Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

Tungemsahau kama Serikali ya Samia isingeyakumbatia majizi Sugu!! Yaani Mwigulu ni Waziri wa fedha kabsaa halafu tumsahau Mzalendo Magufuli? Makamba na Nape kabsaa!!! Haoana hapana lazima tutabaki na Magufuli katika mioyo yetu
Kuendelea kumkumbuka Magufuli na kumlinganisha Samia na Magufuli, kunatatua tatizo la kuwa na hao majizi katika serikali ya Samia?
 
Hapana. Tutakusahau kwa faida ya Tanzania! Lolote linakalotokea baada ya wewe kuondoka tuta deal nalo katika mazingira yaliyopo. Hatutalia kwamba tuna mafisadi kwa sababu Magufuli hayupo - kwa kuwa hilo halituondolei mafisadi. Tunapaswa ku-deal nao sasa, bila kumtaja Magufuli.
Kipimo cha ubaya ni uzuri. Kwa mabaya kwenye uongozi wa Samia hakuna namna lazima tuyakumbuke mazuri ya Magufuli.

Kitendo tu cha huyu mama kuwauzia bandari na mbuga Waarabu ndo kaharibu big time. Kafanya mambo ambayo hata Rais dhaifu kuliko wote(jk) hakuyafanya. Muda utasema
 
Kwa hii bumunda iliyopo madarakani tunaanzaje kumsahau?
IMG-20240409-WA0000.jpg
 
Magufuli ni sehemu ya historia ya Tanzania. Huwezi kukwepa kumtaja.

Umpende, usimpende, ni historia.

Historia haikwepeki.
Hitler ni sehemu ya historia ya Germany. Anatajwa katika historia ya Germany, sio katika kuiendeleza Germany. Acha Magufuli awe historia pia, hilo sijakataa.
 
Inawezekana ndio. Katika vita za wenyewe kwa wenyewe, kumbuka sababu ni uzalendo. Raia wanauwawa, wanawake nk, kwa jina la uzalendo. Kwa hiyo uzalendo hauangalii logic, na kuna wakati unatoka nje ya kuwa reasonable. Uzalendo (patriotisn, nationalism) mara nyingine unahalalisha kuua wale ambao wanaonekana sio wazalendo, tena mara nyingine kwa mateso sana.

Katika kupigania haki na usawa Afrika Kusini, wale waliojiona wazalendo waliona ni halali kuwachoma moto watu wengine kwa kutumia tairi shingoni kwa sababu kushirikiana kwao na makaburu kuliona kuwa sio uzalendo. Na japo waliofanya hivyo walijulikana baada ya uchaguzi wa 1994, hadi leo wanaonwa kuwa wazalendo waliopigania haki na usawa
Uzalendo ni nini?

Unataka kuhalalisha ujinga wowote na kichaa chochote kwa kutumia mwamvuki wa uzalendo?

Ukibeti mali zote za taifa lenu kwenye odds mbaya sana za kushindwa kabisa ukazipoteza mali zote, unaweza kusema ume bet hivyo kwa sababu ya uzalendo?
 
Huyo mwamba hawezi kusahaulika aba dana. Watanzania wanampenda kwa kazi nzuri aliyoifanya kipindi cha uhai wake. Rip Jpm daima utabaki mioyoni mwetu.
 
Kipimo cha ubaya ni uzuri. Kwa mabaya kwenye uongozi wa Samia hakuna namna lazima tuyakumbuke mazuri ya Magufuli.

Kitendo tu cha huyu mama kuwauzia bandari na mbuga Waarabu ndo kaharibu big time. Kafanya mambo ambayo hata Rais dhaifu kuliko wote(jk) hakuyafanya. Muda utasema
Sasa hilo jambo ndilo tunapaswa kushughulikia, na it has nothing whatsoever to do with Magufuli. Huhitaji kumtaja Magufuli kutatua matatizo anayosababisha mama, kama umeweza kuyaona tayari
 
Hitler ni sehemu ya historia ya Germany. Anatajwa katika historia ya Germany, sio katika kuiendeleza Germany. Acha Magufuli awe historia pia, hilo sijakataa.
Kwanza kabisa, Hitler ni sehemu ya historia ya dunia, alitaka kutawala dunia, akaanzisha vita ya pili ya dunia, si historia ya Germany tu.

Pili, huwezi kutenganisha historia na maendeleo. Ili uendelee inabidi uijue historia yako uendeleze mazuri, usirudie mabaya.
 
Ukidhani kwamba kumtaja taja Magufuli kutamfanya Samia aogope na kurekebisha hayo mambo kwenye hiyo list, basi wewe ndio tatizo katika nchi hii, sio Raisi Samia kama unavyosema
Angalau angeweza kuiga utendaji wa mtangulizi wake hata kwa 40% tusingefika hapa tulipo
 
Angalau angeweza kuiga utendaji wa mtangulizi wake hata kwa 40% tusingefika hapa tulipo
Mpe viwango vya kupima utendaji wa kazi kama raisi bila kumtaja Magufuli halafu ndio um-judge kufaulu au kufeli kwake. Hilo haliwezekani?

Nilipokuwa UDSM, sikuambiwa ili ufaulu lazima uwe kama Palamagamba Kabudi, upate first class kama Prof. Kabudi. Sikuhitaji mtu anitajie Kabudi ili nifaulu mitihani yangu.
 
Kwanza kabisa, Hitler ni sehemu ya historia ya dunia, alitaka kutawala dunia, akaanzisha vita ya pili ya dunia, si historia ya Germany tu.
Magufuli pia alitaka kuiweka Tanzania katika top tena za dunia. Kuifanya donor country. Kumbuka malengo yake? Dar es Salaam iwe kama Ulaya.
 
Watanzannia wanapaswa kusahahu Utumwa mamboleo....
20141018_MAP004_0.jpg


Uangamizaji wa Wamaasai

Uuzwahinwa Bandari n.k n.k

Itoshe Kusema, Tanzania haijawahi kuwa kama Nchi ya Kijerumani na J.P. Magufuli, Hayat Rais wa JMT hakuwahi kuwa Dikteta. Kwa lugha nyingine, aliyoyafanya Magufuli hayawezi kulinganishwa na yaliyofanywa na Hitler hata siku moja.

Mama yenu kauza Nchi kwa Wajomba.
 
Watanzannia wanapaswa kusahahu Utumwa mamboleo....
20141018_MAP004_0.jpg


Uangamizaji wa Wamaasai

Uuzwahinwa Bandari n.k n.k

Itoshe Kusema, Tanzania haijawahi kuwa kama Nchi ya Kijerumani na J.P. Magufuli, Hayat Rais wa JMT hakuwahi kuwa Dikteta. Kwa lugha nyingine, aliyoyafanya Magufuli hayawezi kulinganishwa na yaliyofanywa na Hitler hata siku moja.

Mama yenu kauza Nchi kwa Wajomba.
Kuna kumsahu Magufuli, na kusahu historia. Hakuna mahali nimesema tusahau historia ya Tanzania. Usichanganye haya mambo mawili.
 
Umefananisha Simba na Nyani.

Mifano yako Haina uhusiano sawa.

JPM awe kama Hitler kweli? Au unahadithi za vijiweni?
Unafananisha sura au philosophy? Mie niko kwenye mentality, na usije ukaniambia mbona Magufuli hakuanzisha gari kama Hitler. Nitakuambia nenda shule kasome.
 
Sasa hilo jambo ndilo tunapaswa kushughulikia, na it has nothing whatsoever to do with Magufuli. Huhitaji kumtaja Magufuli kutatua matatizo anayosababisha mama, kama umeweza kuyaona tayari
Mkuu,

Mimi huwa napenda kufanya "immanent critique". Yani kupinga kwa kuanza kukubaliana nawe, hata pale ambapo sikubaliani nawe, ili kuonesha ukubwa wa makosa yako, hata kama nataka kukubaliana nawe. Kuonesha internal contradictions katika hoja zako hata kama nataka kuanza kukubaliana nawe.

Hata kama nataka kukubaliana nawe kwamba Magufuli alikuwa rais mzuri (kitu ambacho sikubaliani nacho), Magufuli ali fail kuweka mabadiliko ya kimsingi ma kimfumo kuzuia mabaya anayoyafanya Samia.

Magufuli ndiye aliyesisitiza ukubwa wa Rais na kuponda utawala wa sheria.

Hata pale alipofanya marekebisho ya sheria kuweka ulinzi wa rasikimali za kitaifa kishwria, hakuondoa mfumo wa rais mwenye nguvu sana na uchawa uliosababisha Samia aweze kurudi bungeni na kutengua sheria hizo.

Tena Magufuli alikuwa anasema kabisa kwamba inawezekana rais anayekuja akaharibu mambo, lakininas long as yeye ni rais hatakubali mambo yaharibike. Hiyo ni kauki ya rais ambaye amekubali kuwa hawezi kuweka mfumo endelevu. Rais asiyeele2a kuwa urais ni taasisi na si mtu mmoja.

Hilo ni tatizo, hata kwa anayekubali mazuri ya Magufuli niblazima aone kuwa Magufuli hakuwa broad minded enough kuweka mabadiliko ya kimfumo, alikuwa anacheza na akiki za watu tu kufanya maigizo ya mabadiliko wakati kwenye mambo ya msingibkama katiba mpya kakataa mabadiliko.

Na ikiwa kuna mambo ya kimsingi Rais akikosea anakuwa si Rais mzuri, na hili la kujenga mambo endelevu ni miongoni mwa hayo, basi Rais Magufuli hawezi kuepuka lawama kwenye madudu yanayoendelea leo.
 
Sidhani kama kuna Mtanzania ambae hajui mazuri ya Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, atapinga kwamba Magufuli hakuwa na roho ya uzalendo kwa Tanzania, alichukia ufisadi, alichukia watu ambao anawaona walikwamisha bidii zake za kuindeleza Tanzania. Hakuna Mtazania atakaepinga kwamba Magufuli alikuwa mchapa kazi kweli kweli, mwenye kupenda nchi yake na raia wa Tanzania, mzalendo namba moja.

Lakini hilo linakukumbusha nini?

Linatukumbusha kiongozi aliewahi kuwa na hulka ya Magufuli pale Germany, Adolf Hitler. Hitler alikuwa mzalendo kweli kweli. Alisimamia Germany na kuifanya Germany kuwa taifa lenye uchumi wenye nguvu kuliko mataifa yote. Alipenda uzalendo, alichukia ufisadi na usaliti dhidi ya nchi yake. Hitler alikuwa muasisi wa gari za VW, Volks Wagen (People's Car) ili kila raia wa Germany aweze kumudu kuwa na gari. Hakuna kiongozi katika Germany anaeweza kusemwa alileta maendeleo kwa nchi yake kama alivyofanya Hitler, mzalendo namba moja wa nchi yake.

Lakini sasa, nani leo unamsikia akimsifia Hitler kwa makubwa aliyoifanyia Germany? Hakuna, kwa sababu hakuna mtu aliyesahau machungu yaliyosababishwa na Hitler.

Hakuna mtu hapa Tanzania asiyejua machungu yaliyoletwa na Magufuli katika azma yake ya kuiendeleza Tanzania, machungu ambayo hayana utetezi hata uyaangalie kwa mtazamo upi. Hayana justification.

Hata hivyo, kwa tulio hai, kuwachukia Hitler au Magufuli, ambao tayari wamekufa, ni dalili kwamba tuna matatizo ya afya ya akili, tunahitaji psychiatric help. Kuwasifia pia ni tatizo, kwa sababu tunaumiza wale walioumizwa nao, ambao bado wapo hai pamoja nasi. Tutapanda gari za VW za Hitler, tutapita kwenye flyover za Magufuli, lakini hatutaimba sifa zao.

Kama Germany ilivyoamua kumsahau Hitler pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yake, Tanzania tunapaswa kumsahau Magufuli pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yetu.

Tuangalie mbele sasa. Tusahau yaliyopita, tuachane na kulinganisha uongozi wa sasa na uliopita. Tuvunje magenge. Tuanze upya.

The world and your country need YOU now, not Hitler, not Magufuli.
Wakitaka Magufuli asahaulike;

1. Wahakikishe wanachukia RUSHWA!!

2. Wahakikishe wanawahurumia wananchi wa kipato Cha chini.

3. Wahakikishe maoni ya wananchi yanasikilizwa.

4. Wahakikishe pesa za umma hazicheziwi Wala kuibwa, na miradi ikamilike Kwa wakati.

Hapo atasahaulika, tofauti na hapo, KITI hicho hakitakalika.
 
Back
Top Bottom