Watanzania tubadilike, Kiswahili chetu ni kibovu sana

Kweli kabisa mkuu.
 
Kiinglish hatujui kiswahili tabu....yani ni shida juu ya shida, wanaoharibu kiswahili wakabidhiwe kwa bwana nchemba atajua cha kuwafanya
Primary na secondary za Uganda na South Africa nyingi wanafundisha kiswahili sasa hivi. Wizara ya mambo ya nje na Wizara za kazi+uhamiaji wawawezeshe watanzania.

TANZANIA KUPATA TU PASSPORT YA KUSAFIRIA NI MUZIKI MZITO.
 
Tanzania kupata tu hiyo passport utaita maji mmaa!

Utaulizwa cheti cha kuzaliwa cha bibi yako na babu yako
Kuna oportunities nyingi sana za kufundisha kiswahili, kuna Nchi ambayo nipo, wakenya walikua wemeshikilia dept ya kiswahili lakini siku walipokutana na sisi Watanzania walisema nyinyi ndio mnajua kiswahili hadi leo wanaamini watamzania ndio tunaongea kiswahili fasaha na wanatafuta walimu sema sisi tumelala hatujiongezi!
 
Kweli mkuu tumelala sana. Ule moshi wa mwenge wa Uhuru umetupambaza sana. Uchawi wa Nyerere kiboko
 
Hujui tu! Tanzania hii kupata tu passport ni shughuli pevu,watu kukupa passport ni kama vile wanakupa roho!! Inakatisha tamaa hata pale watu wanapoamua kujiongeza
 
Kweli mkuu tumelala sana. Ule moshi wa mwenge wa Uhuru umetupambaza sana. Uchawi wa Nyerere kiboko
Tuwe aggressive kwenye kupambana kutafuta channels za nje!.tuaisubiri serikali ifanye kila kitu. Kama passport as long as wewe ni mtanzania utaipata tu.
 
Hujui tu! Tanzania hii kupata tu passport ni shughuli pevu,watu kukupa passport ni kama vile wanakupa roho!! Inakatisha tamaa hata pale watu wanapoamua kujiongeza
Kunana watu wana namba za NIDA tangu 2018 ila vitambulisho halisi hawajapewa hadi Leo. Hii ndio tz
 
Nasikia wakenya wanatuzidi kwa kuongea kiswahili vizuri!!
Nashangaa kivipi??
 
Awezi/Hawezi
Atari/Hatari
Alusi/Harusi
Imehairishwa/imeahirishwa

L na R nazo huko ndio kuna hasara kubwa sana.
Apana/ Hapana
Akuna/ Hakuna
Ayupo/Hayupo
Akuja/ Hakuja
Akipo/ Hakipo
Akika/Hakika.

Kuna shida mahali kwenye ufundishaji.
 
Ramaphosa katoa fursa kule South somo LA kiswahili lifundishwe ila balozi wetu kule MEJA JENERALI MILANZI anashangaa tu!
Balozi zetu kwa kweli hazitoi ushirikiano wa kutosha kwa Watanzania kuchangamkia fursa wamekazana na diplomasia tu.
 
Siyo kulala kaka ,hizi ni kazi za Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Balozi zetu, wewe umejua baada ya kwenda lakini kabla hujaenda hukujua, sasa ni Watanzania wangapi hatuzijui hizo nafasi, Wakenya wao walijua kupitia kwa watu wao.

Tanzania kuna ukiritimba mkubwa mno kwenda nje kufanya kazi, vibali havitoki kwa wakati na kiurahisi. Roho mbaya na chuki binafsi zinaongoza kwenye ofisi nyingi hasa Wizarani. Chunguza chunguza ni nyingi kwa mtu anayekwenda nje kuliko anayeingia ndani.

Hakuna uwazi wa hizi nafasi pindi zinapotokea, wakati mwingine mtu anaona bora asiseme kwa kuwa hakuna mtu wake, wote wakose. Hii inapelekea kwenda kwa wengine.

Nikupe kisa. Kuna siku walikuja wageni katika Wizara moja hapa nchini wakihitaji wafanyakazi wa kwenda nao field kufanya nao kazi ya utafiti. Wakawaomba idadi wanayohitaji.

Wakawaonyesha scale ya mshahara wao. Aisee wale viongozi walipinga kwamba haiwezekani walipwe pesa yote hiyo kwasababu serikali hailipi hivyo. Wazungu wakashangaa na kusema hata kama ila sisi tumepangiwa tulipe hiki kiasi, kwahiyo siyo nyinyi mtalipa bali serikali yetu, wakaambiwa mkiwalipa pesa yote hii hawatafanya kazi watalewa tu.

Wazungu wakasema hatuwezi kurudisha pesa bila maandishi tutaonekana tumewadhulumu tupeni doc inayoonyesha kiwango hiki cha mshahara mmekipinga. Kweli bwana walipewa na pesa zikarudishwa.

Lengo la kufanyiwa mtima nyongo ni wivu kwasababu waliotakiwa kwenda field ni wafanyakazi wa ngazi za chini, hivyo basi waliona watalipwa pesa nyingi kuliko wao wakubwa. Ofisi nyingi wanafanya hivi, hiyo ni moja kwingine je penye ulaji mkubwa kukoje?
 
Nimekupata mkuu inaonekana kuna mambo mengi ya kubaniana nyuma ya pazia ila ni kawaida kwa ngozi nyeusi. Kikubwa ni kuendelea kupambana bila kutegemea wizara au serikali channels zipo na unaweza ukafanikiwa bila kutegemea mtu yoyote.
 
Ili mradi tunaelewana acha maisha yaendelee mkuu.
 
Nimekupata mkuu inaonekana kuna mambo mengi ya kubaniana nyuma ya pazia ila ni kawaida kwa ngozi nyeusi. Kikubwa ni kuendelea kupambana bila kutegemea wizara au serikali channels zipo na unaweza ukafanikiwa bila kutegemea mtu yoyote.
Ni kweli ngoja tupambane pasipo kukata tamaa yapo mambo huwa yanawezekana kwa kukomaa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…