Yote tisa, kumi kanishanga Mrisho Mpoto!!
Hivi Mpoto anafahamu kwamba Ruge alikuwa bosi namba mbili pale Clouds?
Hivi Mpoto anafahamu kwamba Joseph Kusaga ndie bosi namba moja pale Clouds?
Hivi Mrisho Mpoto anafahamu kwamba Diamond anamiliki 45% ya hisa za Wasafi TV na ndio CEO wa Wasafi?
Hivi Mpoto anafajhamu kwamba Joseph Kusaga, au mke wa Joseph Kusaga anamiliki 53% ya hisa za Wasafi TV na kwamba ndie majority shareholder wa Wasafi TV?
Sasa hivi huyu Mpoto anaamini kabisa kwamba Diamond na Kusaga hawakuongea in advace kuhusu kutokwenda kwake pale msibani?!
Hivi huyu Mpoto kabla ya ku-post kumtaka Diamond aende msibani anadhani Kusaga hakuwa amekubaliana na sababu za yeye kutokwenda?!
Hivi huyu Mpoto hata kama alidhani Kusaga hakukubaliana na suala la Diamond kutokwenda pale, anadhani hakumshawishi aende just for image?!
Hivi huyu Mpoto kama Kusaga alimshawishi Diamond lakini Diamond hakumsikiliza boss mwenzake, ndo angemsikiliza yeye mtembea peku peku?!
Bado sijafahamu alikuwa anatarajia ku-achieve nini hasa kwenye post yake ile!!
Kwamba, hata kama kumbe Diamond alikuwa amepanga aende siku fulani na hiyo siku inadondokea baada ya Mrisho ku-post; kwahiyo ndo angeamini kasikilizwa yeye "kama kaka", au?!