Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?

Update teuzi upumzike
 
Sasa kama huwezi kuitetea Bandari ndio utaweza kutengeneza Katiba?

Bure kabisa!
Katiba hii ya rais kuteua kila nafasi ya uongozi, kutokupingwa matokeo ya uchaguzi mahakamani, sifa ya ubunge kujua kusoma na kuandika tu. Aisee issue ya bandari ni ndogo sana ukilinganisha na madudu yaliyopo kwenye katiba ya mkoloni.

Bandari ijadiliwe lakini katiba mpya iwe first priority.
 
Kuwaambia uongo wengine ni hatari kama kuwapiga kwa shoka, kuwajeruhi kwa upanga, au kuwapiga risasi au kuwachoma kwa mshale mkali.

Proverbs 25:18

Kile ambacho tumeambiwa katika siku za hivi karibuni kinaweza kuitwa uongo

.....
Mfano mzuri ni Nini / ilikuwa inajadiliwa, inadhaniwa, ni MOU au kama inajulikana sasa IGA na tukaja/ tulitaarifiwa , IGA haina nguvu kwa nguvu zake ila kwenye HGA zifuatayo tunauwezo wa kurakabisha mazito ya IGA na kwa hivyo tuliuaswa kupuuza umuhimu na au athari inayoweza kutokea kupunguza nguvu za uhuru wetu(sovereign powers)?. Kwa kusikitisha, kinyume chake ilikuwa ukweli, kwamba, MOU au IGA huathiri kwa kiasi kikubwa uhuru(sovereign)wetu hadi kufikia hatua ya kupunguza nguvu ya sheria yetu mama, Katiba... humo.utaona shoka upanga na risasi zimepigwa[kwa kukosa tafsiri] kwa saiiki(pysche)ya Taifa letu! Ni aibu kwa taifa letu.

Nini kilichofanyika? Binafsi najiuliza ni Kwanini Wananchi wamefikia hapa na ninajifariji na majibu yangu mwenyewe kwa kuongeza na za Wanafalsafa.
Mosi,
"Ni ukweli unaojulikana wa kisaikolojia kwamba maono yetu ya iwezekanavyo(possibilities) yanaundwa na kile tunachofikiria(imaginations) au kuona(vision) uwezo(capacity) kuwa.

Ukubwa wa mawazo yetu au mtazamo(perception)wetu wa uwezo(capacity) wetu, itakuwa maono(vision) yetu ya iwezekanavyo(possibilities). Kinyume chake, mawazo yetu madogo au mtazamo wa uwezo wetu, itakuwa ni kuyashusha maono yetu ya iwezekanavyo.

Kwa ndoto yoyote au maono ya kuwa na watu au taifa, maono yake ya uwezekano na mawazo yake au mtazamo wa uwezo wake lazima yawe na uhusiano mzuri. [Coordinated and correlated Vision] Kama watu au maono/dira ya taifa ya iwezekanavyo/yawezekanayo na mawazo yake au mtazamo wa uwezo wake ni hasi, basi ni sawa na kujiachia kupigwa shoka, upanga, risasi na mshale kwenye eneo moja... Uchungu wake ndio hizi wanasiasa wanazoziita "kelele" manake ni machungu yanayoelezeka kwa aina yake ya kipekee. Ni mayowe haswa.

Pili,tuliyokuwa tumeanza kuyaamini, kuwa yanayowezekana,tuliyoyafikiria na tukaanza kuyaona tukayaona, yalipigwa vita sana , kuwa yote hayakuwa, kwamba mafanikio tuliyoyapata hayakuwa mafanikio!
Hilo nalo lilikuwa na kama Jeruhi lingine tu la shoka, upanga risasi na mshale, tena kwenye kidonda kilekile chan kwanza walichopata mababu zetu!
Mashallah!
Sasa basi, kwa haya yanayoendelea ni sawa na kusema, Taifa letu limekosa dira, kuwa our imagination, our capacity of the possible zimeyayuka ghafla. Hii ndio Tanzania nionavyo leo hii. Hakuna Mtanzania wa ajabu....Ajabu ni our Imagination, our perception and our perceived capacity has been trampled, historically by the people whom we have resented. Watu waliowatesa mababu zetu, haijalishi....Mzungu, Mwarabau, au beberu wa aina yeyote ile. Itoshe kusema, maamuzi na mwelekeo Serikali ya SsH inapotupeleka ni sawa na kutugeuzia upande wa jeraha kuunyukwa tena kwa shoka , upanga, risasi na nchale! Hiyo ndio ajabu!
Tumepata ulazima gani ghafla hata kujishusha namna hii?

Lazima turudi mezani.
We need to perpetuate a self reliant Dynamism
Tunahitaji kujenga uwezo wa kujitegemea. Bila ya kuwakumbatia wanyonyaji!

Nimalizie na mstari mfupi,...
Njia yako ilipita baharini, na njia yako kupitia maji makuu, ni njia ambayo hakuna mtu aliyejua ilikuwa huko~
Zaburi 77:19


Kumbuka katika hali zote wakati giza imetamalaki na matumaini yote yamepotea, Mwenye nguvu anaongoza

Aluta Continua.
 
Mkataba ungekuwa unasema hivyo kama anavyosema waziri mkuu Kassim Majaliwa tusingelalamika.
Ile ni IGA, sio mkataba, mkataba ni HGA unakuja!.
Sasa hivi ufafanuzi unatolewa mwingine na mkataba unasema mengine, sisi watanzania hatutasikiliza chochote ambacho hakipo kwenye mkataba ,yatakuwa ni matumizi mabaya ya masikio yetu.
Nakusisitizia ile IGA ni makubaliano, Mkataba ni HGA, unakuja!.
Hata chifu Mangungo wa Msovera alipewa maelezo mazuri sana
Unamaanisha nini?.
P
 
Bandari ni jambo dogo?
Yes Bandari ni jambo dogo sana compared to katiba na haki!. IGA ya Bandari na mikataba mingine yote ya kinyonyaji imetungwa kutokana na sheria mbovu ziliztungwa kutokana na katiba mbovu, hivyo mkataba mbovu ni matokeo ya katiba mbovu, sheria mbovu iliyotungwa na Bunge bovu!. Sasa badala ya kudeal na chanzo, watu mnashadadia matokeo!.
P
 
Mimi siyo lawyer lakini Ubovu wa mkataba wa Bandari hauhusiani kabisa na Udhaifu wa Katiba ni Ukosesefu tu wa Uzalendo kwa Watanganyika

Nakuhakikishia mkataba Huu ungepelekwa Baraza la Wawakilishi usingepita

Ruto kasema nchi za Africa zinaelemewa na madeni kwa sababu Viongozi wake hawawezi kusema NO Mbele ya Wawekezaji bali huchekacheka tu huku wanaumiza Wananchi wao Maskini
 
Tuna katiba mbovu inayoruhusu Bunge letu kuridhia mikataba iliyokwisha ingiwa, hivyo Bunge letu kuwa a rubber stamp. Katiba bora ingelitka Bunge kuidhinisha sio kuridhia!. Serikali ya Marekani iliwapo DPW kuendesha Bandari zake 6, Congress ikawagomea!. Kuna tofauti ya kuridhia na kuidhinisha!.
P
 
Nitajie kifungu cha Katiba kinachoruhusu Bunge kuridhia Mikataba tuliyokwishaingia

Niko pale😀
 
Hapa nchini kuna shule na vyuo vingapi vinafundisha viziwi/walemavu wa kusikia na ububu? Viziwi waliosoma na kuelimika wanaweza kupuuza lugha/ mawasiliano yao ya ishara na kusema hawajui kinachoendelea kwenye jamii inayo wazunguka??? Biblia iliposema rushwa hupofusha kumbe upofu ulikuwa ni kiwakilishi tu cha aina nyengine ya ulemavu, kumbe rushwa pia husababisha ukiziwi.
Deut 16:19.
 
Watanzania wanastahili DARWIN AWARD yaani ile zawadi ya juu kabisa anayoweza kupewa HOBO.
 
Kweli mkubwa watanzania ni watu wajinga sana pengine kuliko hata akina kondoo


Nikikumbuka yule kichaa wa Chato alivyokuwa akiwakokota kama ming'ombe huku wao wakimuita mzalendo


Eti tunajenga kwa pesa za ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…