Uchaguzi 2020 Watanzania sio wajinga, hawatachagua chama ambacho wafuasi, viongozi na wanachama wake sio wazalendo

Hakuna mtu anayetaka kiongozi asujududiwe. Bali tunaeleza mambo mazuri aliyofanya. Ambayo hata wewe unasema yalicheleweshwa. Hakuna ulimbukeni hapo, hivi punde utakuwa unakula treni mpaka Dodoma, fasta tu.
 
Je kwa rasilimali tulizonazo tunastahili kua na maisha haya leo?yanayofanywa na chama tawala ni "wema" ama ni wajibu wao?
Wewe unaonaje? Maana hata Mobutu alikuwa na wajibu wa kuindeleza DRC yenye utajiri wa kutosha wa maliasili. Lakini alihamisha pesa za umma na kupeleka Uswiss.
 
Hakuna mtu anayetaka kiongozi asujududiwe. Bali tunaeleza mambo mazuri aliyofanya. Ambayo hata wewe unasema yalicheleweshwa. Hakuna ulimbukeni hapo, hivi punde utakuwa unakula treni mpaka Dodoma, fasta tu.

Ni mazuri ila ya kawaida sana. Mimi nimezaliwa na kukulia hapa Dar. Nimekaa Sweden 10 consecutive yrs, na sikuwahi kuona kiongozi akitaka kusujudiwa kwa kutimiza wajibu wake. Wala sijawahi kuona huko kiongozi akinajisi chaguzi za nchi hiyo ili chama chake kitangazwe washindi, kisa kuna mambo fulani katekeleza kwenye wajibu wake. Hizo tabia ziko kwenye nchi zenye mitazamo ya kikomunisti, kama China, North Korea nk, ambapo wananchi wanatawaliwa kwa mabavu na shuruti, na kuishi kwa kutii utashi wa viongozi, na viongozi hujiona ndio wenye maono ya nchi.

Hiyo treni inayokutisha ww leo, mimi nimetumia zaidi ya miaka kumi, na wala sikushangaa chochote. Mnaweza kuwatisha malimbukeni wenzenu. Sio kila mtu anasujudia vitu mpaka viwe kigezo cha kunyanyasa wenye mitazamo tofauti na mitazamo/itakadi zenu za kichovu.
 
Sweden nchi ambayo kodi yake inatumika inavyotakiwa. Watu wasiseme kweli kuwa serikali inatimiza wajibu vizuri? Maana Sweden mtu akikosa hata dawa ni kashfa kubwa. Kwa hiyo kutimiza wajibu ipasavyo lazima watu wajadili ukweli.
 
Unakosea sana kusema viongozi wanasujudiwa. Hata Usa Trump amekalia kuti kavu. Lakini Obama alifanya mazuri kama Obamacare na watu walimsifia.
Na usifananishe Sweden na Tanzaniam
 
Sina tatizo na kodi kutumika kufanya baadhi ya mambo, maana hayo ndio matumizi ya kodi, na hayo hata wakoloni walifanya. Ila nisichounga mkono ni uonevu, kuchafua demokrasia ya nchi, na kulazimisha watu wote kutawaliwa kwa shuruti kwa mitazamo ya rais, kisa kajenga hospitali, barabara, reli nk. Sio kila mtu anaamini itakadi ya rais na chama chake, yeye atekeleze wajibu wake, na atuache tuishi kwa mitazamo yetu, na tumchague tumtakaye, na sio amtakaye yeye.
 
Unakosea sana kusema viongozi wanasujudiwa. Hata Usa Trump amekalia kuti kavu. Lakini Obama alifanya mazuri kama Obamacare na watu walimsifia.
Na usifananishe Sweden na Tanzaniam

Sikosei chochote maana kila kitu kiko wazi, kuna shuruti ya wazi na ya kificho kuwa kiongozi huyu asujudiwe. Ndio maana taasisi zote za kimamlaka zinaweza kumuonea yoyote asiye upande wa rais, na kutia wananchi hofu ili watawaliwe kwa lazima bila ridhaa yao. Chaguzi zetu zinajieleza wazi, uhuru wa vyombo vya habari uko hoi, labda uwe kundi la kusifia ndio salama yako.

Watu walimsifia Obama kwa ridhaa yao na sio kwa shuruti. Hapa ni kinyume chake.
 
Hapa Tanzania nani anasurutishwa kusema ukweli? Ni aibu watu kutokuitakia mema nchi yenu.
 
Uzalendo wa kizuzu tena nyinyi ni wasakatonge tu wabunge wenu hawasomi miswaada wala kuchambua niwabunge wa ndio Mzee kina Steve Nyerere, Mc pilipili mmefanya mpaka watu wameushusha hadhi ubunge kila mtu anataka kuwa mmbunge nonsense
 
Serekali sio nchi, usitake kuchanganya haya mambo mawili.
[/QUOTE
Sijachanganya,serikali ya Ccm inaongoza taifa letu . Nchi yetu ipo mikononi mwa serikali ya Ccm. Ukiombea mabaya Ccm ni sawa na kuliombea mabaya taifa letu.
 
Ccm hawako madarakani kwa ridhaa ya wananchi, bali wako kupitia chaguzi za kishenzi na kihayawani. Ndio maana tunataka tume huru, ili anayekaa madarakani awe na ridhaa ya walio wengi kihalali.
 
Ccm hawako madarakani kwa ridhaa ya wananchi, bali wako kupitia chaguzi za kishenzi na kihayawani. Ndio maana tunataka tume huru, ili anayekaa madarakani awe na ridhaa ya walio wengi kihalali.
Mh... Kwa hiyo 2015 haukufanyika uchaguzi?
 
Kufanyika hakumaanishi tume ni huru.
Huo uhuru unataka uwe vipi? Maana hata sasa tume ni chombo huru kinachofanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria. We unataka uhuru wa namna gani? Fafanua.
 
Kwa hiyo ukiwa ccm ndo umekua mzalendo?
Siku nyingine usicomment Kama pombe haijaisha kichwani.
 
Huo uhuru unataka uwe vipi? Maana hata sasa tume ni chombo huru kinachofanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria. We unataka uhuru wa namna gani? Fafanua.

Mimi sio mtoto boss, tume iliyo huru, na tume inayoshiriki ushenzi wa kunajisi uchaguzi naweza kuzitenganisha vizuri sana. Tume hii ni sehemu ya ushenzi wa wazi unaoendelea kwenye chaguzi zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…