Watanzania tuchangamkie fursa kibao zitazokuja na DP-World

Tulichelewa wapi??? Hata ATCL, SGR, TANESCO, TPDC, VIWANJA VYA MPITA, ETC TUBINAFSISHE TU
Ongezea na brt hapo,mradi una miundo mbinu mizuri na pendeleo lakini hauna tija yoyote waliopewa kutwa wanalalamika hasara,while nchi za wenzetu bus kama zile full kiyoyozi na abiria sio wengi nauli tofauti kidogo usikii kulalamika
 
Unachanganya mambo! UBINAFSISHAJI ni moja ya mbinu za UWEKEZAJI.
Kuhusu NMB kufanya kazi vizuri ni kwasababu bado serikali ya Tanganyika inamiliki asilimia 31% ya hisa.

Hiyo NBC ambayo ABSA Group wanamiliki hadi asilimia 55% nini kikubwa kimefanyika ???
 
Sawa tuko tayari. Sisi tunataka fursa. Tuwaache watoa povu za ukabila ukanda na udini waendelea kumuandama rais kwa uzanzibar wake.
 
Hao wapuuzi wanavaa vilemba kuficha ushetani wao, mawakala ya shetani ndio yameitana kwenye huu uzi.
 

SiO NBC tu hata NMB inamilikiwa kwa 34.9% na Norway wakati TZ ina 31% tu. NMB ndo bank yenye assets nyingi zaidi bongo na ufanisi uliongeze baada ya kuleta wageni. Kitu ambacho wamatumbi mlikua against vehemently.

Wakati Mlimani city inajengwa mlisema JK kauza nchi ila leo mmesahau na kila siku mnashinda pale mmekenua.

Bandari bado ni mali ya TZ, DP World is a management company. DPW wanaweka ukwasi wao na utalaam, lazima wapate faida na sisi tunataka ufanisi na mapato yaongezeke.

I'm not against ubinafsishali/uwekezaji so long as mkataba ni mzuri.
 
Reactions: Tui
Hakuna fursa za maana kwa watanzania na zaidi wafanyakazi wa bandari watapunguzwa kama njugu, wale jamaa wa clearing and forwarding nao watabaki wachache sana sio muda vilio vitaanza
 
Migodi si pia inapigiwa kelele kwani ni waarabu wale? Nyie ndio mnawatetea kisa ni ndugu zenu, ila sisi tutapinga hata wawe waafrica wenzetu, yaani hata wangekuwa ni Warundi.
Hayo majitu ni mapuuzi sana.
 
Mombasa bandari ilikufa na sasa wana kesi na DP world japo wao wameirudisha tayari kwa sasa
 
Nawashauri vijana anzeni kuwatafuta CDC Group ya Uingereza, utaingia kwa kishindo.

Msiseme hamkuambiwa.
Nina maswali kidogo kuhusu mambo haya ninaweza kukuuliza PM mkuu
 
Hakuna fursa hapa. Kwa nijuavyo waarabu, bila kuwa mtu wa dini yao, vinginevyo uwe mbobezi, fursa hapa huna.
 
Una makasiriko makubwa sana lakini inaonesha hata wewe mwenyewe hufahamu nini unasema. Kinachokutesa wewe ni kupenda udini kupita kiasi hadi unashindwa kutazama ukweli ambao uko wazi kabisa. Mifano uliyoileta hapa, kuhusu DP World kushughulika nchini Uingereza na Marekani ni geresha zisizo na kichwa wala miguu kwasababu mkataba uliosainiwa baina ya DP World na Uingereza uko tofauti kabisa na ule uliosaniwa baina ya DP World na Marekani, vivyo hivyo uko tofauti kabisa na ulivyosainiwa na Tanganyika ambapo kiuhalisia waarabu wamepewa umiliki wa pekee (Exclusive Right) wa bandari za Tanganyika.

Pole sana, lakini muda siyo mrefu tutarudi kupitia hizi nyuzi. Tuendelee kuomba uzima...
 
Nioneshe huo mkataba WA waarabu na UK nione hio tofauti?
Exclusive rights unaelewa maana yake? Hata Azam TV Wana exclusive rights ya kutangaza mpira Tz..ndo nature ya mkataba ...ulitaka mkataba uruhusu wawekezaji wengine kwenye bandari hizo hizo??
 
Reactions: Tui
Bandari bado ni mali ya TZ, DP World is a management company. DPW wanaweka ukwasi wao na utalaam, lazima wapate faida na sisi tunataka ufanisi na mapato yaongezeke.
Unafahamu ni sababu zipi zimeifanya NMB kuwa na mali nyingi na kufanya vizuri zaidi kuliko NBC ???
Wala sababu siyo wageni peke yake, labda hili uwadanganye ambao hawaifahamu Tanzania.

Unaposema bandari bado ni mali yetu, na DP World ni waendeshaji unamaanisha nini ???
Unaufahamu taratibu na sheria kwenye aina ile ya uwekezaji mkuuu

Halafu mwisho kabisa, kwani Mlimani City ilijengwa na Jakaya au Mkapa ??? Umiliki wake ukoje ???
Hebu tusaidiane katika hili,....
 
We bibi funguka bhas hizo fursa ili nianze kupiga short course zakupiga ajira nahao DP
 

NMB na NBC zimefufuka baada ya wageni that's factual. Mlipiga kelele hizi hizi.

Mcity mlipiga kelele hizi hizi enzi za Mkapa/JK. Point is, kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.

SSH akanyage hapo hapo. Mikataba ipitiwe thouroughly ila asirudi nyuma. Akimaliza aende TANESCO, TAA, TANAPA, TANROADS, TTCL, TFS etc etc.

Boma Liwanzaaaa.
 
Nioneshe huo mkataba WA waarabu na UK nione hio tofauti?
Exclusive rights unaelewa maana yake? Hata Azam TV Wana exclusive rights ya kutangaza mpira Tz..ndo nature ya mkataba ...ulitaka mkataba uruhusu wawekezaji wengine kwenye bandari hizo hizo??
Exclusive Rights ambayo inazungumzwa hapa ni kama ile ambayo inatolEwa kupitia Bilateral Investment Treaties (BIT). Tanzania na UEA hatuna BIT hivyo tumesaini Hosting Government Agreement (HGA) kulinda huu uwekezaji, na huu mkataba unawapa wawekezaji wa UAE haki kama zile ambazo ziko chini ya BIT. Sasa hapa tunaposema Exclusive Rights, tunamaanisha haki ya kuendeleza bandari za Tanzania bila kuingiliwa na mtu mwingine awaye yote ikiwemo serikali ya Tanganyika.

Hapa kanuni kama The Most Favoured National na Rules Against Expropriation zinafanya kazi. Endapo mtamgusa basi lazima mpelekwe mburuzwe kwenye mahakama za kimataifa mpaka akili ziwakae. Hili la Exclusive Rights ni moja ya jambo lililoleta ukakasi kwenya majadiliano ya mkataba wa bandari ya Bagamoyo dhidi ya China Merchants na serikali ya Tanganyika.

Sasa ninyi endeleeni kupiga vigelegele kwasababu tu Raisi ni muislamu mwenzenu na mmekuwa na chuki nzito hata hamuoni kwamba hata yeye Raisi ataingia kwenye mtego mzito siyo muda mrefu. Sisi yetu ni macho tu...
 

Unaweza kuwa uko sahihi..
Tatizo lako ni kuingiza dini sehemu isiyo husika....
Unaweza kosoa bila kuingiza chuki za kidini...
Unaweza kuwa sahihi na Mimi ni kawa wrong...bila kuleta mada za dini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…