Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?

Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?

Wanabodi
Nipashe la leo,
View attachment 2667955View attachment 2667956
Kama kawaida yangu kila Jumapili, huwaletea makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, kuzungumzia jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi kwa taifa. Mada hizi huwa zina, swali , na hoja, kisha jibu, utalitoa wewe msomaji mwenywe. Swali la leo ni kutuhusu sisi Watanzania "Watanzania ni Watu wa Ajabu?, Wanapigiaje Kelele Jambo Dogo la Mkataba wa Bandari, wakati Mambo Makubwa Muhimu na ya Msingi sana kama Katiba yao imenajisiwa, na Uhuru Wao wa kuchagua na kuchaguliwa umeporwa lakini Wako Kimya?!.

Leo naendelea na mada ya wiki iliyopita kuhusu makubaliano ya kiserikali, IGA ambapo Bunge letu limeridhia Serikali yetu kuingia mkataba wa HGA na kampuni ya DPW ya Dubai, kutuendeshea Bandari yet ya Dar es Salaam ombalo ni jambo zuri na jambo jema kwa maslahi ya taifa, lakini bado kuna kelele nyingi huku na kule, kupinga jambo hii. Baadhi ya hoja za kupinga ni hoja za msingi na zina mashiko, ambazo inabidi serikali yetu sikivu izizingatie, lakini hoja nyingine ni kelele za kijinga tuu kwa watu wajinga kwa kutokujua.

  1. Tatizo kubwa la Watanzania ni ujinga, ukosefu wa elimu!. Kwenye hili la bandari, Watanzania wanahitaji kuelimishwa tuu.Juzi kati, nimetembelea Idara ya Habari Maelezo, nimekutana na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe, kwanza nikampongeza kwa uteuzi, na kumshushia yeye zigo lote la lawama kwa hizi sintofahamu zote, zinazoendelea kuhusu hili la bandari, kwa kumweleza, limefikia hapa kwa kukosekana uwazi na elimu kwa umma kuhusu jambo hili. Nikampongeza kwa open up hadi Club House, lakini hizo Club House ziwe za proactive na sio kusubiri kelele ndipo wanakuwa reactive!. Tangu kelele za mkataba kuanza, kwanini mpaka sasa hakuna kipindi chochote cha elimu kwa umma kuhusu hili?. Msigwa alimalizia kwa taarifa ya kutia moyo sana, Maelezo inakwenda ku open up hadi kuwa na studio yake.
  2. Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanapigiaje kelele kamkataba kamoja tuu kadogo kwa rasilimali bandari, lakini kuna mambo makubwa muhimu sana ya msingi kama ubatili wa katiba, na kuporwa kwa uhuru wao, ambayo ni mambo muhimu sana!. Kwanini Watanzania wako kimya kwenye mambo makubwa ya msingi ya katiba yao kunajisiwa na uhuru wao kuporwa, halafu wanapigia kelele suala la rasilimali bandari?. Hii tasfsiri yangu, Watanzania ni watu wa kelele kwenye petty issues, lakini very serious issues, wako kimya!.
  3. Ili nisionekane na mimi ni mpinzani, namshauri Rais Samia, usiwasikilize kabisa wanaopinga ukodishwaji wa bandari kwa kampuni ya DPW ya Dubai, kwa hoja muflis, wapuuzwe!, ila wanaopinga kwa hoja za msingi, zenye masikio, wasikilizwe ili kazi nzuri ya Rais Samia iendelee!, ili HGA iwe safi na imenyooka!,
  4. Kati ya Katiba, Uhuru na Rasilimali, kipi ni muhimu zaidi?. Kitu muhimu cha kwanza kwenye nchi yoyote ni watu, uhuru wao, na katiba yao, mengine yote ikiwemo rasilimali yanafuata.
  5. Watanzania nimewaelezea kuwa ni watu wa ajabu sana kwasababu katiba yao imenajisiwa kwa kutiwa ubatili!, huku Watanzania wamenyamaza kimya!. Kwa nini haki zao mbili kuu za msingi za kuchagua na kuchaguliwa, zimeporwa na kufinyangwa finyangwa huku Watanzania wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  6. Serikali yao imetunga sheria batili kinyume cha katiba, ikazipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, Bunge, lililoshehenezwa wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, baada ya kupokea mswada huo, Bunge letu tukufu, likazipitisha sheria hizo batili kwa kuzitunga kuwa sheria!, huku Watanzania wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  7. Rais wa JMT hajawahi kuwa mwanasheria, anawategemea wasaidizi wake wabobezi na wabobevu wa sheria, kama wamezipitisha, sheria hizo batili, rais akazisaini kuwa sheria kamili licha ya ubatili wake!, huku Watanzania wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  8. Mchungaji Mtikila (RIP), akafungua shauri Mahakama Kuu kupinga sheria batili hiyo, bila support ya Watanzania wowote huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, Mahakama Kuu, ikatamka sheria hizo ni batili zifutwe toka vitabu vya sheria!. Serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ikashindwa!.
  9. Baada ya Serikali kushindwa, ikapeleka Bungeni mabadiliko haramu ya katiba ya JMT kwa kuvichomekea vipengele hivyo batili, Bunge letu Tukufu, livichomekee kiubatili ndani ya katiba yetu!. Bunge letu Tukufu likafanya mabadiliko batili ya katiba yetu ya JMT na kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu!, huku Watanzania wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  10. Mchungaji Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, kwa kuchomekewa ubatili!, hivyo akafungua shauri jingine kupinga mabadiliko hayo ya katiba kuingiza ubatili ndani ya katiba yetu!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  11. Mahakama Kuu, ikampa ushindi Mchungaji Mtikila, ikatamka mabadiliko hayo ya katiba ni batili, na yamechomekewa ndani ya katiba yetu kiubatili!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  12. Serikali yetu makini yenye wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, ikakata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu iliyotimiza wajibu wake kikamilifu kupinga katiba yetu kunajisiwa kwa kuchomekewa batili kiubatili!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  13. Mahakama ya Rufani, ikatoa uamuzi wa ajabu kabisa kwa kusema "The Court is not the custodians of the will of the people", na kulitaka Bunge lile lile lililochomekea batili ndani ya katiba yetu kiubatili ndilo liondoe batili hiyo!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  14. Mpaka leo ninapoandika hapa, batili hiyo iliyochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu bado ipo!. Ina maana tuna katiba yenye ubatili ndani yake!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  15. Mpaka leo ninapoandika hapa, bado tuna sheria batili ndani ya sheria zetu, zinazopora uhuru wa Watanzania kuchagua na kuchaguliwa, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia!, hawa sio watu wa ajabu?!Iweje leo, Bunge hili hili lililopitisha ubatili ule wa ajabu kabisa, kwanza kwa kutunga sheria batili, na hata baada ya mahahama kutamka vipengele hivyo ni batili, bado Bunge lilivichomekea kiubatili, vipengele hivyo batili ndani ya katiba yetu likanyamaziwa!, lakini lilipopitisha kijimkataba kidogo tuu cha rasilimali Bandari kwa kampuni ya DPW ya Dubai, watu wanapiga kelele mpaka karibu zifike mbinguni?, hawa Watanzania wanaopigia kelele, haka kamkataba, hawa sio watu wa ajabu?!

Hitimisho
Unanyamaziaje katiba yako inanajisiwa, uhuru wako unaporwa, halafu unapigia kelele jambo la kheri kama uendeshaji wa Bandari?!, huu sio uthibitisho kuwa sisi Watanzani ni watu wa ajabu sana?, kwanini wanashadadia sana kulipinga jambo la kheri, kusaidiwa kuendesha bandari yetu kwa ufanisi baada ya sisi kushindwa, halafu jambo kubwa na la msingi sana kama katiba yako imenajisiwa, uhuru wako muhimu kabisa wa kuchagua na kuchaguliwwa umeporwa!, kwanini tunanyamaza?!, sisi sio watu wa ajabu sana?

Wasalaam

Pasikali
Rejea za mwandishi kuhusu sakata la Bandari
  1. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
  2. Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!
  3. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
  4. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
  5. Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
  6. DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
  7. Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?
Mabandiko ya Mwandishi Kupigia Kelele Mambo Makubwa Muhimu ya Msingi, ya Uhuru, Katiba, Sheria na Haki
  1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  3. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  4. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  5. Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
  6. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
Update teuzi upumzike
 
Sasa kama huwezi kuitetea Bandari ndio utaweza kutengeneza Katiba?

Bure kabisa!
Katiba hii ya rais kuteua kila nafasi ya uongozi, kutokupingwa matokeo ya uchaguzi mahakamani, sifa ya ubunge kujua kusoma na kuandika tu. Aisee issue ya bandari ni ndogo sana ukilinganisha na madudu yaliyopo kwenye katiba ya mkoloni.

Bandari ijadiliwe lakini katiba mpya iwe first priority.
 
Kuwaambia uongo wengine ni hatari kama kuwapiga kwa shoka, kuwajeruhi kwa upanga, au kuwapiga risasi au kuwachoma kwa mshale mkali.

Proverbs 25:18

Kile ambacho tumeambiwa katika siku za hivi karibuni kinaweza kuitwa uongo

.....
Mfano mzuri ni Nini / ilikuwa inajadiliwa, inadhaniwa, ni MOU au kama inajulikana sasa IGA na tukaja/ tulitaarifiwa , IGA haina nguvu kwa nguvu zake ila kwenye HGA zifuatayo tunauwezo wa kurakabisha mazito ya IGA na kwa hivyo tuliuaswa kupuuza umuhimu na au athari inayoweza kutokea kupunguza nguvu za uhuru wetu(sovereign powers)?. Kwa kusikitisha, kinyume chake ilikuwa ukweli, kwamba, MOU au IGA huathiri kwa kiasi kikubwa uhuru(sovereign)wetu hadi kufikia hatua ya kupunguza nguvu ya sheria yetu mama, Katiba... humo.utaona shoka upanga na risasi zimepigwa[kwa kukosa tafsiri] kwa saiiki(pysche)ya Taifa letu! Ni aibu kwa taifa letu.

Nini kilichofanyika? Binafsi najiuliza ni Kwanini Wananchi wamefikia hapa na ninajifariji na majibu yangu mwenyewe kwa kuongeza na za Wanafalsafa.
Mosi,
"Ni ukweli unaojulikana wa kisaikolojia kwamba maono yetu ya iwezekanavyo(possibilities) yanaundwa na kile tunachofikiria(imaginations) au kuona(vision) uwezo(capacity) kuwa.

Ukubwa wa mawazo yetu au mtazamo(perception)wetu wa uwezo(capacity) wetu, itakuwa maono(vision) yetu ya iwezekanavyo(possibilities). Kinyume chake, mawazo yetu madogo au mtazamo wa uwezo wetu, itakuwa ni kuyashusha maono yetu ya iwezekanavyo.

Kwa ndoto yoyote au maono ya kuwa na watu au taifa, maono yake ya uwezekano na mawazo yake au mtazamo wa uwezo wake lazima yawe na uhusiano mzuri. [Coordinated and correlated Vision] Kama watu au maono/dira ya taifa ya iwezekanavyo/yawezekanayo na mawazo yake au mtazamo wa uwezo wake ni hasi, basi ni sawa na kujiachia kupigwa shoka, upanga, risasi na mshale kwenye eneo moja... Uchungu wake ndio hizi wanasiasa wanazoziita "kelele" manake ni machungu yanayoelezeka kwa aina yake ya kipekee. Ni mayowe haswa.

Pili,tuliyokuwa tumeanza kuyaamini, kuwa yanayowezekana,tuliyoyafikiria na tukaanza kuyaona tukayaona, yalipigwa vita sana , kuwa yote hayakuwa, kwamba mafanikio tuliyoyapata hayakuwa mafanikio!
Hilo nalo lilikuwa na kama Jeruhi lingine tu la shoka, upanga risasi na mshale, tena kwenye kidonda kilekile chan kwanza walichopata mababu zetu!
Mashallah!
Sasa basi, kwa haya yanayoendelea ni sawa na kusema, Taifa letu limekosa dira, kuwa our imagination, our capacity of the possible zimeyayuka ghafla. Hii ndio Tanzania nionavyo leo hii. Hakuna Mtanzania wa ajabu....Ajabu ni our Imagination, our perception and our perceived capacity has been trampled, historically by the people whom we have resented. Watu waliowatesa mababu zetu, haijalishi....Mzungu, Mwarabau, au beberu wa aina yeyote ile. Itoshe kusema, maamuzi na mwelekeo Serikali ya SsH inapotupeleka ni sawa na kutugeuzia upande wa jeraha kuunyukwa tena kwa shoka , upanga, risasi na nchale! Hiyo ndio ajabu!
Tumepata ulazima gani ghafla hata kujishusha namna hii?

Lazima turudi mezani.
We need to perpetuate a self reliant Dynamism
Tunahitaji kujenga uwezo wa kujitegemea. Bila ya kuwakumbatia wanyonyaji!

Nimalizie na mstari mfupi,...
Njia yako ilipita baharini, na njia yako kupitia maji makuu, ni njia ambayo hakuna mtu aliyejua ilikuwa huko~
Zaburi 77:19


Kumbuka katika hali zote wakati giza imetamalaki na matumaini yote yamepotea, Mwenye nguvu anaongoza

Aluta Continua.
 
Mkataba ungekuwa unasema hivyo kama anavyosema waziri mkuu Kassim Majaliwa tusingelalamika.
Ile ni IGA, sio mkataba, mkataba ni HGA unakuja!.
Sasa hivi ufafanuzi unatolewa mwingine na mkataba unasema mengine, sisi watanzania hatutasikiliza chochote ambacho hakipo kwenye mkataba ,yatakuwa ni matumizi mabaya ya masikio yetu.
Nakusisitizia ile IGA ni makubaliano, Mkataba ni HGA, unakuja!.
Hata chifu Mangungo wa Msovera alipewa maelezo mazuri sana
Unamaanisha nini?.
P
 
Bandari ni jambo dogo?
Yes Bandari ni jambo dogo sana compared to katiba na haki!. IGA ya Bandari na mikataba mingine yote ya kinyonyaji imetungwa kutokana na sheria mbovu ziliztungwa kutokana na katiba mbovu, hivyo mkataba mbovu ni matokeo ya katiba mbovu, sheria mbovu iliyotungwa na Bunge bovu!. Sasa badala ya kudeal na chanzo, watu mnashadadia matokeo!.
P
 
Yes Bandari ni jambo dogo sana compared to katiba na haki!. IGA ya Bandari na mikataba mingine yote ya kinyonyaji imetungwa kutokana na sheria mbovu ziliztungwa kutokana na katiba mbovu, hivyo mkataba mbovu ni matokeo ya katiba mbovu, sheria mbovu iliyotungwa na Bunge bovu!. Sasa badala ya kudeal na chanzo, watu mnashadadia matokeo!.
P
Mimi siyo lawyer lakini Ubovu wa mkataba wa Bandari hauhusiani kabisa na Udhaifu wa Katiba ni Ukosesefu tu wa Uzalendo kwa Watanganyika

Nakuhakikishia mkataba Huu ungepelekwa Baraza la Wawakilishi usingepita

Ruto kasema nchi za Africa zinaelemewa na madeni kwa sababu Viongozi wake hawawezi kusema NO Mbele ya Wawekezaji bali huchekacheka tu huku wanaumiza Wananchi wao Maskini
 
Mimi siyo lawyer lakini Ubovu wa mkataba wa Bandari hauhusiani kabisa na Udhaifu wa Katiba ni Ukosesefu tu wa Uzalendo kwa Watanganyika

Nakuhakikishia mkataba Huu ungepelekwa Baraza la Wawakilishi usingepita

Ruto kasema nchi za Africa zinaelemewa na madeni kwa sababu Viongozi wake hawawezi kusema NO Mbele ya Wawekezaji bali huchekacheka tu huku wanaumiza Wananchi wao Maskini
Tuna katiba mbovu inayoruhusu Bunge letu kuridhia mikataba iliyokwisha ingiwa, hivyo Bunge letu kuwa a rubber stamp. Katiba bora ingelitka Bunge kuidhinisha sio kuridhia!. Serikali ya Marekani iliwapo DPW kuendesha Bandari zake 6, Congress ikawagomea!. Kuna tofauti ya kuridhia na kuidhinisha!.
P
 
Tuna katiba mbovu inayoruhusu Bunge letu kuridhia mikataba iliyokwisha ingiwa, hivyo Bunge letu kuwa a rubber stamp. Katiba bora ingelitka Bunge kuidhinisha sio kuridhia!. Serikali ya Marekani iliwapo DPW kuendesha Bandari zake 6, Congress ikawagomea!. Kuna tofauti ya kuridhia na kuidhinisha!.
P
Nitajie kifungu cha Katiba kinachoruhusu Bunge kuridhia Mikataba tuliyokwishaingia

Niko pale😀
 
Hapa nchini kuna shule na vyuo vingapi vinafundisha viziwi/walemavu wa kusikia na ububu? Viziwi waliosoma na kuelimika wanaweza kupuuza lugha/ mawasiliano yao ya ishara na kusema hawajui kinachoendelea kwenye jamii inayo wazunguka??? Biblia iliposema rushwa hupofusha kumbe upofu ulikuwa ni kiwakilishi tu cha aina nyengine ya ulemavu, kumbe rushwa pia husababisha ukiziwi.
Deut 16:19.
 
Watanzania wanastahili DARWIN AWARD yaani ile zawadi ya juu kabisa anayoweza kupewa HOBO.
 
Kweli mkubwa watanzania ni watu wajinga sana pengine kuliko hata akina kondoo


Nikikumbuka yule kichaa wa Chato alivyokuwa akiwakokota kama ming'ombe huku wao wakimuita mzalendo


Eti tunajenga kwa pesa za ndani
 
Back
Top Bottom