TATU ni njia itumiwayo na watu wa GIZA kuingia Ulimwengu wa Roho.

Ulimwengu wa Roho ni mmoja bt zipo njia mbili za kuingia huko.

1. Kupitia GIZA, UCHAWI, meditation,freemasonry, UGANGA nk.

2. Kupitia MAOMBI kupitia ROHO wa KRISTO au Roho mtakatifu.

Kupitia njia hii unatimia "MACHO MAWILI" ya Rohoni, Wala Si JICHO moja. Mtu wa ndani ana macho mawili kama mtu wa nje "mwanadamu alivyo na mawili.

JICHO'' la tatu ni la SHETANI na MASSIH JADAL au mpinga Kristo.

Ameeeeen.
 
Aya ya MWISHO umeharibu,

Kwamba unapenda kauli hii, "yajayo yanafurahisha", afu tupige spana?

Mara nyingine Nchi hupigwa Kwa magonjwa au majanga Kwa makosa ya viongozi wao,

Mimi sipendi mabaya yatupate.

Namuomba Mungu awape moyo wa nyama, wasikize vilio na mateso ya wananchi,

WATUBU na kubadilika mapema, wasisubiri mabaya yatokee.

Ameeeeeeeen.
Umenena, umemaliza..

Walio wa Mungu Yehova, watoto wake waliozikana nafsi zao na kujiweka chini ya maongozi yake katika Kristo Yesu, hawatahayaliki wala kutishika na chochote...

Tunalindwa na kukumbatiwa naye kama kuku akumbatiavyo vifaranga wake...

Na NENO lake linasema;

YEREMIA 1: 8
"... usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA..."

Na tena imeandikwa;

ZABURI 91

MSTARI WA 1
"...Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu, Atakaa katika UVULI wake Mwenyezi..."

MSTARI WA 4
".....kwa manyoya yake atakufunika, chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kibao..."

Huu ndiyo urithi wa wote walio wake, wale wenye haki na waliyoipokea neema ya ukombozi ktk Kristo Yesu..

MSITISHWE wala MSIOGOPESHWE kwani aliye upande wetu ni mkuu sana na mwenye nguvu sana kuliko aliye upande wao. Tumwamini tu, baaasi. Ameeeeni!!
 
Sitaki kunyoosha kidole kwa mamlaka maana nina imani kila mamlaka inawekwa na Mungu. Iwe mbaya au nzuri ila anaye isimika ni Mungu pekee iwe kwa wizi wa kura ama kwa namna yoyote bado Mungu ndie anaye ziweka mamlaka nakuzipa ridhaa kuwaongoza watu. Yes kama Mungu angakuwa sio anaye bariki mambo kutokea asinge ruhusu Uzaliwa wa kwanza wa Esau uwende kwa Yakobo. Ndio Yakobo alichukuwa baraka za nduguye kwa kupata taarifa toka kwa mama alie vujisha siri ya kumbariki Esau.

Ndivyo ktk siasa wananchi tunagombana na kuumizana ila watu wamesha peana urithi wa kwanza.

Kifo cha Rais wa Tano wa Taifa hili sio kifo ambacho tunaweza kukichukulia cha kawaida nikifo chenye mambo mengi yakufikirisha na sisi tunasema kazi ya Mungu haina makosa.

Hayati Magufuli ameondoka tumebaki sisi na watoto wetu na kama angekuwa hai akapewa nafasi ya mwisho kuongea angesema Watanzania msinililie mimi ila jililieni ninyi na watoto wenu.

Utabiri unaonyesha zipo nyakati ngumu tutaziendea pasipo kufunga na kuombea hili taifa hali itakuwa mbaya zaidi. Maamuzi magumu sana yapo mbeleni msiniulize maamuzi gani ila chukueni haya maono tunayo yaona na tusio yaona Mungu ndio anaye juwa.

Tupo karibu nakujaa kikombe na mwisho kumwagika ndugu zangu ombeeni Taifa Ombeeni Mungu atupe viongizi wazuri wenye nia ya dhati kuliongoza Taifa pasipo kujali dini au kabila la mtu.

Hili taifa sii mali ya mtu au chama au taifa au kabila au dini fulani hili ni taifa la watanzania ndani yake wakiwemo Watanganjika na Wazanzibari kuwa na fikira Taifa hili ni mali ya watu ni kitisho kwa uchumi na ustawi wa watanzania.

Nilazima tuwa na Tanzania mpya chini ya mwamvuli wa Mungu tuna muamini.

Ndugu zangu mimi napenda hii kauli yajayo yanafurahisha wana maombi tupige spana Mungu huyu ashuke na aonyeshe utukufu wake. Amen
Mwamba huwa nakuamini sana 🙏🙏🙏
 
Umenena, umemaliza..

Walio wa Mungu Yehova, watoto wake waliozikana nafsi zao na kujiweka chini ya maongozi yake katika Kristo Yesu, hawatahayaliki wala kutishika na chochote...

Tunalindwa na kukumbatiwa naye kama kuku akumbatiavyo vifaranga wake...

Na NENO lake linasema;

YEREMIA 1: 8
"... usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA..."

Na tena imeandikwa;

ZABURI 91

MSTARI WA 1
"...Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu, Atakaa katika UVULI wake Mwenyezi..."

MSTARI WA 4
".....kwa manyoya yake atakufunika, chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kibao..."

Huu ndiyo urithi wa wote walio wake, wale wenye haki na waliyoipokea neema ya ukombozi ktk Kristo Yesu..

MSITISHWE wala MSIOGOPESHWE kwani aliye upande wetu ni mkuu sana na mwenye nguvu sana kuliko aliye upande wao. Tumwamini tu, baaasi. Ameeeeni!!
Ameeen.
 
Mkuu

Maamuzi magumu unayozungumzia nadhani ni kiti kutokalika KWA mkaaji wa hicho kiti!!ndipo mamlaka NZITO itataka akae mwingine kabisa tena asetarajiwa na WENGI!!

Kiti kutokalika dalili zinaanza kuonekana mapema KABISA!mfumuko wa Bei,njaa ya chakula NCHINI itaenda kusababisha kitu kiwake Moto KWA mkaaji ndipo aimbe poo na maamuzi kuchukuliwa!!!

Wazee wa jadi wa kisukuma kanda za HUKU ukipiga nao story wanasema mvua itakapoanza kunyesha tu ya mwaka huu hasa mwishoni mwa mwaka vugu vugu litaonekana!

Tena wameongeza eti huyu anakaa KWA muda kitini atampisha ajaye anapaswa kukikalia sawasawa!!

Mimi kilio changu sio mkaliaji kiti bali ni hiki hapa;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA Mpya"
 
Back
Top Bottom