Watanzania tubadilike, Kiswahili chetu ni kibovu sana

Watanzania tubadilike, Kiswahili chetu ni kibovu sana

MUTUYAMUNGU

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
1,825
Reaction score
4,374
Kiingereza hatujui na lugha yetu adimu na adhimu kila siku tunaiharibu kwa kuingiza maneno ya kihuni. Tunakosa nafasi za kufundisha nje ya nchi pamoja na kazi za kutafsiri.

Tutumie lugha moja ili tupate nafasi za kufundisha Uganda, Rwanda, South Africa na kwingineko!

Uganda, Rwanda na South Africa waalimu wote wa kiswahili wanatoka Kenya!
 
Awezi/Hawezi
Atari/Hatari
Alusi/Harusi
Imehairishwa/imeahirishwa

L na R nazo huko ndio kuna hasara kubwa sana.
Siamini katika kutumia nguvu ili kumfundisha mtu.Lakini wanaofanya makosa hayo,hasa katika kuandika,wanatakiwa kukamatwa,kufungwa kamba na kutandikwa fimbo nyingi hadharani hadi mpigaji achoke.
 
Hiyo sio sababu. Sababu ni kwamba watanzania hawajui English. Unapotaka kumfundisha mtu lugha asiyoifahamu inabidi kuwe na lugha ya kumfundisha huyu mtu. Hapa ndipo English inapoingia na ndio hapa hawa jamaa wa 🇰🇪 wanapotupiga bao
 
Tunawalimu wazuri you wa kiswahili nahisi balozi zetu hazifanyi kazi sawa sawa kihakikisha Hilo ma pia watu wetu hawana Ile shauku ya kutafuta fursa zaidi nje ukiongezea na serikali yeti kukwamisha Kila kitu
 
Hakuna jambo linaloniudhi kama kumsikia Mtanzania anaongea kwa lafudhi na maneno mabovu ya kiswahili cha Kenya.
Vyuo vikuu vya Norway na Canada waalimu was Kiswahili wengi ni wakenya.

Uganda sasa hivi somo LA kiswahili ni lazima ila shule zinalalamika hazina waalimu.

Tafuta mzanzibari au MTU was Lamu Kenya usikie Kiswahili fasaha.
 
Wanapoenda kufundisha,wanafundisha ufasaha wa lugha.Hawapeleki sheng za mitaani.
 
Hiyo sio sababu. Sababu ni kwamba watanzania hawajui English. Unapotaka kumfundisha mtu lugha asiyoifahamu inabidi kuwe na lugha ya kumfundisha huyu mtu. Hapa ndipo English inapoingia na ndio hapa hawa jamaa wa 🇰🇪 wanapotupiga bao
Kweli mkuu? Ile English yetu ya form four ya Chinua Achebe na Things Fall Apart haiwezi kumfundishia MTU lugha mama?
 
Tunawalimu wazuri you wa kiswahili nahisi balozi zetu hazifanyi kazi sawa sawa kihakikisha Hilo ma pia watu wetu hawana Ile shauku ya kutafuta fursa zaidi nje ukiongezea na serikali yeti kukwamisha Kila kitu
Ramaphosa katoa fursa kule South somo LA kiswahili lifundishwe ila balozi wetu kule MEJA JENERALI MILANZI anashangaa tu!
 
Kweli mkuu? Ile English yetu ya form four ya Chinua Achebe na Things Fall Apart haiwezi kumfundishia MTU lugha mama?
Na exposure vile vile. Wakenya hadi wanaotoka vijijini utawakuta wametapakaa nchi mbalimbali duniani to tofauti na wabongo ambapo ukimkuta nchi za mbali basi atakuwa ametoka kwenye miji mikubwa. Halafu kumbuka mtu anakwenda kufundisha University sio vichocholoni hivyo hiyo English yake lazima iwe imenyooka kuanzia kwenye interview
 
Kiinglish hatujui kiswahili tabu....yani ni shida juu ya shida, wanaoharibu kiswahili wakabidhiwe kwa bwana nchemba atajua cha kuwafanya
 
Mtu akisema"Mama Samia anaupiga mwingi"anamaanisha nini,uo unaopigwa mwingi unakua ni nini?
 
Back
Top Bottom