Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Sidhani kama kuna Mtanzania ambae hajui mazuri ya Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, atapinga kwamba Magufuli hakuwa na roho ya uzalendo kwa Tanzania, alichukia ufisadi, alichukia watu ambao anawaona walikwamisha bidii zake za kuindeleza Tanzania. Hakuna Mtazania atakaepinga kwamba Magufuli alikuwa mchapa kazi kweli kweli, mwenye kupenda nchi yake na raia wa Tanzania, mzalendo namba moja.
Lakini hilo linakukumbusha nini?
Linatukumbusha kiongozi aliewahi kuwa na hulka ya Magufuli pale Germany, Adolf Hitler. Hitler alikuwa mzalendo kweli kweli. Alisimamia Germany na kuifanya Germany kuwa taifa lenye uchumi wenye nguvu kuliko mataifa yote. Alipenda uzalendo, alichukia ufisadi na usaliti dhidi ya nchi yake. Hitler alikuwa muasisi wa gari za VW, Volks Wagen (People's Car) ili kila raia wa Germany aweze kumudu kuwa na gari. Hakuna kiongozi katika Germany anaeweza kusemwa alileta maendeleo kwa nchi yake kama alivyofanya Hitler, mzalendo namba moja wa nchi yake.
Lakini sasa, nani leo unamsikia akimsifia Hitler kwa makubwa aliyoifanyia Germany? Hakuna, kwa sababu hakuna mtu aliyesahau machungu yaliyosababishwa na Hitler.
Hakuna mtu hapa Tanzania asiyejua machungu yaliyoletwa na Magufuli katika azma yake ya kuiendeleza Tanzania, machungu ambayo hayana utetezi hata uyaangalie kwa mtazamo upi. Hayana justification.
Hata hivyo, kwa tulio hai, kuwachukia Hitler au Magufuli, ambao tayari wamekufa, ni dalili kwamba tuna matatizo ya afya ya akili, tunahitaji psychiatric help. Kuwasifia pia ni tatizo, kwa sababu tunaumiza wale walioumizwa nao, ambao bado wapo hai pamoja nasi. Tutapanda gari za VW za Hitler, tutapita kwenye flyover za Magufuli, lakini hatutaimba sifa zao.
Kama Germany ilivyoamua kumsahau Hitler pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yake, Tanzania tunapaswa kumsahau Magufuli pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yetu.
Tuangalie mbele sasa. Tusahau yaliyopita, tuachane na kulinganisha uongozi wa sasa na uliopita. Tuvunje magenge. Tuanze upya.
The world and your country need YOU now, not Hitler, not Magufuli.