Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mamndenyi; unamaanisha nikawaida hivyo tuendelee kusupport uharibifu wa pesa za umma.heeee mbona ni kawaida sana,
Naona huko makini kweli Hongera nimetambua kosa langu, na wewe muda umefika wa kuachana na imani potofu.Ongera ndio nini?
Ninazingojea pesa mpya za Uingereza nitengeneze chuma ulete wa kuzivuta Pound ya Mwingereza lohhh majangaa hayo ...Australia wanachapisha noti za plastic zinazodumu muda mrefu, noti hizi huwezi kuzichana pembeni hata Uingereza wameanza utaratibu huu. Kuchapisha hela ni gharama. Tuanze kuwa wastaarabu.
Tulia hayo mambo huyajuiLeo hii kumekuwa na ongezeko kubwa la noti kuukuu, zilizochakaa na kuchanwa kwenye ncha au kutobolewa kwa makusudi kabisa kisa wafanyabiashara wanaamini katika ushirikina.
Watanzania wenzetu mnahiaribia nchi yenu wenyewe uchumi wake, haiwezekani pesa umeipokea ni nzima tena mpya inanukia wewe unakunja kunja kama toilet pepa then unaitunza mahali unapojua wewe ukija kuitoa huko kumpa mwenzio utazani imetafunwa na ng'ombe kwa namna hii kwa nini pesa yetu isidharaulike, kwanini mkipewa dollar mnaitunza kwa heshima kuliko mnavyojali vitambulisho vyenu vya NIDA.
Sasa kuna huu mtindo ulioibuka wa sasa sijuhi nani katukaririsha ujinga huu kwa jina CHUMA ULETE kama serikali isipochukua hatua kutokomeza kirusi hiki kipya dhidi ya NOTI zetu hasara ni kubwa.
Haiwezekani katika noti kumi ulizonazo mfukoni lazima ukutane na iliyochanwa au kunyofolewa kipande, katika hizo nawe unakimbilia kuichambua kwenye waleti chap ile yenye tatizo umshikishe mwenzio usibakie na msala huo peke yako matokeo yake mpaka ATM zetu nazo zimeanza kuzitapika noti hizo hizo cha ajabu hata public awareness haifanywi na wadau au serikali pengine wameridhika na hali au ndo tuseme bado wanamudu uharibifu huu.
Kama pesa zetu tumezidharau wenyewe nakuzishusha thamani kiasi cha kuziita pesa za madafu bado hata kuziona zikiwa nzima pia tunaona donge, tafadhali tuachane na dhana hizi potofu za imani zisizo na maana yeyote ndugu Watanzania wenzangu.
Ikiwa kila noti inayopitia kwako utaichana kuepuka chuma ulete, jirani yako naye afanye hivyo keshokutwa tutakuwa na watu milioni 10 kwenye nchi wachanaji pesa. Je, kesho ya pesa zetu itakuwaje?
Eti machinga nae apokei pesa mkononi anakwambia umtupie chini au mahali pachafu eti ndo aokote sijuhi utamuibia nyota mara sijuhi nini itakuwa nini.
Hizi ni imani za kitoto kama kipindi hicho tukiwa watoto tuliaminishwa mara baada ya kukojoa hakikisha unatemea mate hili wachawi wasikuroge au ukinyoa fukia nywele usirogwe mbona siku hizi saluni tunakwenda sana na hizo nywele tunawaachia huko huko na atudhuriki na hao wanga? Haya mambo yamepitwa na wakati huu ni muda wa kufanya mambo yenye kuleta manufaa nakuachana na vitu vya dhahania.
Tafadhali tuache ujinga tufikirie vya maana kama hao wanaozitengeneza huko kwao wanazitunza na kuziheshimu wakijua nje ya kuzitumia kama medium of exchange pia pesa utambulisha taifa na utumika wakati mwingine kama kipimo cha uchumi wa nchi kwanini tusiipe matunzo stahiki?
Yangu ni hayo tu Watanzania wenzangu TUBADILIKE kuendelea kuamini imani potofu nikujidumaza na kulitia taifa lako umasikini usiyo na ulazima.
Upuuzi mtupu.Kinga nzuri dhidi ya chuma ulete
![]()
Je unaijua Chuma ulete...? Kwa kisukuma wanaita *BHUGINDU
Na je unafahamu kinga yake na zuio ili wasikuibie pesa, unga, au chochote ndani mwako....?
Dawa ya kukinga ni hii ukipata mkaa ulio dondoka njiani basi uchukue nenda kauweke kwenye kapu la pesa ukiwa pamoja na tunda lile la njano la ndulele unaviweka pamoja.
Ili huyo mwenye chuma ulete pia ili asiweze kuingia ndani kwako kukwiba unga, pesa na chochote kile basi pale mlangoni unapoingilia napo ning'iniza ndulele na huo mkaa ukiwa umeuweka pamoja au ufunge kwenye kitambaa cheusi kisha uning'inize kwa mlango wako hutokaa uone hata chuma ulete anayekuja kukwibia vitu dukani au nyumbani kwako akijaribu ataumbuka mchana kweupe