Watanzania tuamueni lililosahihi hapa tafadhali

Watanzania tuamueni lililosahihi hapa tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,685
Reaction score
128,178
Je, tung'ang'anie Katiba Mpya huku Uchumi wetu Ukidorora au tuimarishe na tukuze Kwanza Uchumi wetu na Katiba Mpya tuwaachie Vizazi vijavyo?

Leo nitakuwa ninasoma tu Maoni yenu.
 
Uchumi gani unaongelea Macro au Micro?

Kama ni Micro economics tayari watu wana maisha màgumu tangu uhuru na wamerithisha watoto wao Umaskini mpaka mwaka huu 2021

Kama ni Macro economics nchi yetu inategemea msaada wa mabeberu toka tupate uhuru kuanzia vifaa tiba mpaka tekinolojia

Mabeberu mbona walitoa misaada hata kama Mwendazake aliwatukana

Kuna uhusiano gani kati ya katiba na uchumi

Katiba ni mfumo mzima wa nchi kuendesha maisha kwa uhuru na haki na kwa kushirikisha jamii nzima

Katiba ni maoni ya wananchi wanahitaji maisha na mifumo iendeshwe na nani na kwa wakati gani? Na ni hatua gani za kuchukua pale mambo yanapoharibika au kiongozi kukengeuka

Kwa sasa viongozi wamegeuka ndio katiba na wameamua kukanyaga sheria
 
Bila Katiba Mpya hata huo uchumi unaouzungumzia utaishia Mikononi mwa Wachache, kwani Hakuna Check and balance kwa Walio na Access kwenye Keki ya Taifa.

Ebu jiuilize Kama ndege zinanunuliwa kwa maamuzi ya mtu mmoja na Ukaguzi wake tulikuwa tunaambiwa Hakuna Hasara, pili ebu jiulize kama miradi yote Mikubwa including hizo flieover, SGR and Stergiou's gorge zote ukaguzi zero.

In short Katiba Mpya ndio uchumi Wenyewe vinginevyo Nchi inaendeshwa kwa rehema za Wachache.
 
Wengine inawezekana wakiwemo viongozi wakubwa serikalini wanatoa kisingizio cha gharama za kutengeneza katiba mpya. Lakini kama nchi tuna somo kwa kilichotokea 2014 kuhusu Bunge kuuuubwa la Katiba ambalo matokeo yake yalikosa kilichokusudiwa.

Watu takribani 20 (Tume ya Warioba) walifanya kazi nzuri kwa muda mfupi kuliko watu 300 waliokaa Dodoma muda mrefu wakilipwa posho nono na matokeo kuwa kichekesho.

Hili liwe funzo kwamba hatuhitaji lundo la watu kujazana Dodoma au Mwanza kutunga Katiba ambayo Msingi wake upo. Tungekuwa tunaanza from zero sawa, lakini vitu vingi vipo ni suala la kuboresha yaliyopendekezwa na Tume ya Warioba na Taifa likasonga mbele na Katiba inayokubalika na makundi yote, tukafuta uhasama unaochipuka na kuanza upya kama Taifa.

Hatuhtaji Matrilion ya fedha kufanya hili, Bali kukusanya Wazalendo kadhaa wenye uelewa na kuwaweka pamoja toka makundi yote na kisha wengine tukae pembeni tuwasikilize wanavyotutengenezea kitu muhimu kwa nchi.

Ni Nani akitaka kujenga nyumba anasimamisha shughuli nyingine zote kwenye familia yake? Yaani hatanunua nguo za watoto, hatakunywa hata soda kisa anajenga?

Taifa lenye maelewano (lugha moja) hupata maendeleo zaidi kuliko lenye mgawanyiko. Tutafute kitu kimoja kitakachotuleta pamoja tena kama Taifa halafu tuone kama tutakwama kisa tumetumia bilioni 120 kutengeneza katiba bora.
 
Are these two event depend each other or independent. Kama katiba mpya itaathiri ukuaji wa uchumi basi sawa tujenge kwanza uchumi lakini kama katiba mpya na uchumi haviingiliani basi tufanye vyote kwa pamoja, na tuendelee pale tulipoishia kipindi kile.

Ila uoga ndo wa chama tawala kuleta katiba mpya ndo unaoleta sababu mbali mbali.
 
Inawezekana kufanya yote kwa pamoja. Wenzetu wa Kenya waliacha shughuli za kukuza uchumi wakati wakiunda katiba yao mpya? Jibu ni hapana.

Mpango wa Mama wa kukuza uchumi kwa kualika uwekezaji toka nje ni sahihi. Lakini mwekezaji wa malengo ya muda mrefu anataka kuwa na uhakika wa kuweko sheria mama (katiba) inayodumu.

Kwa hivyo basi kuunda katiba mpya inayokubalika na wote ni kuita wawekezaji. Katiba ya sasa haikubaliki na Watanzania wengi. Vyama vya upinzani vinapinga hata kushiriki uchaguzi chini ya katiba hii. Kifupi ni katiba ambayo haimpi mwekezaji uhakika wa stability.

Tuwe na katiba mpya ili wote tuache kuhangaikia katiba na tuweke nguvu kwenye uchumi.

Hofu ya katiba mpya wanayo wachache tu wenye nia ya kuhodhi madaraka.
 
Utakuza vipi uchumi bila demokrasia?Wawekezaji na Demokrasia ni sawa na mtoto na mbeleko! Ikikatika mbeleko, mtoto huanguka!

Ukiminya Demokrasia, wawekezaji hukimbia! Huwezi kumnyima pumzi mama mjamzito ukategemea kuwa mtoto aliye tumboni ataendelea kuishi! Miujiza ya aina hiyo bado haijatendeka katika uso wa dunia.Demokrasia ndiyo pumzi ya wawekezaji.Hakuna demokrasia ni hakuna uwekezaji na ni hakuna ukuaji wa uchumi pia.

Mama ni inept leader anaelinda maslahi yake ya kujinufaisha kisiasa na kadhalika kwa kuitawala Tanzania kidikteta kama alivyofanya Magufuli ndiyo maana hajali yote haya.
 
Je, tung'ang'anie Katiba Mpya huku Uchumi wetu Ukidorora au tuimarishe na tukuze Kwanza Uchumi wetu na Katiba Mpya tuwaachie Vizazi vijavyo?

Leo nitakuwa ninasoma tu Maoni yenu.
Wewe jamaa yangu POPOMA sikiliza; Sisi tunataka Katiba Mpya ya Wananchi! Wengi tumegundua huu uchumi unao hubiriwa na hawa watawala wetu wawili; huyu wa sasa na yule mtangulizi wake, unawanufaisha wenyewe tu! Na siyo wananchi wa kawaida.

Yaani huo uchumi unakuwa kwa wanaccm pekee! Na siyo watanzania walio wengi. Si umewaona akina Mnyeti, Bashite, wanavyo ogelea kwenye dimbwi la utajiri, ndani ya muda mfupi? Ole Sabaya ndiyo kabisaa alinogewa na kujikuta amekuwa Jambazi sugu! Kwa sababu tu katiba ya sasa inawabeba zaidi wao, kuliko sisi tulio wengi na tusio na vyama.

Ila tukipata katiba iliyojengwa katika misingi ya usawa na haki kama ile iliyomo kwenye Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, Wallah nakuambia! nchi hii na wananchi wake tutaishi kama tuko peponi!
 
Mkuu kiualisia KATIBA ndiyo kila kitu
Uchuni unayo zungumizia injengwa na katiba , vilevile maendeleo ya fikra uletwa na katiba.
So in short katiba ndo kila kitu mzee.
Mama asikwepe majukumu yake ya kuleta katiba mpya kwa jusema hivyo
 
Je, tung'ang'anie Katiba Mpya huku Uchumi wetu Ukidorora au tuimarishe na tukuze Kwanza Uchumi wetu na Katiba Mpya tuwaachie Vizazi vijavyo?

Leo nitakuwa ninasoma tu Maoni yenu.
Katiba first uchumi haukuzwi kwa siku moja ni endelevu.
 
Uchumi bora huleta ustaarabu....automatically tu watu wakiwa na uchumi bora wanastaraabika na hapo ndio utapata katiba bora kabisa...wapi ulisikia katiba bora inatengenezwa na watu wenye njaa?...
 
Kwa hiyo wewe unaamini Mama Samia atajenga uchumi wa Tanzania?
Tanzania ilijengwa na inajengwa na itajengwa na watanzania wenyewe na sio mtu mmoja.

Katiba ni muhimu na uchumi ni muhimu na hivi vyote vinaweza kifanyika kwapamoja.

Tuache kuonana wajinga
 
Kwani Katiba inazuiaje kujenga uchumi? Hivi mwekezaji gani makini anayeweza kuja kuwekeza hapa akijua kuwa Katiba hii ndiyo iliwezesha kulea dikteta mwendazake? Yaani hatima ya nchi inategemea Rais kaamkaje,akija kichaa zaidi ya mwendazake tunarudi kulekule.
 
Back
Top Bottom