WaTanzania ni watu waoga na waporojo sana

WaTanzania ni watu waoga na waporojo sana

Kusini pride

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,762
Reaction score
4,079
…naona wote mpo busy na msiba wa Papa, lakini hamjui kinachoendelea Tunisia 🇹🇳…

Tunisia 🇹🇳 kuna Rais mwendawazimu anayeitwa Kaïs Saïd, Dikteta zaidi ya Kambare…

Huyu jamaa anamiliki serikali, Bunge na Mahakama zote nchini humo…

Juzi, kawahukumu viongozi wa upinzani, mawakili wao, wanaharakati, waandishi wa habari na wafuasi mbali mbali wa vyama vya upinzani, wote wamekula miaka 30 hadi 40 jela…

Leo wananchi wameamua kusimama, kama taifa, lengo ni kumng’oa huyo mwendawazimu…

Itakumbukwa ya kwamba, lile vuguvugu la “Arab Spring”, mwishoni mwa mwaka 2010, lilianzia hapo hapo Tunisia 🇹🇳…

Vuguvugu hilo, ambalo lilianzishwa na wananchi wenyewe bila msaada wa nchi yoyote ya kigeni, lilifanikiwa kumng’oa madarakani Rais Zine El Abidine Ben Ali, hapo Tunisia 🇹🇳…

Vuguvugu hilo likahamia Morocco 🇲🇦, hakuna kiongozi aliyeng’olewa lakini Katiba ilibadilishwa…

Baadae vuguvugu likahamia Libya 🇱🇾 likamng’oa Dikteta Gaddafi, na mwisho kabisa likafika Misri 🇪🇬, likamfyeka yule mfia dini Mohamed Morsi…

Hawa wananchi wa haya mataifa ya Kiarabu ni tofauti sana na yale makima ya Kusini mwa janga la Sahara… Hawa watu wakiamua lao, hakuna kinachoshindikana…

Yale makima ya Kusini mwa janga la Sahara especially Watanzania, wakiona matukio kama haya, moja kwa moja wanadai eti “kuna mkono wa Mataifa ya Magharibi”… 😁🤷🏾‍♂️

Guys, uthubutu ambao nyie hamna, tambueni ya kwamba Waafrika wengine wenye ujasiri, wanao uthubutu huo!…

Hakuna mijitu mioga hapo Afrika kama Watanzania, hasa Watanganyika!… Kelele zao huishia mitandaoni, mara sijui “Free Lissu, Free Heche, no rifomzi no ereksheni bla bla blaaa”! Nyie ni kunguru tu!…

Watanzania mnazidiwa uthubutu hata na Warundi…

Mwaka 2015 Dunia nzima ilishuhudia wananchi wa Burundi 🇧🇮 wakiandamana kupinga muhula wa 3 wa yule Dikteta Nkurunzinza!… Walipigwa risasi, waliuawa lakini walisimama kama nchi, kuupigania mustakabali wa taifa lao, jambo ambalo kunguru wa Tanzania 🇹🇿 hawawezi!…

Mwisho kabisa, nasubiri kunguru wa Tanzania 🇹🇿 mniambie nchi gani ya Magharibi ipo nyuma ya haya maandamano yaliyoanza Tunisia 🇹🇳…

Hamchelewi kuitaja Ufaransa 🇫🇷 😁🤷🏾‍♂️
 
Yaani unaandika halafu unataka wengine wajitokeze kama watunisia ikiwa wewe umejifungia ndani.
 
Back
Top Bottom