Watanzania tuamueni lililosahihi hapa tafadhali

Watanzania tuamueni lililosahihi hapa tafadhali

Wewe jamaa yangu POPOMA sikiliza; Sisi tunataka Katiba Mpya ya Wananchi! Wengi tumegundua huu uchumi unao hubiriwa na hawa watawala wetu wawili; huyu wa sasa na yule mtangulizi wake, unawanufaisha wenyewe tu! Na siyo wananchi wa kawaida.

Yaani huo uchumi unakuwa kwa wanaccm pekee! Na siyo watanzania walio wengi. Si umewaona akina Mnyeti, Bashite, wanavyo ogelea kwenye dimbwi la utajiri, ndani ya muda mfupi? Ole Sabaya ndiyo kabisaa alinogewa na kujikuta amekuwa Jambazi sugu! Kwa sababu tu katiba ya sasa inawabeba zaidi wao, kuliko sisi tulio wengi na tusio na vyama.

Ila tukipata katiba iliyojengwa katika misingi ya usawa na haki kama ile iliyomo kwenye Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, Wallah nakuambia! nchi hii na wananchi wake tutaishi kama tuko peponi!
Swadaktaaa
 
Uchumi tumeshahangaika nao zaidi ya miaka sitini toka tupate uhuru umetushinda, bado umasikini umetapakaa kila kona, bora sasa tuanze na Katiba Mpya, huo uchumi atakuja kuuinua mwingine mwenye maono mapya.
 
Back
Top Bottom