Uchaguzi 2020 Watanzania ni waelewa sana, 2020 tunachagua maendeleo

Uchaguzi 2020 Watanzania ni waelewa sana, 2020 tunachagua maendeleo

CCM wakienda ulaya kupiga magoti kuwalilia wazungu kuomba omba misaada huwaita majina haya, wahisani wafadhili, cha ajabu na cha kushangaza hao hao wazungu wakiona CCM wanakiuka haki za binadamu wakaanza kuwakemea huanza kuwaita wanaume wenzao mabeberu utazani CCM ni mbuzi jike
 
Sababu sio mtoto wa miaka ya themanini nikakariri siasa wakati namezaliwa wakati wakudai uhuru
Endelea kukumbatia Tabia mbovu mliyoanzisha ya kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani lakini mkumbuke hakuna mabaya yasiyo na mwisho, ipo siku ubaya wenu utafika kikomo wapo wapi akina chiluba, Bokasa, Gadafi, Sadam Hussein, Abacha, All-Bashiri, mabutu, idd Amin Dada na wenzao waliokuwa na roho mbaya zaidi?
 
Hakuna kitu kibaya Duniani kama uonevu kuwaonea watu Kuwabambikia kesi unyanyasaji hujuma huleta chuki kubwa kwenye jamii
 
Nchi ina zaidi ya miaka 50 hakuna maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani badala ya kujenga viwanda kila kata, vyuo vikuu kila wilaya, Hosptal za rufaa kubwa zenye madaktari Bingwa kila mkoa, barabara vijijini kote, daraja toka Dsm mpaka Zanzibar na pemba iwe Taifa lenye maendeleo level ya Marekani, China, Japan, German, Rusia, UK, Oman na mataifa yote Tajiri, isingekuwa ni CCM wapo madarakani mda huu hata makao makuu ya UN yangeweza kuwa yapo Tanzania, pesa zote za maendeleo zinapotelea kwenye mambo yasiyo na Tija kwa Taifa, kudidimiza demokrasia, kuihujumu chadema kudhoofisha upinzani kutaka kurejesha mfumo wa chama kimoja, kuwalipa mabilioni cyprian Musiba le mutuz na wengineo watengeneza propaganda za kishamba shamba.
Nikisema wewe Ni mtoto na hujui lolote sikosei unataka tufanane na ulaya wakati wanajitawala Karne ya 9 unazungumzia marekani wamepata Uhuru wao zaidi ya miaka 250 iliopita,unazungumzia Oman mtawala wa bahari ya Hindi yote kuanzia Mombasa Zanzibar mzizima(ambayo ndio dar es salaam) kilwa bagamoyo mpaka pwani zote za Mozambique na miji yote iliyo pwani kwa zaidi ya miaka Mia mbili na sisi ambao tumepata Uhuru ndani ya miaka sitini?
 
CCM wakienda ulaya kupiga magoti kuwalilia wazungu kuomba omba misaada huwaita majina haya, wahisani wafadhili, cha ajabu na cha kushangaza hao hao wazungu wakiona CCM wanakiuka haki za binadamu wakaanza kuwakemea huanza kuwaita wanaume wenzao mabeberu utazani CCM ni mbuzi jike
CCM mabeberu wanaijua haiombi toka tuna tumia pesa zetu kuwapiga mabeberu na kuwaondoa mosambique Angola Zimbabwe botwasana nk tunafanya biashara tu na mabeberu sio chadema mawakala wa mabeberu mpaka lisu kawa mpenzi wa jinsia moja ili tu kuwaradhishisha mabwana zake
 
Hakuna kitu kibaya Duniani kama uonevu kuwaonea watu Kuwabambikia kesi unyanyasaji hujuma huleta chuki kubwa kwenye jamii
Mhalifu lazima ashughulikiwe ikiwa baba na mama yako anashugulikiwa kwa uhalifu wake unashangaa nini wajasiriasiasa wa Cha Domo aka chadema wasishugulikiwe?
 
Watanzania tunayo fursa tena ama kuchagua maendeleo yaliyodhahili au ahadi za kusadikika. Ninawaamini watanzania watamchagua tena JPM ili waendelee kupata maendeleo. Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020- 2025 naiona ni bora na inatekelezeka!
 
Watanzania tunayo fursa tena ama kuchagua maendeleo yaliyodhahili au ahadi za kusadikika. Ninawaamini watanzania watamchagua tena JPM ili waendelee kupata maendeleo. Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020- 2025 naiona ni bora na inatekelezeka!
 
*WATANZANIA NI WAELEWA SANA, 2020 TUNACHAGUA MAENDELEO*

Na Emmanuel J. Shilatu

Uchaguzi Mkuu 2020 unazidi kukolea na kupamba moto ambapo kila chama, kila mgombea anajinadi kivyake kwa sera zake. Hapa ndipo penyewe.

Kuna chama kinahubiri JPM asichaguliwe tena kwa sababu analeta maendeleo ya vitu pasipo maendeleo ya Watu. Hapa ndipo ulaghai wa si-hasa unapoanzia.

Hivi inawezekana vipi kuwa na maendeleo ya Watu bila ya kuwa na maendeleo ya vitu? Unatofautishaje maendeleo ya vitu na maendeleo ya Watu? Mathalani ukinunua gari hayo yatakuwa maendeleo ya kitu au ya Mtu?

Mwanasiasa huyo huyo anayepinga maendeleo ya vitu ndio huyo huyo amepanda gari toka kwake kuna lami mpaka uwanja wa ndege kupanda Air Tanzania ya kumuwahisha hotelini kufanya mkutano na Waandishi wa habari! Hapo anatengaje maendeleo ya vitu na maendeleo ya Watu? Kama haoni vitu ni maendeleo ya Watu angepanda Punda toka Kijijini kwake akaenda chini ya Miti kufanya mikutano kila mahali!

Ukweli unabakia pale pale hakuna maendeleo ya Watu bila maendeleo ya vitu. Hauwezi ukasema Watu wa nchi yangu wana maendeleo bila ya kuwa na maendeleo ya vitu kama vile miundombinu bora ya barabara, viwanja vya ndege, reli ya kisasa ya SGR, Madaraja kama ya Mfugale na ya Ubungo, Mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme kama ule wa Mto Rufiji unaozalisha megawatts 2115; Bila ya kuwajengea Zahanati, Vituo vya afya, hospitali; Au kuwajengea shule, hostel na vyuo; Ama kuwa na maendeleo ya ndege za kisasa kama ndege 10 zilizonunuliwa na Rais Magufuli kwa kipindi cha miaka 5 tu.

Watanzania ni waelewa sana, tunajua hakuna maendeleo ya Watu bila ya kuwa na maendeleo ya vitu kama vilivyoanza kuletwa na Rais Magufuli.

Kuna chama sera yao kubwa ni "Kazi na Bata" yaani wakifika Ikulu ni mwendo wa "Bata" tu yaani starehe kwa kwenda mbele. Hilo Bata linawahusu Wapiga kura Watanzania wote ama ni wao peke yao?

Kwanza kabisa neno "Bata" tu ni neno la kihuni kama yalivyo maneno mengineyo ya kihuni yasiyo na heshima wala staha. Kutumia neno la kihuni ni kufikiria Watanzania wote ni Wahuni. Haya ni matusi makubwa yasiyokubalika.

Tanzania ni nchi ya kistaarabu na pia Ikulu sio bar, club ama Casino ya kufanyia starehe na anasa. Ni sehemu ya heshima kwa ajili ya kulijenga Taifa kwa kuliletea maendeleo.

Watanzania hatuhitaji mambo ya kihuni, Watanzania tunahitaji maendeleo.

Chagua Maendeleo
Chagua Magufuli
Chagua Chama Cha Mapinduzi (CCM)

*Shilatu E.J*View attachment 1530022
nimependa ulivyoweza kumnadi ndugu mombea wa ccm, ni wazi mengi yametendeka. ila tusijisahaulishe kuwa ni wajibu wa serikali yoyote ile iwapo madarakni,kuhakikisha inaleta maendeleo chanya kwa watu wake. kwanini uongozi uliopita haukufanya? mimi nawe tuhoji. kazi na bata,,umezungumzia bata ni neno la kihuni,je unaukweli wa kisayansi kuhusu uhuni wa neno bata? mbona dhana ya kazi hujaigusia kabisa? oky..lets wait.
 
Back
Top Bottom