Ni mazuri ila ya kawaida sana. Mimi nimezaliwa na kukulia hapa Dar. Nimekaa Sweden 10 consecutive yrs, na sikuwahi kuona kiongozi akitaka kusujudiwa kwa kutimiza wajibu wake. Wala sijawahi kuona huko kiongozi akinajisi chaguzi za nchi hiyo ili chama chake kitangazwe washindi, kisa kuna mambo fulani katekeleza kwenye wajibu wake. Hizo tabia ziko kwenye nchi zenye mitazamo ya kikomunisti, kama China, North Korea nk, ambapo wananchi wanatawaliwa kwa mabavu na shuruti, na kuishi kwa kutii utashi wa viongozi, na viongozi hujiona ndio wenye maono ya nchi.
Hiyo treni inayokutisha ww leo, mimi nimetumia zaidi ya miaka kumi, na wala sikushangaa chochote. Mnaweza kuwatisha malimbukeni wenzenu. Sio kila mtu anasujudia vitu mpaka viwe kigezo cha kunyanyasa wenye mitazamo tofauti na mitazamo/itakadi zenu za kichovu.