Watanzania tuamke na tuache kuwakabidhi haki zetu wanasiasa

Watanzania tuamke na tuache kuwakabidhi haki zetu wanasiasa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Bado Tanzania ni nchi salama sana kuishi. Kwanini? Watu wake ni wapole na waliomtanguliza Mungu. Hata kwenye haki zetu huwa "Tunamwachia Mungu" na kuendelea na maisha kama kawaida tena kwa furaha. Tumeongezewa kodi ya ovyo inayoitwa kodi ya uzalendo/mshikamano lakini tuko fresh tu na kuanza kutengeneza Memes za kujifurahisha. 🤣 inashangaza.

Leo tarehe 15/07/2021 ni siku ambayo nchi yetu imeweka alama kwenye maisha ya kila mwananchi bila kujali umri, cheo, itikadi, dini, maskini, tajiri wala yeyote yule. Leo ndo siku ambayo watanzania tumebebeshwa mzigo mzito usiobebeka wenye nembo ya uzalendo/mshikamano. Tozo kwenye gharama za miamala ya Electronic money (m-pesa, tigopesa, airtelmoney nk) kwa zaidi ya 100% ya gharama zilizokuwepo ni mzigo mzito usiobebeka.

Wengi wameilaumu CCM huku wakisahau pia CHADEMA kupitia katibu mkuu wake walisema kwamba wangeridhia uwepo wa kodi ya katiba mpya kwenye hii miamala. Kimsingi wanasiasa wote bila kujali vyama wako kwa maslahi yao binafsi. Siku tukiamka huu usingizi na kuacha mambo ya vyama hatutachezewa kabisa.
 
FAO LA KUJITOA NSSF lirejeshwe

Wafanyakazi wapo na malalamiko

Bado hamjatosheka, mmeleta tozo za simu, vocha, miamala na mafuta
 
Bora tuajiri watu toka nje wa kutuongoza kuliko hawa wanasiasa.Rais tuajiri toka Israel au USA,waziri mkuu toka india, mawaziri toka nje ajira ya miaka 5 mitano,ndio watakaoweza kutuvusha na sio hawa wanasiasa.

Mtu mweusi hawezi ongoza jamii 60 yrs wameproof failure.
 
Bora tuajiri watu toka nje wa kutuongoza kuliko hawa wanasiasa.Rais tuajiri toka Israel au USA,waziri mkuu toka india, mawaziri toka nje ajira ya miaka 5 mitano,ndio watakaoweza kutuvusha na sio hawa wanasiasa.
Inaweza kuonekana kama utani, LAKINI nina hakika kama kungekuwa na uwezekano wa kupata watu kutoka nje ya Tanzania, waje waongoze Serikali, maendeleo ambayo yangeonekana yangemshangaza kila mtu.

Tatizo kubwa la nchi ni kukosa viongozi wazuri na wenye uwezo.
 
Bora tuajiri watu toka nje wa kutuongoza kuliko hawa wanasiasa.Rais tuajiri toka Israel au USA,waziri mkuu toka india, mawaziri toka nje ajira ya miaka 5 mitano,ndio watakaoweza kutuvusha na sio hawa wanasiasa.
Unahisi umeongea utani...kumbe ni bonge moja la point
 
Mtoa post nenda kwa Mangi kanywe soda nitalipa.

Uliloandika ndio chanjo kikubwa cha matatizo yasiyoisha ya nchi hii mpaka miaka yote ,kizazi kimoja kwenda kingine
 
Back
Top Bottom