Wazo nzuri ila Watu wengi wamejaa kuwaza hasi kichwani mwao....kushindwa kwa ubia wenu wa kwanza isiwe sababu ya ubia utakaokuja kuundwa nao kushindwa...na tusipende kusema mambo kiujumla eti watz wengi hawawez kufanya biashara za ubia,eti hawaaminiki,..la hasha...Nina ushahidi mwingi tu vijana tena wamekutana mitandaoni tu km hivi...wakaundwa kampuni ya kilimo miaka 5 imepita..na bado wanazidi kupiga pesa, kuna vijana wengine wameweka ushirikiano wa kujengeana nyumba kila mmoja kupitia mishahara yao...waliweka makubaliano yao kwenye maandishi...wamefanikiwa kila mtu kujengeana Nyumba nzuri kwa awamu...(yaan miaka mitatu tunajenga nyumba ya japhet,miaka mitatu mingine nyumba ya Joshua....na limewezekana...sio ndg wala nini...ni marafiki tu wenye the same interest ya mafanikio,.pia vijana wengine wanafanya ufugaji wa nguruwe miaka mitatu sijasikia hiyo migogoro.,,kuna jamaa zangu wana saccos yao wanaume tupe...imedumu miaka mingi tu...sasa hivi wana benk hapa mjini,Mimi mwenyewe mwaka wa tano huu wafanyakazi wenzangu wanawekeza pesa zao kwangu mi nazalisha kupitia biashara zangu nawapa faida 7% ya pesa aliyoweka kwa mwezi,kila baada ya miez mitatu nawapa faida yao,hakuna malalamiko yeyote,(ina maana nao ni ubia pia ingawa wao hawaingia kwenye mchakato wa kuizalisha ile pesa na kujua imeleta faida kias gani) wanaridhika..Kwa hyo kufanya biashara za ubia na kufanikiwa inawezekana...sema upate watu sahihi,wenye kiu na mafanikio kweli...sio hawa watoto wa chips mayai eti ameshiba...hata kwenye mafanikio account ikianza kusoma 5 millions anaona kafanikiwa...anaanza mawenge...VIJANA WAPO WANAOFANYA UBIA NA WANAFANIKIWA.. NA NDO MFUMO WA BIASHARA WA KARNE YA 21....tofauti na hapo komaa mwenyewe na familia yako basi...maana sio lazima utafute watu wa nje na familia yako...chukua hata Mjomba,kaka,shangaz,mama,baba,...n.k labda hao utawaamini zaidi.
Tusijifanye kila kitu tunakijua eti tulishajaribu...hailipi sijui ...tulikosana na nani kisa ubia...yaweza kuwa mikakati,makubaliano,na uendeshaji wenu haukua mzuri...VIJANA WATANZANIA TUAMKE ,TUHAMASISHANE KUHUSU MAFANIKIO,TUSIWE WAPESI WA KUKATISHANA TAMAA....DUNIANI HAPA KILA JAMBO LINAWEZEKANA....NI SWALA LA MUDA TU. leo tunatumia % kubwa ni bidhaa za China...fatilia wamiliki wa hizo kampuni...nyingi utakuta zinamilikiwa na watu zaidi ya 5,10,nakuendelea... ,
"The different between ordinary and extra ordinary is that little extra" zig zaglar.