Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

Kuwa na roho mbaya na kufikiria kuua au kuumiza yeyote anayepingana na mawazo yako sio uzalendo au kujifanya wewe mungu mtu huo sio uzalendo.
Mtu ukiwa katili hata mema yako yanaonekana upuuzi tu.
 
Sidhani kama kuna Mtanzania ambae hajui mazuri ya Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, atapinga kwamba Magufuli hakuwa na roho ya uzalendo kwa Tanzania, alichukia ufisadi, alichukia watu ambao anawaona walikwamisha bidii zake za kuindeleza Tanzania. Hakuna Mtazania atakaepinga kwamba Magufuli alikuwa mchapa kazi kweli kweli, mwenye kupenda nchi yake na raia wa Tanzania, mzalendo namba moja.

Lakini hilo linakukumbusha nini?

Linatukumbusha kiongozi aliewahi kuwa na hulka ya Magufuli pale Germany, Adolf Hitler. Hitler alikuwa mzalendo kweli kweli. Alisimamia Germany na kuifanya Germany kuwa taifa lenye uchumi wenye nguvu kuliko mataifa yote. Alipenda uzalendo, alichukia ufisadi na usaliti dhidi ya nchi yake. Hitler alikuwa muasisi wa gari za VW, Volks Wagen (People's Car) ili kila raia wa Germany aweze kumudu kuwa na gari. Hakuna kiongozi katika Germany anaeweza kusemwa alileta maendeleo kwa nchi yake kama alivyofanya Hitler, mzalendo namba moja wa nchi yake.

Lakini sasa, nani leo unamsikia akimsifia Hitler kwa makubwa aliyoifanyia Germany? Hakuna, kwa sababu hakuna mtu aliyesahau machungu yaliyosababishwa na Hitler.

Hakuna mtu hapa Tanzania asiyejua machungu yaliyoletwa na Magufuli katika azma yake ya kuiendeleza Tanzania, machungu ambayo hayana utetezi hata uyaangalie kwa mtazamo upi. Hayana justification.

Hata hivyo, kwa tulio hai, kuwachukia Hitler au Magufuli, ambao tayari wamekufa, ni dalili kwamba tuna matatizo ya afya ya akili, tunahitaji psychiatric help. Kuwasifia pia ni tatizo, kwa sababu tunaumiza wale walioumizwa nao, ambao bado wapo hai pamoja nasi. Tutapanda gari za VW za Hitler, tutapita kwenye flyover za Magufuli, lakini hatutaimba sifa zao.

Kama Germany ilivyoamua kumsahau Hitler pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yake, Tanzania tunapaswa kumsahau Magufuli pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yetu.

Tuangalie mbele sasa. Tusahau yaliyopita, tuachane na kulinganisha uongozi wa sasa na uliopita. Tuvunje magenge. Tuanze upya.

The world and your country need YOU now, not Hitler, not Magufuli.
Kati ya watu wameongea kitu cha maana ni wewe watu wamebaki kuzungumzia mzoga kila siku unatusaidia nini mama ni Bora maraelfu ya maguful
 
Mkuu tafuta maandiko kuhusu Germany (19th&20th centuries), Hitler, the NAZI Party na the SS ujielimishe kikamilifu kuhusu unachoongea.

Halafu nenda taratibu na dhana ya uzalendo. Hiyo ni propaganda illusion inayotumika sana na madikteta kuwamaliza mahasimu wao.
Sijajua unachotaka kusema hapa, kwamba Hitler hakuua Wajerumani wenzake kwa kisingizio cha uzalendo? Soma hapa chini;

Adolf Hitler is known to have ordered the execution of fellow Germans. There were several instances where Hitler ordered the killing of Germans who he perceived as threats or enemies:
  • Night of the Long Knives: In this event, Hitler ordered a bloody purge of his own political party, assassinating hundreds of Nazis whom he believed had the potential to become political enemies in the future.
  • Attempted Coup: Several German military commanders plotted to remove Hitler from power to negotiate a more favorable peace as they acknowledged their imminent defeat. However, their attempts to assassinate Hitler failed, and in his reprisals, Hitler executed over 4,000 fellow countrymen.
  • The Holocaust: While the primary victims of the Holocaust were six million Jewish men, women, and children, it’s important to note that many of these Jews were also German citizens. The Holocaust also targeted other groups, including Slavs, Roma, gay people, Jehovah’s Witnesses, and others
 
Kwahiyo Magufuli ndiye Rais WA Kwanza, makosa yake ni ku-crake down rushwa siyo na kuwaudhi wakubwa

Sent from my Nokia C10 using JamiiForums mobile app

Nani kasema Magufuli ni rais wa kwanza? Rais wa kwanza katika nini? Kwani rais wa kwanza tu ndiye anayetakiwa kukumbukwa?

Hili ni swali au statement?

Maana umeanza kama swali ukamalizia kama statement hata kukuelewa vigumu.
 
Sijajua unachotaka kusema hapa, kwamba Hitler hakuua Wajerumani wenzake kwa kisingizio cha uzalendo? Soma hapa chini;

Adolf Hitler is known to have ordered the execution of fellow Germans. There were several instances where Hitler ordered the killing of Germans who he perceived as threats or enemies:
  • Night of the Long Knives: In this event, Hitler ordered a bloody purge of his own political party, assassinating hundreds of Nazis whom he believed had the potential to become political enemies in the future.
  • Attempted Coup: Several German military commanders plotted to remove Hitler from power to negotiate a more favorable peace as they acknowledged their imminent defeat. However, their attempts to assassinate Hitler failed, and in his reprisals, Hitler executed over 4,000 fellow countrymen.
  • The Holocaust: While the primary victims of the Holocaust were six million Jewish men, women, and children, it’s important to note that many of these Jews were also German citizens. The Holocaust also targeted other groups, including Slavs, Roma, gay people, Jehovah’s Witnesses, and others
Bandiko #9 umeandika:

Wa-Germany aliowaua Hitler, aliwaona kuwa sio wazalendo, wasaliti.

Kwa hiyo uliyobandika hapa ndio kuhusu hao Hitler aliowaua kwa kuwaona si “wazalendo”?

Halafu ulipoamua kuweka hili bandiko ulikuwa hujaona uzito wa Holocaust? Umemuita Hitler mzalendo na kumfananisha na Magufuli! Seriously?

Kwangu mimi neno “uzalendo” ni ghilba ya kipuuzi na Magufuli alikuwa janga. Lakini kumfananisha Magufuli na Hitler ni wendawazimu usiomithilika. Completely incomprehensible! I’m very very sorry kwa kusema hivyo.

Kumzungumza mtu aliyeleta maangamizi ya kiwango cha holocaust ndani ya maafa ya WW2 kama vile ni mtawala wa kawaida wa nchi, tena “mzalendo” haina namna ya kuelezea!
 
Wewe hujaelewa. Holocaust haiondoi uzalendo wa Hitler. Hapa nilichotaka kuonyesha ni kwamba unaweza kuwa na kiongozi mwenye mentality kali ya uzalendo lakini bado akaumiza watu, pamoja na kuua watu wa taifa lake mwenyewe kwa kisingizio cha uzalendo.

Sasa kama unataka kuanzisha definition ya uzalendo ambayo haitii ndani matendo mabaya kama uuaji, hilo ni suala jingine. Mzalendo anaweza akawa haibii nchi yake, sio fisadi, mchapa kazi na bado akawa muuaji wa wale ambao anaona sio wazalendo kama yeye. Sasa usichanganye maana ya uzalendo na kuwa mstaarabu.In fact, wazalendo mara nyingi wanakosa ustaarabu. Nimekupa mfano wa South Africa ambako wazalendo wapigania uhuru waliwaua wenzao waliowaona wasliti kwa kuwawashia tairi za moto shingoni. Msukumo wa Mau Mau ya Kenya ilikuwa uzalendo, lakini unajua walichofanya?

Mengistu Haile Mariam wa Ethiopia alikuwa mzalendo kwa taifa lake? Ndio, sana tu. Lakini alikuwa muuaji mkubwa wa watu wake
 
Sijajua unachotaka kusema hapa, kwamba Hitler hakuua Wajerumani wenzake kwa kisingizio cha uzalendo? Soma hapa chini;

Adolf Hitler is known to have ordered the execution of fellow Germans. There were several instances where Hitler ordered the killing of Germans who he perceived as threats or enemies:
  • Night of the Long Knives: In this event, Hitler ordered a bloody purge of his own political party, assassinating hundreds of Nazis whom he believed had the potential to become political enemies in the future.
  • Attempted Coup: Several German military commanders plotted to remove Hitler from power to negotiate a more favorable peace as they acknowledged their imminent defeat. However, their attempts to assassinate Hitler failed, and in his reprisals, Hitler executed over 4,000 fellow countrymen.
  • The Holocaust: While the primary victims of the Holocaust were six million Jewish men, women, and children, it’s important to note that many of these Jews were also German citizens. The Holocaust also targeted other groups, including Slavs, Roma, gay people, Jehovah’s Witnesses, and others
Watu wanamtajataja tu Hitler, hawajasoma historia.

Wamsome angalau William L Shirer katika "The Rise and Fall of The Third Recich" kujua unyama wa Nazism.

thirdreich.jpg
 
Kwa sababu suala la Magufuli Vs Samia linaleta mgawanyiko na makundi, hatujawa kitu kimoja. ndio maana tunapaswa kumsahau.

Hao kina Nyerere, Mkapa, Mwinyi tulishawasahau, tunachokumbuka kwa sasa ni historia zao. Na pia hawakuwa na issue za kuumiza au kufaidisha kama ilivyokuwa kwa Magufuli, kiasi kwamba vifo vyao vionwe kuwa sherehe kwa baadhi ya watu. Wewe ulishasikia katika zama hizi za Samia kuna watu wa kundi la Nyerere?
Samia hana jinsi kikombe cha Magufuli hakiwezi kumuepuka.
Sababu kwanza kabisa uwepo wake hapo alipo ulisababishwa na Magufuli.
Hatujawahi kumchagua Samia kwa sera zake ila yupo hapo kwa sera za Magufuli.
Ndio maana mapungufu ya utawala huu yana semwa kwakulinganisha na utawala wa aliyemrithisha. Sababu haswa tulitegemea kuwa Samia na Magufuli ni wamoja na sera zao ni moja.
Akigombea uchaguzi ujao kwa sera zake na akashinda hapo atakuwa kaufunika mzimu wa Magufuli automatically.
Hatupaswi kuzuia watu kumtaja Magufuli, ni shujaa wetu kwa kipindi hiki mpaka pale atakapokuja mtu wa kumfunika.
 
Uzalendo ni dhana inayobidi kurejewa na kuangaliwa kwa kina.

Hitler alikuwa mzalendo?

Ukianzisha vita ya kijinga itakayoifanya nchi yako iangamizwe na watu wako wengi kuuawa, ukawabagua raia wa nchi yako wengi na kuwaua, je, wewe ni mzalendo?
Mkuu,
Ni vyema kua na true color kuliko kua mnafik na mzandik..

Magufuli na aldolf waliita koleo Ni koleo hawakuita kijiko kikubwa..

Atleast,
Kuna mtu aliishi maono yangu na kuwaonesha show sio mwingine Ni JPM
Japo Kuna mambo nilipingana nae Ila kwa asilimia kubwa Mimi Nina elements za umagufuli na nilisha ambiwaga na wengi 😊 for sure Kuna watu ambao akili zao hazipo sawasawa Ni jukumu letu kuwasaidia kuamua kwa niaba yao..

Zawadi ya kitabu kizuri Adolf Hitler alituachia..
*Mein Kampf (my struggle)

Ingependeza pia JPM na yeye angetuachiaga kitabu Cha Maisha yake alicho andika mwenyewe kwa faida ya vizazi vijavyo
 
Okay. Tuseme ukweli. Kumtajataja Magufuli, inatusaidia matatizo yetu kwa namna yeyote ile, au inayafanya yawe makubwa zaidi?
 
Mkuu,
Ni vyema kua na true color kuliko kua mnafik na mzandik..

Magufuli na aldolf waliita koleo Ni koleo hawakuita kijiko kikubwa..

Atleast,
Kuna mtu aliishi maono yangu na kuwaonesha show sio mwingine Ni JPM
Japo Kuna mambo nilipingana nae Ila kwa asilimia kubwa Mimi Nina elements za umagufuli na nilisha ambiwaga na wengi 😊 for sure Kuna watu ambao akili zao hazipo sawasawa Ni jukumu letu kuwasaidia kuamua kwa niaba yao..

Zawadi ya kitabu kizuri Adolf Hitler alituachia..
*Mein Kampf (my struggle)

Ingependeza pia JPM na yeye angetuachiaga kitabu Cha Maisha yake alicho andika mwenyewe kwa faida ya vizazi vijavyo
Hapana mkuu,

Magufuli na Hitler wote walikuwa na unafiki kama wanasiasa wengine.

Kuna kipindi Hitler alikuwa Finland kwenye sehemu fulani ya mikutano, baada ya kitu kama conference, sasa hakujua kuwa zile mic za kumrekodi bado zinamrekodi, akawa anatoa mawazo yake akifikiri harekodiwi anaongea na mwenzake tu, kumbe alikuwa anarekodiwa, alichosema hapo kilionekana tofauti na alivyojionesha publicly, si alichosema tu, mpaka sauti yake.

Magufuli ndiyo kabisa alikuwa na show kuliko za Kanumba.

View: https://youtu.be/WE6mnPmztoQ?si=PptFN-GzYX1sGOLB
 
Wewe hujaelewa. Holocaust haiondoi uzalendo wa Hitler. Hapa nilichotaka kuonyesha ni kwamba unaweza kuwa na kiongozi mwenye mentality kali ya uzalendo lakini bado akaumiza watu, pamoja na kuua watu wa taifa lake mwenyewe kwa kisingizio cha uzalendo.

Sasa kama unataka kuanzisha definition ya uzalendo ambayo haitii ndani matendo mabaya kama uuaji, hilo ni suala jingine. Mzalendo anaweza akawa haibii nchi yake, sio fisadi, mchapa kazi na bado akawa muuaji wa wale ambao anaona sio wazalendo kama yeye. Sasa usichanganye maana ya uzalendo na kuwa mstaarabu.In fact, wazalendo mara nyingi wanakosa ustaarabu. Nimekupa mfano wa South Africa ambako wazalendo wapigania uhuru waliwaua wenzao waliowaona wasliti kwa kuwawashia tairi za moto shingoni. Msukumo wa Mau Mau ya Kenya ilikuwa uzalendo, lakini unajua walichofanya?

Mengistu Haile Mariam wa Ethiopia alikuwa mzalendo kwa taifa lake? Ndio, sana tu. Lakini alikuwa muuaji mkubwa wa watu wake
I hope hii itakuwa comment yangu ya mwisho kwako.

Mzalendo mwenye “mentality kali”, “aliyekosa ustaarabu”? Anayeumiza na kuua raia wake wanaomkosoa kwa maamuzi mabaya yanayotia hasara taifa? Au matendo yake yanayokiuka haki za raia wasio na hatia (innocents)? Au wanafichua matendo yake ya kifisadi? Kwako hiyo ni sawa?

Wewe unaweza kudai kuwa Hitler na Magufuli unaowalinganisha hawakuwa mafisadi wala hawakuwahi kuibia nchi zao ikiwa ni pamoja na kufuja fedha za umma kwa matumizi yasiyozingatia sheria, kanuni, na taratibu za manunuzi?

Kama wewe ni supporter wa dictators na dictatorships, basi sawa. Unaeleweka.
 
Hapana mkuu,

Magufuli na Hitler wote walikuwa na unafiki kama wanasiasa wengine.

Kuna kipindi Hitler alikuwa Finland kwenye sehemu fulani ya mikutano, baada ya kitu kama conference, sasa hakujua kuwa zile mic za kumrekodi bado zinamrekodi, akawa anatoa mawazo yake akifikiri harekodiwi anaongea na mwenzake tu, kumbe alikuwa anarekodiwa, alichosema hapo kilionekana tofauti na alivyojionesha publicly, si alichosema tu, mpaka sauti yake.

Magufuli ndiyo kabisa alikuwa na show kuliko za Kanumba.

View: https://youtu.be/WE6mnPmztoQ?si=PptFN-GzYX1sGOLB

Asante mkuu nimeisikiliza yote
 
Uzalendo ni dhana inayobidi kurejewa na kuangaliwa kwa kina.

Hitler alikuwa mzalendo?

Ukianzisha vita ya kijinga itakayoifanya nchi yako iangamizwe na watu wako wengi kuuawa, ukawabagua raia wa nchi yako wengi na kuwaua, je, wewe ni mzalendo?
Uzalendo ni pamoja na Sacrifice.

Itikadi za Kisiasa Ulaya kuna Watu huuitwa ultra nationalist mfano Hitler, Trump, viongozi wa Japan kabla ya vita ya pili ya Dunia na wengine wapo Hadi Leo, jambo ambalo wazungu wanalipigania ni hao Watu wasishike Madaraka.
 
Sacrifice ni nini na kichaa ni nini?

Sacrifice ni nini na kupenda vita kijinga ni nini?

Idi Amin alitaka kuiongeza Uganda ichukue Mwanza ichukue mpaka bandari ya Tanga, akisema Uganda nayo ilitakiwa iwe na bandari baharini.

Bila ya kuwa na mpango wa kushinda vita.

Alikuwa mzalendo au kichaa tu aliyependa vita?
 
Unadhani wanaopigana vita ni wajinga?
 
Back
Top Bottom