Diamondplatnumz ni msanii maarufu na mwenye mafanikio makubwa kwa sasa Tanzania na hata Africa.
Kitu ambacho nimekuwa nikijiuliza, Diamond pamoja na Harmonize kulindwa na Mabaunsa zaidi ya mmoja hali ya kuwa usalama nchini kwetu si wa kutisha kihivyo kama Somalia au Mogadishu, Je hizi ni sifa za umaarufu au ni jeuri ya pesa ama ni jambo jema kwa usalama wao?
Kwa mfano jana kwenye msiba wa Ruge harmonize na Diamond wamefanya jambo jema sana kwenda. Lakini kulimuwa na haja gani ya kwenda na msululu wa Mabaunsa hali ya kuwa Pale kulikuwa na viongozi wakubwa wa serikali Raisi pamoja na Raisi msitafu mana yake ulinzi uliokuwa pale ni wakutosha sana.
Mi nadhani hawa madogo wajifunze jinsi ya kwenda misibani pale sio sehemu ya show off mbona hatukuona matajiri wengine na watu maarufu hawana mabodigadi kama vile au wao wana maadui wengi sana?
Matokeo yake wameshindwa hata kuaga mwili wa marehemu hatujui kama walizuiliwa kwa sababu ipi Lakini diamond pamoja na Management yake lazima wajue jinsi ya kwenda kwenye public mbona mbona wasanii wenzao hawana hizi drama au wao hawana hela?
Punguza sifa za umaarufu mwisho wa siku haya maisha tu hata ulindwe vipi siku kifo hakikwepeki.
Sent using
Jamii Forums mobile app