Watanzania tuamke, Bunge la chama kimoja limezaa tozo

Watanzania tuamke, Bunge la chama kimoja limezaa tozo

Ukweli ni kwamba tulikuwa hakuna kitu kinatuleta pamoja kama nchi ndo maana hata maandamano yalikuwa haiwezekani.sasa wametuunganisha
 
Watanzania muda tulio nao kwa sasa na matatizo tunayo pambana nayo liwe fundisho.

Mwaka 2020 October tukubali kuwa tulichezewa sana na tukakubali na matokeo yake ndiyo haya sasa.

Bunge lililopatikana ni matokeo ya sisi kukubali kudanganywa kwa maneno mazuri lakini sasa tunaonja shubiri.

Hakuna waziri anayejali wala kusikiliza kilio cha tozo gandamizi za miamala na sasa tozo za majengo kupitia huduma za umeme.

Hatuna mwakilishi pale bungeni tukubali kuwa wote waliopo pale ni wana CCM tu na wapo pale kutetea maamuzi yoyote ya kutoka CCM.

View attachment 1901401
Limezaa wizi mkuu,Wala sio tozo tena
 
Ukweli ni kwamba tulikuwa hakuna kitu kinatuleta pamoja kama nchi ndo maana hata maandamano yalikuwa haiwezekani.sasa wametuunganisha
Hata wale watu wa iraq na Afghanistan hawakuzaliwa na chuki kama ile ila ni kutoka kwa watawala
 
Yaani Serikali ya huyu mama wa viti maalum imeamua kutupora hela Watanzania, mfano kodi ya majengo ya mwaka wa fedha 2021/22 tulikwishalipa kabla ya July mosi 2021 lakini leo tunaambiwa tulipie kodi ya mwaka mwingine upya, huu si ni wizi na uporaji? Wanasheria hebu litazameni suala hili kwa jicho pana zaidi ili mfungue kesi Mahakamani kupinga unyanganyi huu wa Serikali. Wameshindwa kubuni vyanzo stahiki vya mapato wameamua kutupora kwa nguvu pesa zetu kupitia Huduma ambazo hatuwezi kuzikwepa
Mwigulu hana huruma kabisa kwa watanzania
 
Sisi Watanzania tutazoea tu...ndio hulka yetu
 
Hakuna mtu yeyote yule anaye zoea mateso

Sasa mtanzania ndio huyo mtu aliyekwishazoea mateso...

Kitendo tu cha kuwapa madaraka CCM kila mara, wakati huo huo kuwalalamikia kila mara ni dalili kuwa watanzania wamezoea shida zao
 
Mwenda zake katuachia msala mzito kweli kweli
JamiiForums1005392681.jpg
 
Sasa mtanzania ndio huyo mtu aliyekwishazoea mateso...

Kitendo tu cha kuwapa madaraka CCM kila mara, wakati huo huo kuwalalamikia kila mara ni dalili kuwa watanzania wamezoea shida zao
Naunga mkono hoja yako kwa 100%
 
Back
Top Bottom