Watanzania ni Watu wanaopenda habari za Uzushi, Conspiracy theories na udaku

Watanzania ni Watu wanaopenda habari za Uzushi, Conspiracy theories na udaku

Interview ya CDF sio ya bahati mbaya. Ni ishara kuwa ukweli utakuwa wazi, utakuja vipande vipande ila naamini mwisho wa siku ABCs zote za kifo cha jiwe na zile siku 3 kabla ya kuapishwa SSH zitakuwa wazi.

Jana lakini ni kumbukumbu ya kifo cha Jpm hivyo maelezo kama hayo ni kawaida kwa siku kama ya jana
 
siyo watanzania ni miongozo ya kiulimwengu katika kustawisha dola uongo huwa ni mwingi kuliko ukweli na kwa bahati mbaya akili inapenda mambo yaloyopita au yajayo kwani huwa hayana mashiko kwa muda huo.

ukweli una athari kubwa watu tusingesalimiana na tungerudi kwenye pre social contract era.
 
Dotto magari anasemaje 😄

Mange kimambi akisema amesema hakosei mange aisee
Ana data za ndani na za ukweli 😄
Ehe kigogo naye vp anasemaje naye mimi ndy namuaminia kigogo bana 😄

Ova

Huwezi washughulikia Watu kama kina Kigogo na Mange Wakati huna chakula cha kuwapa Watu wapenda Udaku.

Udaku unasaidia pia kuwa-keep busy Watu wasio na kazi ili wasiwaze mambo ya msingi kama katiba na nchi yao
 
siyo watanzania ni miongozo ya kiulimwengu katika kustawisha dola uongo huwa ni mwingi kuliko ukweli na kwa bahati mbaya akili inapenda mambo yaloyopita au yajayo kwani huwa hayana mashiko kwa muda huo.

ukweli una athari kubwa watu tusingesalimiana na tungerudi kwenye pre social contract era.

Kikawaida Ukweli hauna faida kwa sababu mara nyingi ni out of our expectations
 
Kwema Wakuu!

Jadili Chozi la CDF Mstaafu Mabeyo litolee ufafanuzi kana kwamba unajua alichokuwa anafikiri. Fafanua na elezea tabasamu na kila cheki lake na maana iliyojificha. Kwa kina onyesha jinsi body language yake inavyokinzana na anachozungumzia, hakikisha unaeleza uongo mtamumtamu unaopatana na akili za Watanzania kuhusu habari zilizofichwa ambazo watanzania wengi hata kabla hawajaambiwa huwa na hizo habari akilini.

Watanzania wanapenda assumption, imagination, fiction stories, ndio maana ukiwa mbobevu kwenye hayo mambo kwa hapa Tanzania lazima utoboe. Wachungaji wa kileo wengi washasoma saikolojia ya Watanzania, wanasiasa, waganga, biashara ya michezo ya kubahatisha itazidi kustawi na kushamiri kutokana fikra za Watanzania.

Ukishakuwa Star Tanzania ni rahisi kuwaendesha Watanzania vile unavyotaka. Unaweza ukawapa cha kuzungumza wakakizungumza mwezi mzima.

Mange Kimambi, Kigogo kigogo, ni miongoni mwa Watu walioweza kutumia fikra za Watanzania.

Tanzania unaweza ukavaa tuu nguo yenye fuvu la kichwa au pete yenye fuvu la kichwa na ukishakuwa na pesa ya kubadilisha mboga utatungiwa stori za uzushi mara wewe Freemasonry mara sijui kitu gani. Watanzania hawapendi Ukweli. Na ukiwa umesimama mbele ya mtu unayemjua ni Mtanzania hata kama una ukweli wa jambo usimwambie kwa sababu hatakuamini. Mtanzania ni rahisi kuamini uzushi na udaku kuliko kuamini UKWELI.

Hata hivyo haishangazi kwa sababu ukweli mara nyingi(sio zote) Hauna Faida, na Pia ukweli kikawaida unakatili sana. Ukweli ni uhalisia. Na mwanadamu hasa Mtanzania hapendi Uhalisia (ukweli).

Mimi nimemaliza.
Akili kubwa zinaongelea maendeleo.

Akili za kawaida zinaongelea matukio.

Akili mbovu zinaongelea watu.
 
Dunia nzima wanapenda habari kama hizo siyo bongo peke yake sababu duniani watu wajinga ni wengi kuliko werevu

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Binafsi nafikiri kuhoji hoji na kudadisi ni kitu kizuri, ila matumizi ya huu udadisi labda ndiyo siyo chanya.

Ukipata habari/taarifa baada ya kuchunguza unazifanyia nini, ndipo ilipo shida.

Ukitumia vizuri ndiyo tunapata vitu vinaitwa ujasusi/ ushushushu/ upelelezi. Majasusi wazuri ni watu wanaofuatilia kila detail including even eye gestures.
Kila detail kwenye upelelezi ina maana, hupaswi kupuuzia hata kikohozi na chafya.

Kukaa kindezi na kumeza kila jambo kama linavyoonekana ndiyo kinyume cha werevu, ni kutokujali, kutokutaka kiwajibika.
 
Kwa hiyo hutaki watanzania watumie bongo zao kufikiri, unataka wawe wazembe tu wanaosubiri kuletewa kila taarifa kama ilivyo?
Hahaaha haloo una kitu utafika mbali,Wabongo sie tuchoree picha tu caption kila mtu ataweka yake!
 
Nakumbuka ile mada yako ukijaribu kueleza namna mzee alivyo ondoka. Na ulisema kifua sijui kilibana akashindwa kupumua vizuri akaanguka n.k unaikumbuka? Wengine bado tunaikumbuka
 
Back
Top Bottom