itakiamo
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 893
- 1,739
Kuna ajali ya lori la mafuta imetokea hapa Mzambarauni , Morogoro.
Kitu kilichonishangaza ni uwepo wa watu ambao wamejiandaa kabisa kwa kuchota mafuta wakati si miaka mingi naeneo hayo hayo palitokea vifo halaiki kutokana na moto August 2019.
Kitu kilichonishangaza ni uwepo wa watu ambao wamejiandaa kabisa kwa kuchota mafuta wakati si miaka mingi naeneo hayo hayo palitokea vifo halaiki kutokana na moto August 2019.
Wakuu,
Lori la mafuta lenye usajili T 257 EAU limepata ajali asubuhi ya leo maeneo ya Mzambarauni, Manispaa ya Morogoro, likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Njombe.
Kufuatia ajali hiyo, wananchi walifurika kuchota mafuta, hali iliyozua taharuki kutokana na kumbukumbu ya ajali kama hiyo iliyotokea miaka mitano iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, likishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, lilifanikiwa kudhibiti hali hiyo.
Mrakibu Msaidizi Daniel Ibrahim Myalla amewaonya wananchi dhidi ya kukimbilia kuchota mafuta kwenye ajali kama hizi, akisisitiza kuwa ni hatari na inaweza kusababisha mlipuko na vifo.