Siyo kulala kaka ,hizi ni kazi za Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Balozi zetu, wewe umejua baada ya kwenda lakini kabla hujaenda hukujua, sasa ni Watanzania wangapi hatuzijui hizo nafasi, Wakenya wao walijua kupitia kwa watu wao.
Tanzania kuna ukiritimba mkubwa mno kwenda nje kufanya kazi, vibali havitoki kwa wakati na kiurahisi. Roho mbaya na chuki binafsi zinaongoza kwenye ofisi nyingi hasa Wizarani. Chunguza chunguza ni nyingi kwa mtu anayekwenda nje kuliko anayeingia ndani.
Hakuna uwazi wa hizi nafasi pindi zinapotokea, wakati mwingine mtu anaona bora asiseme kwa kuwa hakuna mtu wake, wote wakose. Hii inapelekea kwenda kwa wengine.
Nikupe kisa. Kuna siku walikuja wageni katika Wizara moja hapa nchini wakihitaji wafanyakazi wa kwenda nao field kufanya nao kazi ya utafiti. Wakawaomba idadi wanayohitaji.
Wakawaonyesha scale ya mshahara wao. Aisee wale viongozi walipinga kwamba haiwezekani walipwe pesa yote hiyo kwasababu serikali hailipi hivyo. Wazungu wakashangaa na kusema hata kama ila sisi tumepangiwa tulipe hiki kiasi, kwahiyo siyo nyinyi mtalipa bali serikali yetu, wakaambiwa mkiwalipa pesa yote hii hawatafanya kazi watalewa tu.
Wazungu wakasema hatuwezi kurudisha pesa bila maandishi tutaonekana tumewadhulumu tupeni doc inayoonyesha kiwango hiki cha mshahara mmekipinga. Kweli bwana walipewa na pesa zikarudishwa.
Lengo la kufanyiwa mtima nyongo ni wivu kwasababu waliotakiwa kwenda field ni wafanyakazi wa ngazi za chini, hivyo basi waliona watalipwa pesa nyingi kuliko wao wakubwa. Ofisi nyingi wanafanya hivi, hiyo ni moja kwingine je penye ulaji mkubwa kukoje?