---------Eti uzalendo!!!
Uzalendo ni itikadi ya kuweka maslahi ya taifa lako mbele ili liweze kufanikiwa kwa kila namna. Lakini inatia aibu sana CHADEMA na wanachama wake pamoja na wafuasi wake hawana uzalendo kabisa na hawalitakii mema taifa letu.
====Ukiweza kuweka tafsiri ya taifa! nitakujibu vizuri. Je ikiwa taifa linaongozwa na vibaka na wauaji utawaweka mbele wao na taifa? Kitendo cha kuwatenga mbali na taifa na kuwapiga ni uzalendo tosha. Yaani ukiwapiga vita vibaka na wauaji wanaoharibu taifa wakiwa viongozi huo ndio UZALENDO.
Kwa mwananchi mzalendo ambae unalitakia mema taifa lako huwezi kubeza mambo ambayo CCM imelifanyia taifa hili tangu tunapata uhuru mpaka sasa. Serikali ya CCM inaimarisha sekta ya afya kwa kujenga vituo vya afya na hospital, mnasema eti ni maendeleo ya vitu. Kwani hawatakuja kutibiwa watu?
== haitoi chochote bure. CCM inatumia kodi zetu kufanya hayo. Tatizo linakuja pale vipaumbele vya wananchi vinatupwa mtu mmoja anatumia uongozi wake anampa madaraka mpwa wake ya katibu mkuu hazina na kuchota mabilioni kama ya kwenye wallet yao kujenga uwanja wa ndege nyumbani kwao. Kununua madege wakati wafanyakazi wa serikali wako dhoofu bin taabani kwa mateso ya kukosa mafao na stahili zao. Hao ni viongozi na sio taifa. Tutawatenga kuwapinga na kuwaondolea mbalimbali na huo ndio uzalendo
Serikali ya CCM inajenga mradi wa JNHPP ili taifa lipate umeme mwingi na wa uhakika. Mnasema eti ni Mega structures na hazina manufaa kwa watu. Kwani huo umeme nyie wanaChadema hamtautumia? Tena kwa bei rahisi! Mradi wa Sgr mnasema ni maendeleo ya vitu sio watu. Kwa hiyo hiyo treni hamtaipanda? Hamtasafirishia mizigo yenu?
====Tena na tena tenganisha uzalendo kwa taifa na uzalendo kwa chama na viongozi madikteta wasiosikia la mtu. Ni wapi bunge lipi lilipitisha hiyo miradi na lini?
Yaani wewe kwa sababu tumekupa uongozi uamke kitandani kwa mkeo uchukue kodi zetu uweke kwenye mamiradi ambayo wawakilishi wetu hawajapanga kwa niaba yetu?
Uzalendo mavi huo.
Kwa ujumla watanzania wameshawajua ninyi ni wapiga dili na chama chenu kipo kimaslahi binafsi. Sio kuwaletea watanzania maendeleo kwa maslahi mapana ya taifa letu.
====Wee mpiga debe mtumwa ndiye unayeongozwa kama ngombe wa machinjioni ndiye unayebwabwaja. Hebu acheni upenyo wa uhuru wa kidemokrasia kama hamtaambulia mashimo ya choo cha stendi
Natoa ushauri tu Oktoba msijaribu kugombea nafasi yoyote maana watanzania hawawataki tena.
Siasa sio chuki na uadui.
====Hayo nenda kawaulize walimkatakata aloys mawazo, waliomteka Ben saanane, walioua diwani wa hananasifu, waliompiga lisu risasi 40. Kamuulize magufuli na genge lake.