Watanzania tubadilishe fikra za kufanya biashara

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Unakuta mtu anakomaa afungue biashara peke yake matokeo yake anaishia kusajili kampuni ama anafungua biashara kwa kutumia gharama kubwa mno ambayo wengi wao wanakuja kupoteza investment zao kwasababu katika kuanzisha biashara huwa hakuna kujiamini moja kwa moja kama ulichoanzisha kitafanikiwa. Mwisho wa siku wengi wetu tumekuwa tukiunguza pesa nyingi sana kuanzisha mambo ambayo yanakuja kufeli.

Kwanini labda kama mtu una idea nzuri ya biashara usitafute wenzako kama kumi mkachanga mtaji wa hata milioni kumi (moja kila mtu) halafu mkafanya planning ya kutekeleza hilo wazo?

Faida ya kufungua biashara ama kampuni mkiwa wengi ni kwamba

  • Inapunguza risk ya kuchoma mahela yako mengi kwa ajili ya wazo la biashara ambalo halijazaa matunda bado. Imagine uchungu wa kupoteza milioni 10 wewe mwenyewe na ule uchungu wa kupoteza milioni 1 ikiwa mlikuwa kikundi?
  • Mnapokuwa wengi inaongeza urahisi wa kufanikiwa kwenye jambo kwa maana kwenye watu kumi mtakuwa ni wetu wenye profession tofauti tofauti ambayo ni faida sana kwa biashara inayoanza kwa sababu inarahisisha kufanikiwa kwa mipango ya kibiashara inayopangwa.

Huko nchi za wenzetu aina hii ya ufanyaji wa biashara ama ufunguaji wa makampuni ndio imeshamiri huko na ndio mfumo wa maisha.

Imagine kwa mfano, mimi kuna classmate wangu wa form 6 juzi nilikutana naye. Yeye amekuwa ni mjasiriamali wa kutengeneza hizi mambo za culture culture. Ila kwa kumuangalia kwa haraka haraka, yeye inaonyesha hana mtaji wa kutosha.

So hapo mimi nikaona fursa kwamba naweza kumuita nikaongea naye halafu nikampa hata wazo la kupanua biashara yake kwa mimi kumuongezea mtaji wa lets say milioni 5, ambayo najua kabisa hiyo milioni tano yangu anaweza kutafuta mahali kwenye biashara akalipia kodi na ikampa capacity ya kuweza kuzalisha zaidi na kuongeza faida ya biashara yake.

Ama kama alikuwa na ofisi moja au duka unampa capacity ya kuanzisha duka la pili kwenye sehemu yenye mzunguko ambayo unajua kabisa kutakuwa a potential.

So hapo nikawa nafikiria, kuliko mimi mwenyewe nimpe hiyo milioni tano ni kwanini nisipate wadau kama 20 tukakusanya hata laki mbili na nusu kila mmoja (250K x 20 = 5 Million) halafu akatupa 60% kama mmoja wa wamiliki wa biashara ambayo baadae itakuja kutunufaisha kwenye gawio?

Imagine mwaka wa kwanza biashara ikareport profit ya kama Tzs 2 Million hapo ina maana kama investors tukichukua 60% yetu hiyo ni kama Tzs 1.2 Million ambayo tukiigawanya kwa investors wote 20 ni kama kila mtu atakuwa amepata dividend ya Tzs 60,000 ambayo ni sawa na 24% return kutoka kwenye uwekezaji wake wa Tzs 250,000.

Umeona how lucrative is? (24% returns per year) Na huu ni mfano namna hivi vitu vinavyofanya kazi.

Kama kuna mtu kanielewa ni kwamba tunaweza tukafanya namna tukatengeneza kikundi cha watu wachache ambao tutakuwa kama wawekezaji wa pamoja kwenye biashara hizi ndogo ndogo ama ideas ambazo mmoja wetu anaweza kuja nazo.

Then kwa sababu tunaweza kuwa watu wenye profession zetu tutakuwa tunaangalia biashara ama wazo kwa angle nzuri ambayo itahakikisha kila wazo linalowezeshwa ni lile lenye potential ya kufanikiwa. Ama kutafuta biashara ndogo yenye potential ya kukua huko mbeleni.

Hii ndo namna biashara inavyofanyika kwenye karne ya 21.

Kama tupo on the same page embu comment chochote.
 
Kwa mfumo huu wa biashara sidhani kama utafika mbali
Sababu kubwa ni kuwa watu hawajzoea kufanya biashara pamoja na la pili ni uaminifu
Uaminifu ni moja lingine ni kuibiana
Wazungu biashara inaanza na mtu mmoja au familia moja na inapokuwa na anahitaji kukuza biashara akijua kuwa imefika sehemu nzuri na haiyumbi tena
Hapo ndio anatafuta share holders

Lakini biashara mpya kuanza na watu wengi ni ngumu sana kwani hakuna guarantee ya kukua

Tafuta mwenye biashara ya uhakika na wekeza kwake kiasi cha fedha au chochote ambacho hiyo biashara ilivyo kama ni Mkulima na hana uwezo wa kununua tractor, ingia nae ubia wa kuwekeza tractor kwa mfano
Hapo unaweza kuwa umepata mtu wa kusukuma nae gurudumu

Huo ni mfano tu na zipo biashara nyingi unazoweza kuingiza hela yako lakini biashara mpya na watu wengi ni mtihani
Na mwisho wake huwa ni mbaya

Huu ni ushauri tu sio kuwa napinga fikra zako
 
Comment tatu tu.. Tayar watu washaanza kuwa negative instead ya kuwa na solution to every challenge wameshakuja na challenge to every solution.

Huwez kufanikiwa kwa mindset ya namna hii ya kutanguliza kuona matatizo badala ya fursa
 
Watanzania wamerogwa tena mnoooooooooooo.

Watakuja kukumbuka shuka kumekucha kabisa.

Kila mtu ana vimatumaini koko akidhani eti atafanikiwa,upuuzi mtupu.

Binafsi nimewahi kuwashirikisha hili.

LINK 1 : Cheki hapa Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara . Hapo kila takataka inaona kama naiomba msaada inisaidie.

2. LINK 2 Unayo akiba ya Tsh 150,000 kila mwezi na hutaki kufa Masikini, Kataa Ubinafsi, Soma Hapa

Tuendelee tu kwenda kuwaimbia wanasiasa baba baba baba huyooooooooooooooo

Ushirikiano kwa vijana wa kitanzania hata uwaambie tutaweka kila kitu kisheria ndo kwanza watakuona tapeli, labda uwaambie WATATAJIRIKA KESHO kupitia QNET, FOREVER, AIM GLOBAL.

Hapo utayadaka kama mbuzi
 
😁😁😁😁😁😁😁
 
Usitake kulazimisha kila mtu awe na mtazamo kama wako. Wote hatuwezi kuwa na mtazamo sawa.Na wewe pendekeza soln au fursa ulizozioona kupitia hii thread acha kulaumu.
 
Watanzania wamrogwa tena mnoooooooooooo.

Watakuja kukumbuka shuka kumekucha kabisa.

Kila mtu ana vimatumaini koko akidhani eti atafanikiwa,upuuzi mtupu.

Binafsi nimewahi kuwashirikisha hili.

LINK 1 : Cheki hapa Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara . Hapo kila takataka inaona kama naiomba msaada inisaidie.

2. LINK 2 Unayo akiba ya Tsh 150,000 kila mwezi na hutaki kufa Masikini, Kataa Ubinafsi, Soma Hapa

Tuendelee tu kwenda kuwaimbia wanasiasa baba baba baba huyooooooooooooooo

Ushirikiano kwa vijana wa kitanzania hata uwaambie tutaweka kila kitu kisheria ndo kwanza watakuona tapeli, labda uwaambie WATATAJIRIKA KESHO kupitia QNET, FOREVER, AIM GLOBAL.

Hapo utayadaka kama mbuzi
Ngoja nikazisome hizi
 
Comment tatu tu.. Tayar watu washaanza kuwa negative instead ya kuwa na solution to every challenge wameshakuja na challenge to every solution.

Huwez kufanikiwa kwa mindset ya namna hii ya kutanguliza kuona matatizo badala ya fursa
Wengine hayo yalishatukuta kwny utafutaji na pia tulishawashauri wengine kama wewe wakawa wabishi sasa wako wanapambana na hali yao na ndio maana tunakataa jambo hili.

Sasa wewe sababu hujawahi kufanya hio kitu ndio maaana unadhani hili wazo lako ni genuine/wazo jipya/bonge la wazo.
 
Wote wanajaribu ku show negative side yake. Sio kupinga. Kwan Kila Jambo liko hivyo upande wa faida na hasara pia
 
Wengine hayo yalishatukuta kwny utafutaji na pia tulishawashauri wengine kama wewe wakawa wabishi sasa wako wanapambana na hali yao na ndio maana tunakataa jambo hili.

Sasa wewe sababu hujawahi kufanya hio kitu ndio maaana unadhani hili wazo lako ni genuine/wazo jipya/bonge la wazo.
Mlifungua kabiasa kampuni kisheria au mlifanya kikundi koko tu kwa kuaminiana ?
 
Comment tatu tu.. Tayar watu washaanza kuwa negative instead ya kuwa na solution to every challenge wameshakuja na challenge to every solution.

Huwez kufanikiwa kwa mindset ya namna hii ya kutanguliza kuona matatizo badala ya fursa

Hapo ndio unakosea kabisa
Hoja inapingwa na hoja
Huko unakosema kwa wengine ukikusudia kwa wazungu nawajua
Hayo ni niliyoandika ndio ukweli take it or leave it
 
Watanzania wamerogwa tena mnoooooooooooo.

Watakuja kukumbuka shuka kumekucha kabisa.

Kila mtu ana vimatumaini koko akidhani eti atafanikiwa,upuuzi mtupu.

Binafsi nimewahi kuwashirikisha hili.

LINK 1 : Cheki hapa Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara . Hapo kila takataka inaona kama naiomba msaada inisaidie.

2. LINK 2 Unayo akiba ya Tsh 150,000 kila mwezi na hutaki kufa Masikini, Kataa Ubinafsi, Soma Hapa

Tuendelee tu kwenda kuwaimbia wanasiasa baba baba baba huyooooooooooooooo

Ushirikiano kwa vijana wa kitanzania hata uwaambie tutaweka kila kitu kisheria ndo kwanza watakuona tapeli, labda uwaambie WATATAJIRIKA KESHO kupitia QNET, FOREVER, AIM GLOBAL.

Hapo utayadaka kama mbuzi
FOREVA LIVING AT WORK.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom